Uteuzi wa Wakuu wa Mkoa umekaa kimkakati, Hongera sana Rais Samia

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,638
Nimpe Hongera Rais wetu mama Samia Suluhu, kwa teuzi za wakuu wa mikoa alofanya. Nimependa kwani imekaa kimkakati zaidi na hasa kwa kuangalia uwezo na kushabihiana kwa wasifu wa wakuu hao na mikoa waliopangiwa. Mfano kwa uchache:

Mhe. Makala kupangiwa Dar, huyu ni mtu wa shughuli, na ni mwongeaji pia. Hivyo atawezana na pilikapilika za Dar. Lakini ni mtu wa hamsha hamsha, Dar itarudi kuchangamka, kwani ilipooza sana utadhani Singida. Hivyo kipele kimepata mkunaji.

Mhe. Kunenge ni mchapa kazi, ila ni mtaratibu sana, ambalo ni jambo jema, hivyo Pwani inamfaa zaidi.

Mhe. Chalamila, huyu ni shughuli, huyu ni zege hailali, ni moja ya wakuu wa mikoa wenye misimamo, lakn hapendi mzaa kwenye kazi. Ni mtu anae simamia maagizo ya serikali kwa moyo thabiti. Huyu Mwanza inamfaa. Ule mkoa unawatu wabishi, na kunawengine wanajiona maliwatani.

Ni mkoa unawazee ambao mkuu wa mkoa akifika wanamkamata na kumfanya mkuu wa mkoa kutulia. Sasa Mwanza inakutana na mjeshi asie kuwa jeshi. Kuna miradi mingi ya maendeleo Mwanza inasuasua, kwa huyu Mhe. nadhani Mwanza itakaa vizuri hiyo miradi itamalizika kwa wakati.

Lakini Mwanza nayo ilipoa, huyu mhe. natumai atairejesha mwanza ktk tabasamu na vituko vyake. Yule alokuwepo Mhe. John Mogella aliifanya Mwanza ipoe.

Mhe. John Mongella ni mchapa kazi, ila kwa wajihi wake ni mpole na mtaratibu. Kwa jiji la Mwanza na mikikimikiki alielemewa. Mwanza ikawa chafu, ule usafi ukapotea. Lakini kwa Simiyu alikopelekwa panamfaa sana.

Mhe. Mtaka, kupelekwa Dodoma ni mkakati mzuri. Huyu Mhe. Yuko smart, na ni mtu wa mikakati ambaye mara nyingi utaka kuona matokeo ya kile alichopanga. Mhe. Ataweza kuisimamia, vizuri Dodoma, na kufanya Jiji hilo kukua zaidi, na kufungua mianya mizuri ya kuboresha uwekezaji jijini Dodoma. Alifanya vizuri sana alipokuwa Simiyu.

Hivyo tutarajie kuona Mhe. Mtaka akiiweka Dodoma katika chat. Si mtu wa mbwebwe bali ni mchapa kazi, tena kimya kimya.

Mhe. Hapi, huyu kupelekwa Tabora kunafaa sana. Tabora ni mkoa wenye utamaduni toka zamani kuwa na maisha ya uswahilini. Yaani ni vigenge vya gahawa. Kuna wazee wakigoma jambo lisifanyike alifanyiki. Japo mkuu wa wakati huo, mzee wa Toronto aliibadilisha kweli Tabora. Nategemea Hapi ataendeleza na kusimamia kuubadili mkoa wa Tabora, kama alivyosimama Iringa na kuiweka katika Mstari. Mhe. Hapi ni jasiri na mwenye misisimamo, anaependa tension, hivyo Tabora itarudi kwenye vyombo vya habari tuanze kuona nini kinatokea leo Tabora. Mtumishi yupi kabanwa leo. Kama yale ya "Wewe shika kamba huko soma"!

Mhe. Kafulila, yupo vizuri sana, katika utendaji na ni mdiplomasia mzuri. Kwa mazingira ya Arusha ataendana nayo, hivyo kuondoa migogoro na kujenga maelewano mazuri. Lakini kwa kua ni mji wa kidiplomasia na utalii. Na yeye ni mzuri kwenye maswala ya kujenga uchumi. Ataimarisha vyema vyanzo vya kiuchumi vya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Arusha.

Hata Mhe. Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti alokuwa Kagera na kuhamishiwa Mtwara, ataweza kukomesha uharamia huko Mtwara kutokana na tishio hili la Al shabab wanao sumbua Msumbiji. Alipokuwa Kagera, kulitulia hakukua na uharamia tena wa wafugaji wa Kitutsi kuvamia na hata kuuwa raia wetu. Hivyo tutarajie atakuwa imara kuondoa tishio la magaidi huko Mtwara.

Kwa ufupi, hata ambao sikuwataja hapa Rais wetu amekuwa makini kuwapanga hawa wakuu wa mikoa kimkakati zaidi. Hongereni mlioteuliwa, chapeni kazi. Msaidieni Rais wetu.
 
Naona kaamua kurudisha utawala wa kiraia

Takukuru na kule Foreign affairs


Mambo ya Kidiplomasia Wizara ya Mambo ya nje ilikuaje ikaongozwa na Mwanajeshi?

'Mtoto wa Mstaafu' kaletwa Dar!

Hongera zake maana alitumbuliwa kwa kutouza Vitambulisho vya Wamachinga kule Katavi
 
Chupa mpya mvinyo uleule , kijani kibichi ni chama cha ajabu sana unawabadilisha vituo halafu unasema umeteua ? .
 
Kagera kapelekwa nani na kwa mkakati upi kulingana na uchambuzi wako?
 
Bashite ndiyo hivyo tena, anapotea ktk anga na duru za kisiasa. Teuzi naona bado zinampitia mbali, labda tusubiri afikiriwe tena ktk nafasi ya ukuu wa wilaya. Ijapokuwa inaweza kuwa ni ngumu kwani kwa kupenda sifa aliwahi kumuhusisha "prince" wa mfalme mmojawapo aliyepita na biashara ya unga.
 
Mwanza wameunganishwa na kifurushi cha cheka zogo ili waendelee kudemka vizuri...😂😂
 
Back
Top Bottom