UTEUZI: Waziri Mbarawa amteua Hamza Said Johari kuwa Mkurugenzi Mkuu TCCA

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
JAMHURI YAMUUNGANO WATANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO​

JMT.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USAFIRI WAANGA TANZANIA (TCAA)

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kwa mujibu wa Kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Usafiri wa Anga 'The Civil Aviation Act Principal Legislation Reviewed Edition 2006' amemteua Bw. Hamza Said Johari, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafrri wa Anga Tanzania (TCAA) kuanzia 22/2/2016.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Hamza Said Johari alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA Consumer Consultative Council).

Bw. Hamza Said Johari anajaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, nafasi ambayo ilikuwa ikikaimiwa na Bw. Redemptus Peter Bugomola .

Sign.jpg
Dkt. Leornard Chamuriho

KATIBU MKUU (UCHUKUZI)

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

23 Februari 2016​
==========

utezi TCAA.jpg
 
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Hamza Said Johari alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA Consumer Consultative Council).

BAKITA, binadamu wanakulaje Mamlaka ya Usafiri na Anga? Kiswahili cha wapi hiki?
 
Hamza Said... Haya waje tena na takwimu zao sijui hawana kazi za kufanya.. Mtu anakaa anaanza kukusanya takwimu kwenye mashirika ya umma kwa kutumia tu majina ya waarabu .. Akikuta nyangiswe mkoropwinyo sijui anamuweka kwenye kundi gani..
 
Naamini "malalia sugu" atalala kwa amani leo. Sijui alikula ban ya milele,simuoni hapa jukwaani. Hata hivyo ana dada yake hatari kweli kweli, yupo live hapa JF 24/7.
 
Hongera

Nenda Nawe Kafanye Kazi Acha Mihemko Ya Majipu!!!
Maana Viongozi Wa Ccm Mpaka Aibu Kila Jambo Wanasema Jipu Hata Rais Wengine Aliowateuwa Ni Majipu Ila Wanajifanya Wao Wasafi Sana
 
Naona Magufuli ametukumbuka na sisi Waislamu...... Maana tangu mwanzo amepambana kujaza makafir wenzake.
 
Back
Top Bottom