Uteuzi wa Mwantumu Mahiza

Uteuzi wa Mwantumu Mahiza

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,585
Reaction score
3,180
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mama Mwantumu Bakari Mahiza,ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shule ya Msingi Julius Kambarage Nyerere,uteuzi huu umeanza ramsi July 01,2018.
Mahiza anachukua nafasi ya aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Lyimo ambaye ameondoka shuleni hapo.
IMG-20180723-WA0023.jpg
 
Maisha yanaendelea kuna nafasi za uteuzi na nafasi za kitaaluma aliyenayo mtu.
 
Hongera Sana Kwa Uteuzi
Ataapishwa Lini Huyo Mheshimiwa
 
Kwa kweli huyu Mama namkubali alikuwa mchapa kazi hodari sana enzi zake. Mhe.Rais mfikirie kwa nyadhifa zaidi ya hii.
 
Hayo ni majina tu yanafanana au ni yeye mwenyewe?kama ni kweli basi atakuwa ana hisa hapo au ni shule.yake
 
Alikuwa mkuu wa shule hiyo tena kama sikosei mwanzilishi kabla hajanyakuliwa na JK kwenye vyeo vya kisiasa, kwa hiyo anarudi kuimarisha shule hiyo ya binafsi. Shule ilianza vzr sana miaka hiyo ya 90s lkn baada ya kuondoka yeye kiasi ilipoteza mwelekeo watu wakaaza kuikimbia taratibu.
 
Hakika wewe unamfahamu Mwalimu Mahiza. Huyu mama ni kati ya Walimu bora na mahili katika sekta husika. Siasa zilimtoa kwenye wito wake (Ualimu). Kwa wanaomfahamu ni mtu makini sana.
Nampongeza kurudi katika kazi yake aliyoipenda na kuifanya kwa weledi. Nakutakia kila la kheri Mwalimu Mahiza.
 
Alikuwa mkuu wa shule hiyo tena kama sikosei mwanzilishi kabla hajanyakuliwa na JK kwenye vyeo vya kisiasa, kwa hiyo anarudi kuimarisha shule hiyo ya binafsi. Shule ilianza vzr sana miaka hiyo ya 90s lkn baada ya kuondoka yeye kiasi ilipoteza mwelekeo watu wakaaza kuikimbia taratibu.
kwa io ameitwa kuweka mambo sawa?
 
Kwa kweli huyu Mama namkubali alikuwa mchapa kazi hodari sana enzi zake. Mhe.Rais mfikirie kwa nyadhifa zaidi ya hii.
Huyo hawezi kurudi, ali mess up na kuwaletea nyodo Saidi Mtanda na Nape..walichofanya "wakamkomesha" kama ambavyo yeye aliwakomesha 2015..matokeo yake wote wamekosa! mama ana nyodo sana huyo..!
 
Back
Top Bottom