UTEUZI: Catherine Ruge(CHADEMA) ateuliwa kumrithi Dr. Macha(aliyefariki), Ubunge Viti Maalum

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Tume ya Uchaguzi(NEC) imemteua Ndg. Catherine Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) kujaza nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Dr. Macha aliyefariki mwezi uliopita.

ruge.jpg




UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.

Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:-

Kailima, R.K

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

 
Hiyo barua haielezi kama baada ya kupata taarifa ya spika kuwa nafasi wazi kama cdm ilikuwa consulted before the issuance of this selection notice!!
Viti maalumu vyama vyote hupeleka majina kwa rank za kura walizopata kwenye chaguzi ndani ya vyama hivyo akiondoka mbunge wa viti maalumu tume inaenda tu kwenye list waliyopewa na chama husika wanampa aliyefuatia kwa kura.
 
If selection have been done basing on merits then she deserve that position ,kudos kwake mrembo mteuliwa.
 
Back
Top Bottom