kudra hamidu
Senior Member
- Jul 1, 2012
- 152
- 107
Habari zenu wanajukwaa.Natumai ni wazima wa afya.Poleni na majukumu.
Leo nimekaa zangu nyumbani natafakari mawili matatu. Ghafla mwanangu wa miaka 7 akanigusa bega na kunisalimu. Baada ya salamu akaniambia kuhusu pesa ya tution(40,000) kwa mwezi. Ambayo ni nje ya ada (900,000). Bila kusahau 30,000 ya usafiri kwa mwezi. Hapo kuna gharama nyingine kama pesa ya watoto yatima 20,000 kwa mwaka. Nikiandika zote nitaanza kuchukia lugha ya kiingereza.
Kwa nini nichukie kiingereza? Ok ni kwasababu ndo lugha iliyonifaNya nimpeleke mwanangu shule za school bus.
Nimeanza kujiuliza mimi nimesoma (CBE) kwa ada ya 1.2 mill kwa mwaka (hapo msosi na usafiri juu yako) iweje mtoto wa darasa la pili au grade 2 kwa kimombo afikie zaidi ya pesa hiyo? Hata kuikaribia tu inatosha mimi kujiuliza maswali.
Wakuu nachoona mimi ni hawa wamiliki wa hizi shule wamezidi kufanya watakavyo kana kwamba hakuna serikali.
Sijui akifika hadi chuo nitatumia shilingi ngapi. Inabidi niandike kwenye daftari kama kumbukumbu. Maana mali bila daftari huenda bila habari.
WAMEZIDI!