Uteuzi wa Trump nini tunajifunza?

Uteuzi wa Trump nini tunajifunza?

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Rais mteule wa Marekani anateua timu ya watu watakaomsaidia katika uongozi wake wa miaka 4. Kuna kitu kikubwa sana nimejifunza kwa huyu jamaa na hakika wamarekani wako mbele kwasababu wanajua nini maana ya uchumi.

Ukiangalia bodi ya ushauri wa Trump kwenye mambo ya uchumi utajua kwanini wamarekani wako mbele. Hakuna masikini yuko kwenye hiyo list na hii si kosa wala ubaguzi maana mchango wa masikini kwenye uchumi ni mdogo sana. Masikini hawawezi kupanga mambo ya kustabilize economy, hawajui nini kinaweza kufanya nchi ikaleta ushindani na kuvutia mitaji mikubwa, masikini hawana uwezo wa kuleta ajira wala kuajiri.

Uwepo wa matajiri kwenye ushauri wa uchumi ni jambo muafaka sana maana watajua athari ya maamuzi ya serikali kwenye biashara zao na taifa kwa ujumla. Jamaa hajaweka watu wa chama chake wala mkewe kama mshauri mkuu wa suala nyeti la uchumi wa marekani maana anajua hapo chama hakina nafasi, hajeweka wanajeshi wastaafu maana suala la uchumi haliwahusu. Ni ma CEO na marais wa makampuni makubwa hakuna professor humo na kama yupo basi naye ni billioner maana uchumi wa nchi ni tofauti na madesa inahitaji experience ya walioko kwenye field.

Tanzania tungekuwa na washauri wa Rais kwenye mambo ya uchumi watu kama dk Mengi, Bakhressa, MO, KIMEI na wakurugenzi wengine wa taasisi za kibiashara. Ifike sehemu ukada ubaki pembeni wawekwe washauri wanaojua nini hasa maana ya uchumi kwa vitendo. Najua kuna watu wana chuki na matajiri na hata humu wapo.

Hawa ni watu wanaoona ufahari wakiwa masikini, wanafurahi akisikia tajiri fulani kafilisika. wanajipa moyo eti ni vigumu tajri kuingia mbinguni huku wao wakiwa wanadhambi nyingi kuliko matajiri.

TUACHE MAWAZO YA KIMASIKINI JAMANI NI MUDA WA KUWAPA MATAJIRI NAFASI WAJENGE VIWANDA NA KUSHAURI KUHUSU UCHUMI WETU.
HUU HAPA UTEUZI WA BODI YA USHAURI WA UCHUMI WA BWANA TRUMP

Mwenyekiti wa Bodi, Stephen Schwarzman ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Blackstone.

Paul Atkins, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa General Motors
Toby Cosgrove, Mkurugenzi Mtendaji wa Cleveland Clinic
Jamie Dimon, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa JPMorgan Chase & Co.
Larry Fink, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa BlackRock
Bob Iger, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa The Walt Disney Company
Rich Lesser, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Boston Consulting Group
Doug McMillon, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Wal-Mart Stores Inc.

Jim McNerney, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Boeing
Ginni Rometty, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa IBM

Kevin Warsh, Mjumbe wa zamani wa Bodi ya Magavana wa Federal Reserve System
Mark Weinberger, Mwenyekiti wa dunia na Mkurugenzi Mtendaji wa EY
Jack Welch, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa General Electric
Daniel Yergin, Mshindi wa Tuzo ya Pulitzer na Makamu Mwenyekiti wa IHS Markit

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kundi hilo litamshauri Trump jinsi ya kuweka mipango itakayochochea ukuaji wa upatikanaji ajira na kuongeza uzalishaji nchini Marekani
 
Tusio makada tumewekwa mbali sana na mambo yote ya utawala na hata ushauri ndani ya nchi yetu. Yaani tupo tupo tu kama mayatima au wahamiaji fulani.
 
Kina Soyinka ujinga unawaumiza, ngoja wakabakwe na bokoharamu wajutie green card zao.

Soyinka nadhani kakimbilia Canada, mimi najiuliza tu hivi kweli hiyo timu trump japo ni rais ataweza kuwaendesha na kutokuwasikiliza? jibu kwangu ni hapana, hivyo kwenye uchumi nadhani atakuwa poa sana.
 
Soyinka nadhani kakimbilia Canada, mimi najiuliza tu hivi kweli hiyo timu trump japo ni rais ataweza kuwaendesha na kutokuwasikiliza? jibu kwangu ni hapana, hivyo kwenye uchumi nadhani atakuwa poa sana.
Naiunga mkono dhana yako. Atakuwa anaongea na watu wenye direct impact kwenye uchumi wa nchi yao ambao hawatapenda sera za uchumi zilete hasara kwenye mitaji, si hivyo tu lakini pia hao washauri wanajua in and out maana na ujazo wa fedha kwenye mzunguko wa uzalishaji, mitaji, riba na gawio.

Naamini watazalisha ajira nyingi na kuvutia mitaji mikubwa kuja nchini mwao.
 
Tusio makada tumewekwa mbali sana na mambo yote ya utawala na hata ushauri ndani ya nchi yetu. Yaani tupo tupo tu kama mayatima au wahamiaji fulani.

kaka hii hali ya chama tawala na serikali yake kujimilikisha nchi ndiyo inayotufanya tuwe masikini. inatakiwa wananchi wasikilizwe hata kama hawako upande wa serikali. Kwenye mambo ya uteuzi tujaribu kuangalia watu na si vyama vyao wala imani zao, washauri katika mambo ya uchumi tuweke watu wanaojua biashara kama hawa CEOs wa makampuni makubwa hata kama si mtz ,maana ushauri wao hautabase kwenye asili zao bali hali halisi ya uchumi wa nchi ambayo na wao ina faida kwao
 
Kibongo bongo unaangaliwa ulimsifia kwa kiwango gani mkuu wa kaya au ulimsaidia nini ktk kampeni kisha unapewa kitengo hata kama kichwani darasa la saba na ana njaa hatari,limtu linateuliwa toka linaapishwa mpaka linakabidhiwa office linawaza jinsi ya kuiba unafikiri kuna kitakachoendelea hapo?
 
Naiunga mkono dhana yako. Atakuwa anaongea na watu wenye direct impact kwenye uchumi wa nchi yao ambao hawatapenda sera za uchumi zilete hasara kwenye mitaji, si hivyo tu lakini pia hao washauri wanajua in and out maana na ujazo wa fedha kwenye mzunguko wa uzalishaji, mitaji, riba na gawio.

Naamini watazalisha ajira nyingi na kuvutia mitaji mikubwa kuja nchini mwao.

Aksante sana kaka umenielewa, hivi Phd holder kukushauri kuhusu uchumi huku akiwa hana hata kiwanda cha juice ya miwa ni utimamu kweli? . Si dharau wasomi na si kwamba wasiwepo ila na mabwenyenye wawepo tena wengi tu maana hawa watu pesa na investment zao ndizo zinaongoza hiyo uchumi.
 
Mbele ni mbele tu...Africa tunaendekeza uchama
 
Back
Top Bottom