Utoroshaji wanyama hai, Ikulu ya Kikwete yahusika

Utoroshaji wanyama hai, Ikulu ya Kikwete yahusika

...na hao waandishi wa habari (wanaoitwa sasa vidagaa) sielewi ilikuaje wakamdhamini huo dalali... yani mtu anaonyesha ni mpiga dili wa kimataifa, wapi na wapi hao waandishi wa habari kumdhamini? Pia nashangaa, kwani uandishi wa habari (investigative journalism) si ni kama act of policing tu? sasa wapi na wapi kumdhamini mtu mnae muhisi anahusika na uhalifu?
Hao waandishi nao walikuwa na Maslahi binafsi, mimi hata siwaonei huruma.
 
daaahhh... inasikitisha sana, yaaani hii tz mh ila walaaniwe hadi kwa Mungu wakute moto wao unawasubiri
 
Sasa tutaliondoa je ili hali hata wale wa upande wa pili nao walituletea yale yale yaliyokuwa kwenye system?

Wa upande upili wameweka wazi msimamo wao kuhusu katiba, hapo ni mahali pa kuanzia... Miaka 54 ya kujaribu imetosha mkuu.
 
Tatizo kubwa lilikuwa pale kwenye JENGO JEUPE hao Polis niwatu wakuamrishwa tu....hawa jeuri ya kukataa.....ndio maana wanufaika na Ufisadi hataki kusikia mambo ya Katiba ya wananchi...yakummulika mpangaji wa pale anapomaliza utawala wake

..kinachosikitisha ni jinsi hao wadhamini wa mshtakiwa walivyopelekwa jela, wakati mshtakiwa ametoroshwa na polisi.

..Ikulu ingeweza kabisa kumlazimisha muendesha mashtaka afute kesi, lakini siyo kuwafunga vidagaa huku vigogo wahusika wakuu wakitanua mitaani.

cc The Boss
 
Nchi ngumu sana hii....Utakuta hao wadhamini wameenda JELA hakuna chochote walichopata Waliopiga miHELA wamejifungia kwenye Magari ya Hela nyingi
 
Tanzania chini ya hiki chama kamwe siyo nchi ya kujivunia.

Hii ishu ya wanyama kutoroshwa ni cha mtoto. Ebu angalieni tu ishu ya gesi halaf hayana hata uoga na aibu yakiiba yani yameshajiaminisha yakiiba kwao ni sahihi na hayatafanywa kitu.

Tuwaache watawale
 
Ni sababu tosha za kuichukia CCM. Watu wengi watapoteza maisha kama kafara inayotolewa na CCM. Na mtaji wao wa "ujinga" na "umasikini" ambao wameuatamia hakuna wa kufurukuta. MAPAMBANO YAENDELEE
 
Katiba mpya ndio suluhisho la matatizo yote haya hakuna aliye juu ya sheria,lakini ajabu unaambiwa ata Rais hana ubavu wa kuhoji kilichotangazwa na NEC/ZEC sasa hii ni nchi ya namna gani na kama ndio hivyo mnaleta sanduku la kura mbele yetu la nini wakati matokeo mnayo tayari.
 
Hapa tunapata tathimini gani,ninani mlizi wa kweli wa nchi yetu wapendwa?
 
JK amehusika vipi hapo? Na huyo mpakistani alikua na vibali vyote na alishalipia kila kitu sasa kosa lake liko wapi? Hii ni biashara kama biashara zingine, hakuna kosa lililo fanyika hapo.
Kama hakuhusika je sakata lenyewe hakulisika na kama alilisikia alichukua hatua gani?kama hakusikia je alistahili kuwa kiongozi wa nchi?
 
Kuna uwezekano uozo tunaoujua ni mdogo sana kuliko ambao hatuujui...Na kukiwa na uhuru wa kuchunguza makandokando ya tawala hizi mbili tu za mwisho za miaka 20 itachukua miaka kama hiyo 20 kuweza kumaliza kila kitu na kila mmoja atabaki akishangaa Waafrika wenzetu kutufanyia utumwa na wizi wa hali ya juu kiasi hicho
 
Huku tunapoenda itafika mahali watu wenye Jina la Kikwete au Jecha wakatengwa na jamii
 
JK amehusika vipi hapo? Na huyo mpakistani alikua na vibali vyote na alishalipia kila kitu sasa kosa lake liko wapi? Hii ni biashara kama biashara zingine, hakuna kosa lililo fanyika hapo.
Kabla hujakurupuka kutoa comments zako ,fahamu kwanza sheria inasema nini juu ya kusafirisha wanyama
 
Wa upande upili wameweka wazi msimamo wao kuhusu katiba, hapo ni mahali pa kuanzia... Miaka 54 ya kujaribu imetosha mkuu.
Me hofu yangu ilikuja pale wale wale jamaa waliokuwa kwenye system mbovu kuanza kujikosha na wao wakakubali honestly I was very disappointed.
 
Kama hakuhusika je sakata lenyewe hakulisika na kama alilisikia alichukua hatua gani?kama hakusikia je alistahili kuwa kiongozi wa nchi?

...hujamwelewa majebere mkuu, huyu anamaanisha biashara ya kuuza wanyamapori ni halali na kwamba mali asili wanaweza wakauza hata wanyama wote huko maporini ilimradi tu mtu awe na kibali... na kwa hiyo jk hana kosa...
 
Me hofu yangu ilikuja pale wale wale jamaa waliokuwa kwenye system mbovu kuanza kujikosha na wao wakakubali honestly I was very disappointed.

Siasa za hii nchi ni mbovu sana mkuu... unayemsema kama angekuwa na makandokando hayo angekuwa amesha shughulikiwa hakuna utani...
 
Siasa za hii nchi ni mbovu sana mkuu... unayemsema kama angekuwa na makandokando hayo angekuwa amesha shughulikiwa hakuna utani...
Me kitu nilichokuwa nataka ni kuingiza watu wapya kabisa sasa walewale ndo wakajinasibu ndo wanaenda kuwafundisha kazi. Me niliona masihara.
 
Back
Top Bottom