Utumishi siwaelewi

Utumishi siwaelewi

kamba0719

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Posts
804
Reaction score
1,917
Nakumbuka kipindi cha nyuma hapa niliwahi kulalamika ,kwa nini utumishi hawanichagui.Nashukuru kuna watu waliniambia wakaniambia niende nikaonane nao ana kwa ana Maktaba kuu ya taifa.Mimi nina Degree ya Telcommunication Engineering na CCNA (R&S).Nimeanza kuapply kazi kuanzia 2016 lakini sikubahatika kuitwa katika usahili hata mmoja,kuna nafasi za TCRA amabazo nilikuwa na fiti sikuitwa,kuna nafasi za TPA (Network Engineer) sikuitwa, wizara ya ardhi (Network Engineering) sitatwa.eGA na TBS zote sikuitwa ,nafasi zote hazikuwa na uhitaji wa mtu mwenye uzoefu.

Nakumbuka wiki kama tatu nyuma nilienda kukutana nao pale maktaba,bahati nzuri niakakutana na mama wa makamo,nikamuuliza tatizo langu, mbona mimi sijawahi kuitwa kwenye udahili tokea nianze kufanya application 2016.Yule mama aliangalia profile langu kalikagua akaliona lipo sawa,akangalia zile requirement za kazi ,nilizoomba akaniambia tatizo naomba nafasi za watu wa Computer Science,Software, IT.

Nikamwambia inamaana CV zetu tunazowapa hamtizami,akaniamabia wao wanaangalia kwanza kozi,nikajaribu kumueleza ya kuwa upande wa Networking hamna course inayoingia deep kama Telcom sasa mbona hata hizi mimi sichaguliwi na vilevile nina CCNA ,akanipa jibu nahisi kama limeninyong'onyesha ,aliniambia kwa post ninazo omba ni za watu wa Computer Science,IT,Software,Computer Engineering kama vipi nisubirie za TTCL (wana miaka zaidi ya mitatu siajona tangazo lao la ajira),nilichoka sana.Nikaona tena nitafute shughuli nyingine ya kufanya.

Baadaye nikaja gundua si mimi peke yangu nina jamaa yangu mmoja tulipiga nae project kwenye kamapuni za minara ana Diploma ya Electronics and Telecommunication Engineering na Degree ya Electronics and Communication ,kumbe nae ana tatizo kama langu ,ila yy aliitwa interview moja ya Business analyst basi lakini tokea 2015 kila akiapplya anakosa hata hii ya juzi ya TBS ilikuwa ikitaka mtu kama yeye (haina experince) hakuitwa.Sasa pata picha una mwita mtu udahili wa Business analyst,lakini katika sehemu anayofiti kabisa ya TBS humwiti hamuoni kama kuna walakini.

Nimeziona nafasi hizi za TAMISEMI nimezitamani sana na nyingi upande wa network administrator,lakini nikiangalia kutokana na majibu ya yule mama naona bora niache na nafasi zipo zaidi ya 20.Labda nilikuwa naomba ushauri labda niende ngazi gani ya juu ili niweze saidiwa manake nimechoka na hizi tempo za kuungaunga.
 
Hawa majamaa siyo aseee, Jana wametangaza kazi za TPA Leo hii ukiangalia wameshazitoa wamebakiza kazi zilizotangazwa siku za nyuma, hivo hivo na zile za tamisemi kwa watu wa IT hazipo tena washaondoa....waweza jiuliza je wametangaza ushahidi tuuu ama ndiyo kusemaje.
 
Mbona nimeangalia mda huu zipo.
 
Attachments

  • Screenshot_20181128-204417.png
    Screenshot_20181128-204417.png
    28 KB · Views: 117
kamba0719 Mimi ningekuwa wewe ningeenda hapo DIT nikachukuwa Computer Engineering Degree ili niwakomeshe!!!
Sijafikiria kusoma master,ila mimi sasa hivi nahangaika na Programming,ili inisaidie katika maswala ya Network automation ,ujue kusoma sana wakati hivi vyenyewe bado hujavifanyia kazi practical naona itakuwa si vizuri sana na hata kama nikisoma basi nitasomea Network Engineering.
 
Mbona mi nmemaliza mwaka Jana, nimeomba Mara moja ajira portal na nkapata kazi. MUNGU kanisaidia.
Kila mtu ana bahati yake ,mimi mwenzio nipo kizani sielewi na majibu sina.
 
Mda mwingine ukubali mkuu, watu walioitwa wamekuzidi.
Duu Telcom mixer CCNA (pepa ngumu kuliko hizo za utumishi) ,hunijui wewe mimi sijisifii nimesoma Telcom lakini hamna eneo ninalo jiamini kama Networking,alafu wanaoitwa wengi ni rafiki zangu na uwezo wao wakawaida ila tatizo lipo kwangu.Wewe kama umepata shukuru mungu na usijione bora,ukawaona wenzio hawafai ,acha kejeli kwani hunijui mimi.
 
kama kazi inasema degree in IT/COMPUTER SCIENCE,MTU WA TELECOM UKIOMBA HUITWI,UTUMISHI WAKO VERY SENSITIVE KWENYE COURSE ULIYO SOMA,
 
Jaribu bahati yako tena, Round hii huwezi kujua Mungu atakubariki
 
kama kazi inasema degree in IT/COMPUTER SCIENCE,MTU WA TELECOM UKIOMBA HUITWI,UTUMISHI WAKO VERY SENSITIVE KWENYE COURSE ULIYO SOMA,
Lakini sasa CV tunaituma ya nini,alafu Telcom networking anacover karibia layer zote 7,kama umesoma Telcom au una mtu unayemjua wa telcom utanielewa,hamna course inayoingia deep katika Networking kama Telcom.Sasa nashangaa nakosaje nafasi ya Network Engineering na Network Administrator.
 
utumishi hawako na Cv sana,nasema hvyo mm ,nimesoma computer science hakuna interview ya utumishi ambayo sijawahi itwa ni vile tu siendagi,wana angalia course uliyo soma kama kwenye tangazo la kazi iliandikwa.Kama wanataka mtu wa It na computer science hata wa info system ila telecom hapana.cha kuuliza hao marafiki zako wanao itwa mmesoma wote telecom ama wao wamesoma course zingine
 
" similar field " Wanaiwekaga ya nini.Mimi silalamiki nisichokijua,hichi ninacholalamika nina kijua.Sasa dada yangu juzi wametoa nafasi TBS wanataka mtu wa Electronics and Telecommunication Engineering ,huwezi amini mpaka hapa napo sijaitwa na rafiki yangu ambaye amesoma Electronics and Telecommunication Engineering hajaitwa nae na nafasi haikuhitaji mtu mzoefu, sasa mimi najiuliza wanatumia kigezo gani.
 
swali?
1.ume-certify vyeti vyako?
2.ukituma application unakumbuka kuweka saini yako?
 
Pamoja na ushauri wa huyo Mama, nakushari uangalie kama attachment za vyeti zote zipo! Kuna mtu alikuwa na same problem! Kumbe certificate ya chuo haionekani kwenye system ipo transcript tu! Wakawa wanampiga chini mara zote!
 
Back
Top Bottom