Kiraka Kikuu
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 5,903
- 1,983
- Thread starter
-
- #41
Tuliambiwa na kaka yetu kuwa ukitaja nyoka usipotema mate na kusema "Mungu pishia mbali sio mimi niliyesema ni mchawi" nyoka atatokea na kukung'ata. Basi kaka yetu mkubwa akawa anatutesa kweli mimi na mdogo wangu. Anakuja mbele yetu na kusema nyoka, nyoka, nyoka mara nyingi tu. Sisi kwa ajili ya imani kuwa nyoka atatokea tulikuwa tukitema mate na kusema hayo maneno hapo juu. Kwa kila mtajo mmoja wa nyoka tulikuwa tukitema mate na kusema hayo maneno. Basi kaka yetu anaweza kutamka hilo neno mfululizo hata mara 50. Tulitema mate hadi yanakauka mwisho tunalia na kumkimbilia mama tukidai kaka anatuchokoza, anataka nyoka waje. Utoto jamani! Lakini natamani nirudie utoto mie!
ili uwe na meno meupe ukiona nyange nyange imba nyange nyange nipe meno meupe
ukila huku umelala mama yako anakufa
ukimruka aliyekaa au kulala bac yule uliyemruka atakua mfupi.
ukimchungulia mtu anajisaidia mama yako anakatika titi.
nilikua nikimwona mtoto wa punda mbiooo..
kwenda kuoga kisimani then tunacheza mpaka giza then ha2ogi, kipigo cha hapo usisme...
enzi hizo hakuna shida,kila christmass lazima ulilie nguo mpya...dah!sasa ivi majukumu nyomi na mimi naliliwa nguo na Evergreen "the boss"kumbe ndo maana Jd aliimba nataman kuwa kama mtoto,aliona mbali sana.hahaha!!
Hiyo ya kukataa kuoga watu karibu wote tumepitia...
Sijui shida ninini!
enzi hizo hakuna shida,kila christmass lazima ulilie nguo mpya...dah!sasa ivi majukumu nyomi na mimi naliliwa nguo na Evergreen "the boss"kumbe ndo maana Jd aliimba nataman kuwa kama mtoto,aliona mbali sana.
Ukikalia Kinu utaota majipu kwenye masaburi... duuh wakubwa zetu walikuwa na mbinu za ajabu za kukukataza usifanye jambo.. Maana tulikuwa tunatahadharishana wenyewe kwa wenyewe
Nilishindwa kuvaa suruali, ilibidi dada yangu anivue suruali akimbie nyumbani kunichukulia kaptura safari ya kwenda kanisani iendelee, utoto bwana we acha tu, natamani kurudia utoto lakini ndo ishatoka hiyo.