UTEUZI: Rais Samia ateua Katibu wa Rais, Mnikulu na wasaidizi wake wa Uchumi, Sheria, Siasa, Diplomasia n.k

Rais ametoa salaam hasa za Jamhuri ya Muungano kwa kuteua wasaidizi toka Zanzibar na Tanganyika.

Kero za Muungano zinazidi kupunguzwa na Muungano kuimarishwa kwa kutosahau wasaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano lazima waonekane kutoka pande zote mbili.
Han'na Nzanzibari hapo waangalie vizuri sana.
 
Elimu ya Ngusa mpaka sasa bado haifahamiki.

Ila Jiwe nae sijui alitumia vigezo gani katika kuteua wasaidizi wake. Mistery!
Unapata picha gani hapo?
images%20(3).jpg
 
Nakumbuka wakati wa hayati Rais Magufuli, katibu wa Rais( Private Secretary to the President of the United Republic of Tanzania) na mnikulu ( Comptroller State House) alikuwa ni mtu mmoja ndugu Ngusa Dismas Samike

Naona mheshimiwa Rais Samia yeye ameamua kutenganisha tena kama ilivyokuwa kwa mheshimiwa Rais mstaafu Kikwete

Kongole na hongera kwa wateule wote
Uko sahihi kabisa
Alishikilia vyeo viwili.
 
With all due respect madame President, Mbona wasaidizi wengi?mi nirifikiri wasaidizi/washauri wako ni mawaziri?mbona unatengeneza mavyeo Mengi?
Hivi vyeo viliuwepo awamu zilizopita?
Mfano unawaziri wa mambo ya nje,anayesimamia diplomasia,harafu unateua Mshauri/msaidizi wa mambo ya kidiplomasia,sasa hapa ushauri wa nani utazingatiwa?
km huvijui kaa chini nyamaza
 
Religious biased
Siku izi Majina ya waTanzania hayaendani na udini, kuwa muangalifu utakuja kuwaangamiza ndugu au jamaa zako kama utakuwa unabase katika majina.
Ila Mzanzibar utamjua na Mtanganyika utamjuwa ,yaani chogo tu amna jingine. Si ndio wanatuita machogo walivyokuwa hawana adabu watu wale .ila nasie hatunazo tunawaita wapemba ,utasikia boti ya wapemba imeshafunga gati,Yaani wazanzibari wote ni wapemba.
 
Ipo siku mtasema ccm idumu ndo kilichobaki.
Ili siku kiongozi wenu mbowe akipindisha macho nyoote mtapindisha na kuachana na sifa kwa huyu mama.

Nati za vichwa vyenu spana anazo mbowe.
Akili zenu anazo jiwe na tutamuongezea madaraka mpk 2030 #Atake asitake.
 
Bado sijaona mantiki ya kuambiwa hizi teuzi hadharani. Ni upuuzi mtupu.
Hivi kuna haja ya kuutangazia umma uteuzi wa wasaidizi wako binafsi wa ofisini ukiwa kama Rais?
Hivi watangulizi wake walifanya hivi?

Maana ukianza kufanya haya, itabidi kila msaidizi wa Rais awekwe wazi.
Kwa mfano; msaidizi wa mambo ya afya, michezo, biashara, kilimo, uvuvi, walemavu, Daktari wa Rais, Dereva wa Rais, Dressing designer wa rais, Mpishi wa rais nk.

Na pia siku ukimbadilisha msaidizi itabidi uutangazie umma.

Yoyote kwa yote hao wasaidizi unawaweka katika mazingira ya kufuatwa fuatwa na watu ili wawasaidie kufikisha ujumbe kwa rais au kufanya lobbying. Na wakipata kashfa itahusishwa na ofisi ya rais.

Binafsi naona hili ni kama jambo la kishamba, kutokujiamini na udhaifu wa rais Samia ambao ameuweka hadharani. Sio kila kitu kinapaswa kuletwa hadharani.
Cjashangaa hili sana kwani naamini wasaidizi wa mama ni zaidi ya hawa na tumejulishwa hawa kwa sbb ni muhimu, ninachoshangaa ni uteuzi kufanyika tarehe 19/3/2021...hii ilikua siku ya pili ya msiba wa mwendazake kama sikosei na nadhani ndo siku alipoapishwa mama akiwa na simanzi kuu, hivi ni kweli siku ileile alifanya uteuzi wa wasaidizi wake wa karibu na kuwatoa wa mtangulizi wake au wame-backdate uteuzi tu kwa malengo fulani ya kiintelijensia????
 
Bado sijaona mantiki ya kuambiwa hizi teuzi hadharani. Ni upuuzi mtupu.
Hivi kuna haja ya kuutangazia umma uteuzi wa wasaidizi wako binafsi wa ofisini ukiwa kama Rais?
Hivi watangulizi wake walifanya hivi?

Maana ukianza kufanya haya, itabidi kila msaidizi wa Rais awekwe wazi.
Kwa mfano; msaidizi wa mambo ya afya, michezo, biashara, kilimo, uvuvi, walemavu, Daktari wa Rais, Dereva wa Rais, Dressing designer wa rais, Mpishi wa rais nk.

Na pia siku ukimbadilisha msaidizi itabidi uutangazie umma.

Yoyote kwa yote hao wasaidizi unawaweka katika mazingira ya kufuatwa fuatwa na watu ili wawasaidie kufikisha ujumbe kwa rais au kufanya lobbying. Na wakipata kashfa itahusishwa na ofisi ya rais.

Binafsi naona hili ni kama jambo la kishamba, kutokujiamini na udhaifu wa rais Samia ambao ameuweka hadharani. Sio kila kitu kinapaswa kuletwa hadharani.
Utakuwa mchawi wewe..
 
Back
Top Bottom