Uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya wavuja, Luhanjo atengeneza mtandao wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya wavuja, Luhanjo atengeneza mtandao wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ludewa, Dec 2, 2011.

 1. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UTEUZI wa wakuu wa wilaya na wale wa mikoa mitatu mipya unaotarajiwa kufanywa wakati wowote na Rais* Jakaya Kikwete, umezua tafrani kubwa katika baadhi ya wilaya na mikoa baada ya kuvuma kwa taarifa kwamba miongoni mwa wateuliwa hao ni wabunge wa zamani waliokataliwa na wananchi katika kura za maoni kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

  Taarifa za kuaminika zilizolifikia Tanzania Daima zimesema kuwa mmoja wa watu wanaotajwa kuwa watateuliwa kushika nafasi ya ukuu wa mkoa, kati ya ile mitatu mipya, tayari ameanza kupita mitaani akitamba na kuanza maandalizi ya sherehe ya kujipongeza.

  ‘Mteuliwa’ huyo aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo moja lililoko katika moja ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambaye inadaiwa anapigiwa chapuo kwa kiwango kikubwa na kigogo mmoja wa Ikulu ambaye wana uhusiano wa kirafiki wa siku nyingi.

  Kigogo huyo wa Ikulu (jina linahifadhiwa) anadaiwa kutumia wadhifa wake kupenyeza jina la mbunge huyo wa zamani ambaye alianguka vibaya katika kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi na tayari ameanza tambo dhidi ya watu wanaodaiwa kuwa mahasimu wake walioongoza mapambano yaliyomwangusha katika uchaguzi mkuu uliopita.

  Habari zaidi zimesema kuwa mbunge huyo wa zamani amekuwa akipita katika baadhi ya wilaya za mkoa mpya wa Njombe akiwataarifu rafiki zake juu ya kuteuliwa kwake kushika nafasi ya ukuu wa mkoa huo na kwamba uteuzi huo umesimamiwa kikamilifu na kigogo huyo wa Ikulu.

  Hata hivyo, kuvuja kwa siri hiyo kumewachefua wananchi wengi wa mkoa huo mpya na wameliambia Tanzania Daima kuwa hawako tayari kumpokea mbunge huyo wa zamani kama mkuu wao wa mkoa ikiwa taarifa hizo ni za kweli.

  Baadhi ya wananchi wameliambia gazeti hili kuwa mbunge huyo anayeandaliwa kushika nafasi ya ukuu wa mkoa wa Njombe, hafai kwa kuwa ni mtu wa visasi na hivyo ataacha kufanya kazi za kuendeleza mkoa wao mpya, badala yake ataleta malumbano ya kisiasa pasipo na sababu za msingi.

  Wananchi hao pamoja na kumpongeza Rais Kikwete kwa kuwapatia mkoa mpya, walimtaka asikubali kupotoshwa na msaidizi wake huyo na kukubali kuwateua watu waliokataliwa na wananchi kuwa viongozi wao.

  “Kitendo cha Rais* Kikwete* kuwateua** wabunge* waliokataliwa na* wana* CCM katika* kura za maoni* kuwa wakuu* wa mikoa mipya* kutaleta matatizo makubwa…ni vema aangalie hili kwa makini,” alisema mkazi mwingine wa Ludewa.

  Baadhi ya watu wanaotajwa kuwa wakuu wa mikoa mipya ni pamoja na aliyewahi kuwa waziri mwandamizi katika serikali tatu zilizopita, wabunge wawili kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mkuu mmoja wa wilaya moja mkoani Kilimanjaro.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Philimon Luhanjo alikataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na madai hayo, kwa maelezo kuwa hawezi kuzungumza jambo lolote mara baada ya kutajiwa jina la mwandishi na sababu za kutafutwa kwake.

  “Ni nani mwenzangu…. hapana kwa sasa sina utaratibu wa kuzungumza na waandishi wa magazeti; tafadhali nakushuru,” alisema Luhanjo na kukata simu.

  Rais* Kikwete* anatarajiwa kutangaza majina ya wakuu* wa wilaya* na mikoa mipya iliyoongezwa hivi karibuni ya Njombe, Katavi, Geita na Simiyu.

  source: tanzania daima
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakuu wa Mikoa mitatu mbona wapo tayari wanasubiri kupangiwa vituo? Au Tanzania Daima wamesahau kwamba mara ya mwisho Rais alipofanya Uteuzi wa RC's kuna vigogo watatu alisema watapangiwa vituo vingine?

  ....Kwa hali inavyokwenda si ajabu kuwa wakubwa wamesahau kuna watu wanasubiri vituo.
   
 3. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu wa mkoa mpya wa njombe???
   
 4. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  msaada kwenye tuta. ni akina nani hao?
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Nahisi harufu ya Mwakipesile humu jamani.
   
 6. b

  baba koku JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ni vyema tusiwe tunapotoshwa na watu wa fitina wanaotumia magazeti kufitini. Hivi Rais akimteua aliyekosa ubunge kuna nongwa gani? Kutokuchaguliwa ubunge sio kigezo pekee kuwa muhusika hafai kufanya kazi yoyote.Mfano, wabunge wengi wa kuteuliwa kupitia CDM ni wale walioshindwa katika kinyanganyiro cha ubunge. Je kweli hawafai kwa wadhifa kama huo? Tuepuke kutumiwa na watu wa fitina.
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jackson Makwetta Njombe!!!
   
