MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ndugu zangu wanaJF,
Kuna kitu nakiona si kizuri hata kidogo, Hivi ni kwanini hiki cheo au nafasi hii ya utendaji ambayo kimsingi ni ya kiongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya inashushwa hadhi kiasi hili, kwa sasa ni ukweli usiopingika ni kwamba vijana wengi wanaililia hii nafasi wakidhani ni sawa na utendaji wa mtaa!
Nishauri tu Mh Raisi kwa kuzingatia unyeti wa nafasi hii aangalie watu hawa wakati wa kuteua!Maana hawa watu hustaafu wakiwa bado ni nguvu kazi na uzoefu mkubwa kwa kuzingatia kua mkuu wa wilaya ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.Hawa watumishi binafsi naona ni muhimu kwa nafasi hizo.
1. Maafisa wastaafu waadilifu wa JWTZ
2. Maafisa wa wastaafu waadilifu wa Jeshi la polisi
3. Maafisa wastaafu waadilifu wa usalama wa taifa
4. Maafisa wastaafu waadilifu wa jeshi la uhamiaji
5. Maafisa waandamizi wa taasisi kubwa za umma ambao ni makada wa chama
6. Maafisa wastaafu wa Waadilifu Jeshi la Magereza
Kwa sababu hizi nafasi zipo kwa mujibu wa katiba basi nina imani katika majeshi haya na taasisi za umma wapo makada watiifu wa chama,wapewe nafasi hizi kwa kuzingatia weledi wao na sio kuwabebesha vijana ambao hata mgambo hawakupitia ndio maana maamuzi yanakua mabovu na migogoro hasa ya kijamii haiishi.
Vijana wapewe mikopo wafundishwe elimu za kujitegemea wakazalishe taifa lisonge mbele, kama ni kulea au kuandaa viongozi wa baadae basi walelewe kwenye chipukizi za vyama na taasisi za vyama na sio kuwalelea kwenye ukuu wa wilaya.Hii pia itapunguza uvivu wa baadhi ya vijana kukaa vijiweni kuwaza nafasi hizi huku hawafanyi kazi.