Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Bahati mbaya mtazamo wako umeangukia katika kulipana fadhila na kuheshimiana kuliko kujali maslahi ya taifa.
Hdi hivi sasa bado mwandosya ana kundi kubwa nyuma yake ingawa hana makeke kama walivyo wanasiasa wengine
kuna kazi na kazi! Kwanza J.K hajampa Mwandosya kazi yoyote amempa mshahara wa bure.Labda uanze kwa kuniambia ni fadhira zipi JK atakuwa analipa kwa Mwandosya. Na kuhusu maslahi ya taifa, hilo ndilo usiloelewa; ikiwa tunalalamika kwamba tuna viongozi wengi ambao hawajali maslahi ya taifa, na wapo wachache wachapa kazi kama kina Mwandosya, kwa nini tuwatupe kwa kuwa tu kwa kuwa kwa kipindi fulani afya yao haikukaa sawa? Niliwahi kuuliza swali, kwamba wengi wetu humu ndani ni wafanyakazi; nani kati yetu aliyemchapa kazi hodari kwa miaka mingi angeona ni haki kuachishwa kazi kwa kuwa amekuwa mgonjwa kwa miezi kadhaa badala ya angalau kupewa muda wa kupona sawa sawa bila kuachishwa kazi?
Nina mpongeza sana kwa busara zake na hekima nyingi za kuchagua kutozungumzia afya yake ovyo ovyo.
Wengi wanamlaumu JK juu ya kumteua Prof. Mwandosya kuwa Waziri asiye na Wizara maalum. Nadhani upembuzi huo si sahihi. Mie nadhani JK amemheshimu sana Mwandosya. Kumbukeni Mwandosya bado hajarejesha afya yake vema, na hivyo JK hajampa Wizara kamili ambayo ingehitaji nguvu nyingi. Wengi tungeishia kusema Mwandosya bado mgonjwa kwa nini apewe Wizara kubwa wakati Watanzania wengine wapo.
Alichofanya JK ni sawa na kuamua kumpumzisha Mwandosya huku bado akimweka karibu ili asiwe mbali na yanayojiri katika Baraza la Mawaziri, ikimaanisha bado anahitaji busara za Mwandosya na anaamini atapona kabisa na kuendelea na kazi. Kumbukeni kuna wakati Nyerere alimpumzisha Sokoine akiwa mgonjwa kwa karibu kipindi cha miaka miwili. Sokoine alipopona kabisa ndipo Nyerere akamrudishia Uwaziri Mkuu. JK angempumzisha Mwandosya kwa namna hiyo watu ndio mngesema hata zaidi!
In fact JK kumfanya Mwandosya Waziri asiye na Wizara maalum Mwandosya atakuwa katika ofisi ya Raisi, ikimaanisha atakuwa karibu zaidi na JK kushauriana mambo yanayohusu Wizara yeyote ile. Mie binafsi ninaheshimu sana utendaji wa Mwandosya, na kwa hili alilofanya JK kwa Mwandosya nimeona JK katumia busara sana. Fikirieni kwa makini.
Labda cha kumsihi JK ni kwamba sasa atumie busara na umakini wa Mwandosya kwa namna kubwa hata zaidi kwa kuwa wako ofisi moja; Ofisi ya Raisi.
Lakini pia Mwandosya ni mtaji wa kisiasa. Kikwete mwenyewe anajua kama si mizengwe asingeweza kumshinda 2005. Hdi hivi sasa bado mwandosya ana kundi kubwa nyuma yake ingawa hana makeke kama walivyo wanasiasa wengine
Tuwe na subira, ipo siku umma utakuja kugundua nini kilimsibu our renowned Professor. Nina mpongeza sana kwa busara zake na hekima nyingi za kuchagua kutozungumzia afya yake ovyo ovyo. Otherwise I personally believe kwamba uteuzi wake kuwa a minister without portfolio was inevitable; upon a cost-benefit analysis, handling the repercussions za kumwacha ni more costly. Otherwise mungu atamjalia na kumrudisha katika afya yake ya kawaida kwani tunamhitaji sana kama taifa
Hivi isingekuwa busara zaidi kwa mh Mwandosya kuomba apumzishwe?