Utoaji wa gari bandarini

Utoaji wa gari bandarini

fredie92

Senior Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
133
Reaction score
32
Habari zenu wakuu!!! Mimi ni kijana ambaye nafanya harakati za kutengeneza maisha mazuri... sasa napata michongo mingi ila shida muda unakuwa mdogo sana. mara nyingi natakiwa kwenda maeneo tofauti tofauti so suala la kutumia daladala lina-nicost! nikifikiria bodaboda ndo hata kupanda naogopa.

Sasa wakuu, katika bajeti yangu inayoanza mwezi ujao (ndo mwaka wangu wa bajeti unaanza), nimeona niingize suala la ka-usafiri kakunisaidia angalau hata kufika kwenye wilaya za karibu. Nataka niweke bajeti, naomba ushauri wa yafuatayo:-

  1. Niweke bajeti ya sh ngapi kwa ka-gari katakofika angalau chunya, tukuyu, tunduma (ndo maeneo ya mishe zangu kwa sasa).
  2. Napenda kuagiza nje kwani nahisi nitapata kwa bei angalau nitamudu na ili nisiharibu bajeti nzima kwani nimesikia wauzaji wa huku mjini wanaweka faida kubwa sana.
  3. nimeongea na dereve wa IT mmoja leo kaniambia kutoa gari bandarini ni $350 tu. Hii ipoje? mi sijaelewa kwani kuna uzi humu niliona kutoa gari uwe na pesa inayokaribia au kufanana na uliyonunulia + kusafirisha.

Natanguliza shukrani za dhati!

Swai
Mbeya.
 
Mkuu kawa uwezo unao jitahidi kutafuta toyota rav4 ni gari nzuri sana ukiachilia mbali forester gari ambayo nitabaki kuikubali siku zote.kuna ndugu yangu amenunua ameagiza last week kama us 6000 na tukajaribu gharama zote in total ni kama 16.5M.SUbiri waje wataalam watakupa ushauri mzuri zaidi what to do
 
Mkuu nashukuru kwa taarifa! kwa 16.5m inakuwa ipo road kabisa hiyo RAV 4? kwa sababu ni suala la bajeti na linatakiwa litekelezwe kabla ya June, 2015. ningependa nipate hata option mbili, tatu za magari na bei zake. Shukrani mkuu... ngoja niwasubili watoke kwenye sherehe mkuu...
 
Nunua Rav 4 old Model zile za 97 hadi 98 ila bei yake uwe na balance ya 14m kuagiza na kuitoa mpaka barabarani huyo dereva wa IT(Transit) labda anamaanisha gharama za kumlipa yeye kuitoa bandarini/yard hadi huko kwenu mbeya hata hivyo bei yake ni kubwa sana wengi wanafanya laki 2.
~kwa kifupi tueleze bajeti yako na tutakushauri gari gani ya kununua.
 
Mkuu KING KONG III kwa ukweli nilitaka kuweka 10M ila kwa ushauri mnaonipa naona niweke 15M nipunguze pesa kwenye bajeti zingine... sasa naomba ushauri hata wa magari mawili matatu kwa mishe hizo nijue kabla sijakaa kikao cha kuipitisha!
 
Back
Top Bottom