 8. b

  baba koku JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ni vyema tusiwe tunapotoshwa na watu wa fitina wanaotumia magazeti kufitini. Hivi Rais akimteua aliyekosa ubunge kuna nongwa gani? Kutokuchaguliwa ubunge sio kigezo pekee kuwa muhusika hafai kufanya kazi yoyote.Mfano, wabunge wengi wa kuteuliwa kupitia CDM ni wale walioshindwa katika kinyanganyiro cha ubunge. Je kweli hawafai kwa wadhifa kama huo? Tuepuke kutumiwa na watu wa fitina.
   
 9. b

  baba koku JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ni vyema tusiwe tunapotoshwa na watu wa fitina wanaotumia magazeti kufitini. Hivi Rais akimteua aliyekosa ubunge kuna nongwa gani? Kutokuchaguliwa ubunge sio kigezo pekee kuwa muhusika hafai kufanya kazi yoyote.Mfano, wabunge wengi wa kuteuliwa kupitia CDM ni wale walioshindwa katika kinyanganyiro cha ubunge. Je kweli hawafai kwa wadhifa kama huo? Tuepuke kutumiwa na watu wa fitina.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kitu cha msingi sio kuangalia uCCM au uCDM bali manufaa ya nchi katika maendeleo yake. Kama watu wamemkataa kiongozi, kuna sababu gani za kuwang'ang'aniza kuwa mtu husika lazima awe kiongozi wao? Madhara ya teuzi kama hizi tumeyaona baada ya Mwakipesile kupewa uRC kule mbeya ambako kwa sababu za kisiasa mpango makakati ulikuwa kudumaza maendeleo ya mkoa kwa kumchagua mtu ambae watu hawakumtaka as a result akatumia muda wake mwingi kulipiza vizasi vya kisiasa badala ya kusukuma maendeleo. Makosa kama hayo yasije yakatokea kwa mkoa wa Njombe kwa kumteua Makwete mtakuwa hamtutakii mema!! Luhanjo inabidi astaafu kwa amani ama sivyo atakosa pa kujificha akija njombe.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Njia ya mwongo fupi. Rais Kikwete amenukuliwa akiwaambia wabunge wa CHADEMA kuwa muswada wa katiba mpya ni mbovu, lakini asipo sign wabunge wa chama chake (CCM) hawatamwelewa! Sasa inakuwaje kwenye maazimio ya kumfukuza kazi Luhanjo Rais Kikwete haonekani kuwaogopa wabunge wa CCM?

  Kamati maalum ya bunge ilimkuta Luhanjo ana hatia kwenye saga la Jairo na walipendekeza Luhanjo aondoke kwenye nafasi yake, wabunge wote na hasa wale wa CCM wamekubali mapendekezo hayo na kupitisha kama maazimio ya bunge sasa inakuwaje Kikwete (muoga/muongo?) bado anamkumbatia Luhanjo? Ikulu imeguka Mafia centre!
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kama ni makwetta basi Njombe mmekwisha
   
 13. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukiisoma hii stori vizuri anayesemwa hapa ni prof mwalyosi, makweta na dr norman sigala. wote hawa walikataliwa kwenye kura za maoni majimboni kwao ludewa, njombe kaskasini na makete.
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Norman Sigalla awe mkuu wa mkoa mara hii,kwa utendaji gani? Pengine kwavile mshirika wake Pindi Chana yuko karibu na vigogo wa ccm!!
   
 15. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama kweli hakuna watu wengine kabisa wanaofaa kupewa nafasi hizo ni bora sehemu husika ziendelee kubaki bila viongozi hao, hadi hapo watakapopatikana kuliko kupeleka watu wasiokubalika.
   
 16. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tatizo la mkuu wa kaya ni kigeugeu ndivyo alivyo poleni mnaomfuatilia..
   
 17. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  umeona CDM ndiyo ya kutolea mfano!
   
 18. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kama ni Prof.Rapha Mwalyosi au Jack Makweta au Hozee Mungai.,Nawaunga Mguu am sorry Mkono 100% waibebe Njombe japo mimi sio Fisadi au Gamba,Hawa wanaweza,lakini sio Monica,Mwantumu Mahiza wa Pwani au Batilda Burian yule wa R-Chugga,hawa ni vimeo balaa,Pwani tatizo wanapenda tende ndio maana hawajasanuka juu ya Mwantumu.Wadau wa JF,japo hatupendi baadhi ya mambo ya Kifisadi,Lakini Makweta ana Uthubutu,Mwalyosi alichakachuliwa na yule dogo asiye na mbele wala nyuma anajiita DEO Fillkunjombe,mambo yote yanayohusu Liganga na Mchuchuma aliandika Mwalyosi,so anafaa kuwaa RC kiukweli.
   
 19. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa mtazamo wangu hao wote walotajwa hapo juu ni viongozi wazuri. sigala, makweta, mwaluosi, etc. sie ni wapenda maendeleo katu hatutaki ya mwakipesile na
  mwakyembe yatokee ktk hii mikoa mipya. wananchi wa maeneo husika wanataka maendeleo na si visasi.
   
 20. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Blackbold:
  Mkuu una ushahidi na hili?
   
Loading...