Utoaji mimba unaweza kuwa haki za binadamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utoaji mimba unaweza kuwa haki za binadamu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Plato, Jan 3, 2012.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Tangu mwaka 1973 Marekani kupitia case ya Roe Vs Wade utoaji mimba unaruhusiwa kisheria kama haki na uhuru wa mwanamke.kuna kliniki zinazotambulika kisheria zinazotoa watu mimba.daktari aweza kufungwa akikataa kumtoa mwanamke mimba.kwa sasa nchi karibia zote za ulaya zinaruhusu utoaji mimba kisheria,Marekani ya kaskazini yote na nchi nyingi za Marekani ya kusini.Kuna msukumo mkubwa sana kutaka Afrika nayo iruhusu utoaji mimba.Kupitia MAPUTO PROTOCOL.

  Tanzania na nchi nyingi za africa zimeidhinisha (Ratified) mkataba huo.kipengele cha 4:2c cha protocol hii kinazitaka nchi wahusika kuruhusu haki za wanawake kutoa mimba.

  Je kutoa mimba inaweza kweli kuwa haki ya mwanamke? na je kuruhusu utoaji mimba siyo kuruhusu wanawake na madaktari kuuwa watu wengine kwa sababu hao watu hawana nguvu za kujijitetea? je haki za mwanamke kuchagua zinazidi zile za mtoto kuwa na haki ya kuishi?  Nakumbuka tulivyopiga kelele kuhusu mambo ya ushoga.je kwa nini hatupigi kelele kuhusu kuambiwa turuhusu utoaji mimba? Na tujadili

   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nahisi tusikimbilie tu kuiga eti kwa sababu nani wamefanya na sisi tufanye. Mataifa ya magharibi wana tamaduni zao na sisi tuna zetu. Tunapozungumzia haki, kwanza tuangalie wajibu. Ukiwachia kesi za ubakaji na kuhatarisha afya na maisha ya mama ikiwa itathibitishwa na wataalamu, hakuna sababu ya kusema mwanamke atoe mimba kwa sababu ni haki yake. Huyu angepaswa kwanza kuangalia na kutimiza waibu wake kabla ya kupata hiyo mimba. Pitia uzi huu kwa maelezo zaidi juu ya hiki ninachokizungumza:
  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/199018-better-be-safe-than-sorry.html
   
 3. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,727
  Trophy Points: 280
  Ibara ya 14 ya SADC Gender Protocol inasema kwamba a woman has the choice to decide whether or not to have a baby and a number of baby(ies) she want..........


  Tanzania ni party katika protocol hii, ila tu haijadomesticate (ilikuja bungeni na ikakataliwa)

  Bado kuna room ya kujadili suala hili, nchi nyingi tu za Afrika hasa zle ambazo ni monolist zinaprctise legal abortion mathalan ukienda SA utakuta vibao vimeandikwa AbortionDr is available here (nimekuta hiki Pritoria na kiwingineko mm mwenyewe)
   
 4. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,727
  Trophy Points: 280
  ni kipengele cha 14
   
 5. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kutoa mimba ni suala pana, na ambalo halina jibu la moja kwa moja. Hoja ni kwamba kila mtu ana haki ya kuishi. haki hii haipaswi kuingiliwa ama kuchukiliwa na mtu yeyote (kuua). sasa issue ni kwamba maisha yanaanzia wapi....kabla ya mtu kuzaliwa (unborn baby) au baada ya kuzaliwa..... ndio tuna haki za binadamu, na haki hizo zinabeba maudhui na maadili ya binadamu, lakini pia ni kweli kwamba suala la haki za binadamu limeanzia ulaya na haki hizo zina akisi tamaduni zao. haijakubalika duniani kote kwamba haki za binadamu zina fanana au zina status sawa kwa nchi zote, ndio tulipinga ushoga kwa sababu sio sehemu ya utamaduni au maadili ya watz kwa ujumla. kuhusu kutoa mimba mwanamke ana haki ya kutoa mimba katika mazingira fulani.mfano kama amebakwa na kupewa mimba au mimba hiyo inahatariisha maisha yake...kwetu bado kutoa mimba ni kosa la jinai. tatzio ni kwamba ukirusu kutoa mimba haki hiyo inaweza kutumika vibaya (abuse of a right). unaweza kusema bora tupige marufuku kutoa mimba lakini turuhusu ufanyike katika mazingira fulani....exceptions
   
 6. K

  Kilaza Flani Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mbona lipo wazi hilo, hakuna ishu hapo ila kulazimisha mambo tu!! life starts pale mimba inapotungwa, kuanzia pale ni kiumbe, kinakua, kinamove na kinakua pia!!
   
 7. C

  CHAKUDIBUA Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuruhusu utoaji mimba ni ukiukaji wa haki za binadamu kwani mimba inapotungwa tu uhai wa binadamu ndipo unapoanza thats why kuna matukio huwa tunasikia mtoto amefia tumboni this means that maisha yanaanzia tumboni
  Kuhusu circumstance kama upatikanaji wa mimba kwa kubakwa haimanishi mwanamke atoe mimba kwani mimba hi haina tofauti na aliyepata mimba bila kukusudia.
  Kunakitu tunatakiwa kuangalia kitu kimoja je kama mimba inahatarisha maisha ya mwanamke nani aachwe hai?
   
Loading...