Utofauti unatisha

Utofauti unatisha

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,566
Reaction score
2,966
Ndugu zangu tazama hii picha
1000062732.jpg


Angalia na hii
1000062733.jpg


Ivi ni kwa namna gani watu wa Spain waliweza kujenga daraja zuri namna hii miaka ya 1793 .. yaan elfu moja mia saba hukoo.. na Wafrica kufungwa fikra zetu tokea miaka hiyo ya utumwa mpaka leo.

Umasikini tulionao Africa ni mgumu sana kufahamu chanzo chake, undani wake unapita mali zionekanazo kwa macho mpaka mambo ya Rohoni. Kuna jambo tulikosea kuna kitu hakipo sawa Majira yametupita sanaa ukilinganisha na wenzetu.

Mind you huyu Spain ni mzungu wa jioni hajachangamka sana ukimlinganisha na Germany au England. Kuna kitu kibaya walifanya mababu zetu, kwani mbona watoto wa wenzetu wanaridhi vitu vizuri kiasi hiki huku sisi tukiwa hatuna cha kuonyesha. Something is Not Right, hii si sawaa na Sisi tunastahili.
 
Hiyo ni imported knowledge kutoka maeneo mbalimbali ya dunia. Chimbuko la European civilization linatisha.
 
Hebu tulia kwanza ili uweze kufikiria vyema na kwa ukubwa.

Sisi tupo kwenye kipindi cha mpito/Transition. Tunayopitia wenzetu walishayapitia pia.

Ustaarabu unaenda sambamba na maendeleo. Waliowahi kustaarabika walipata maendeleo mapema pia.
 
Ngoja waje CCM wakudanganye kwamba "Sisi" ni masikini kwa sababu mabeberu walitunyonya sana.Haujakaa vema kutafsiri aliyokueleza,atakuambia tena nchi yetu ni tajiri hadi mabeberu yanatuonea gere.Utajua wewe kama uishi na maelezo ya kwanza au ule kabunyau na kitisho cha pili.
 
Mababu zetu hawakua na akili tu mzee,haiwezekan dunian tumeanza wote kwa pamoja sio kwmb mzungu ndo alianza kabla yetu,then mpk wanafanya innovation za kujenga meli wakatufata kuja kuchukua mali ambazo hata sisi hatukujua thaman wala faida zake,above all wakatubeba kuwa watumwa wao,hii kitu hata mm huwa inanifikirisha sana.
 
Spain imetawaliwa na dola ya kiislamu kwa zaidi ya miaka 800 tizama historia ya elimu kwenye maktaba za Cordoba utaona.

Huku kwetu tizama how Europe under developed Africa.
 
Uwanja wa mpira wa Timu anayochezea yule Mghana nadhani umezungukwa na bahari na sehemu ya parking za magari ipo pembeni kama kisiwa hivi ukiwa pale utajiuliza maswali mengi hauwezi kupata jibu kama nakumbuka vizuri ni mji wa Bilbao..
 
Wafrika hawakuanzia maisha hapa kuna mahali tulikuwepo huko ndiko asili yetu, hapa tulifika kwasababu kule tulikokuwa tulivamiwa na wengi sana waliuwa hivyo sisi tulikuwa watu wa kuhamahama kuopa kuangamizwa.
 
Back
Top Bottom