UTEUZI: Catherine Ruge(CHADEMA) ateuliwa kumrithi Dr. Macha(aliyefariki), Ubunge Viti Maalum

Wacha ujinga wewe, kinachotoa mwongozo ni kura za maoni kwenye viti maalum. Hivyo huyu binti alikuwa anawafuatia walioteuliwa mara ya kwanza, hivyo tume huingia tu kwenye orodha na kuchukua aliyekuwa anafuatia kwa wingi wa kura. Hata Mama Rwakatare ilikuwa hivyo hivyo!!

Sidhani km ya mama Rwakatare ilikuwa hivyo hivyo.
M/kiti wa UWT huwa ana nafasi kwenye ubunge wa viti maalum.
Sophia Simba alipata ubunge wa viti maalum kwa kuwa m/kiti wa UWT.
Sasa sijui kuhusu mama Rwakatare.
 
Sidhani km ya mama Rwakatare ilikuwa hivyo hivyo.
M/kiti wa UWT huwa ana nafasi kwenye ubunge wa viti maalum.
Sophia Simba alipata ubunge wa viti maalum kwa kuwa m/kiti wa UWT.
Sasa sijui kuhusu mama Rwakatare.
Hudhani kwa kuwa Hujui ama hukujihusisha kujua.

Nikweli kuwa Sophia Simba alikuwa muwakilishi kupitia UWT alikuwa mbunge automatically kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa Umoja wao as structure yao ilivyo.

Lakini Mara baada ya kuvuliwa uanachama akakosa sifa za Ubunge then tume walipoarifiwa waka preview list akawa picked mama Rwakatate while yeye sio kiongozi UWT.
 
W
Mbona CCM wamempa ubunge viti maalumu Mch Getrude Lwakatare! Je ana positive influence?Wapinzani ni wachache ila wana mchango mkubwa sana bungeni, chama changu CCM ni kama wameondolewa ufahamu
We pumbavu acha kusema wewe ni Ccm
 
Sasa Ndugu chadema kindakindaki aka MPAMBANAJI.COM ni kwa Vipi Chama chako kingeweza kuingilia mchakato huo ambao uko kikatiba, ili sasa waweze kukidhi matakwa/matarajio yenu yakupitisha mtu mtakayeona anafaa?

Rejea Jinsi alivyopatikana Mama Rwakatare ambaye hakuwa mwenyekiti wa UWT (as replacement ya Sophia Simba ambaye aliupata Ubunge kupitia Wing ya Umoja huo). Pia Jikumbushe jinsi alivyopatikana Mrithi wa Hayati Regia Mtema.

Vyama havina nafasi ya Kubadili/kuingilia upatikanaji wa Mbunge wa viti maalum anayekuja kujazia nafasi iliyoachwa wazi.
sawa, yawezakuwa nahitaji kuchambua mantiki kwa undani zaidi, tatizo yawezakuwa kama walivyo wengine kuna uwezekano fikra zimesongwa na mzio wa kukata tamaa na maono yaliyokuwa miongoni mwa wengi yanaupamguza upepo wa fikra kandamizi kadri mfumo hasi unavyozidi kutuaminisha kwa upo chanya
 
Sidhani km ya mama Rwakatare ilikuwa hivyo hivyo.
M/kiti wa UWT huwa ana nafasi kwenye ubunge wa viti maalum.
Sophia Simba alipata ubunge wa viti maalum kwa kuwa m/kiti wa UWT.
Sasa sijui kuhusu mama Rwakatare.
Mama Rwakatare kwenye mlolongo wa wingi wa kura ndo alikuwa anafuatia, kwa maneno mengine mstari ulipita mgongoni kwake baada ya nafasi kuwa chache. Sasa ilipojitokeza nafasi ya Sofia Simba ndo mlango ukafunguliwa kwa mama Rwakatare. Vivyo hivyo na kwa Ruge mstari ulipita mgongoni kwake ndo maana amechukua hii nafasi ya Dr. Macha!!
 
Wasifu wa mbunge Catherine Nyakao RUGE


Bi. Catherine Nyakao Ruge ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii anayepinga mila kandamizi na kutetea haki za watoto wa kike na kina mama. Amekuwa akitetea haki za watoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni, ukeketaji, ukatili dhidi ya wanawake na ubaguzi dhidi ya watoto wa kike (wanawake) katika elimu na kazi/ajira.

Catherine ni mwanamke anayejituma katika kazi (hardworking), anayejiamini (confident), uwezo mzuri wa majadiliano, uwezo mzuri wa mawasiliano, mcheshi na mchangamfu kwa watu wa jamii na rika zote.

ELIMU:

i.Kwa sasa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam Shahada ya Uzamivu (Daktari wa Falsafa) katika masuala ya jinsia na Uhasibu (PhD in Gender and Accounting)

ii.Shahada ya Uzamili (MBA) katika Usimamizi wa Biashara toka chuo cha ESAMI – 2015

iii.Shahada ya kwanza ya Biashara na Uhasibu (Bcom) toka UDSM – 2007

iv.Shahada ya taaluma ya Uhasibu (CPA) toka NBAA – 2009




UZOEFU WA KAZI:

i.Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Girls Education Support Initiatives (GESI) kuanzia November 2015 hadi sasa

ii.Meneja Miradi, Taasisi ya Association of Private Health facilities in Tanzania (APHFTA), January 2013 hadi September 2015.

iii.Afisa Fedha Kiongozi, Taasisi ya Association of Private Health facilities in Tanzania (APHFTA), May 2011 hadi December 2012.

iv.Maneja Uhusiano, National Bank of Commerce (NBC), May 2010 hadi April 2011.

v.Mchambuzi wa miradi ya Biashara, National Bank of Commerce (NBC), August 2007 hadi April 2011.

MAJUKUMU YA KIJAMII:

Mshindi wa shindano la UN- empower women champions for change 2016/2017. anafundisha na kuwezesha wanawake kujikomboa kiuchumi kwa kuendesha mafunzo kwa makundi yafuatayo;

i.Kufundisha wanafunzi wa sekondari ili waweze kujitambua na kutimiza ndoto zao

ii.Kufundisha wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi

iii.Kufundisha uelewa wa masuala ya fedha kwa wanawake wajasiriamali wadogo


UZOEFU WA UONGOZI:

i.Mweka hazina CHADEMA Kanda ya Serengeti, February 2017 hadi sasa.

ii.Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Girls Education Support Initiatives (GESI), November 2015 hadi sasa.

iii.Katibu wa kamati ya fedha na rasilimali CHADEMA Kanda ya Serengeti, 2013 hadi 2017

iv.Mkurugenzi wa fedha taasisi ya Dar es Salaam entrepreneurship Forum (DUEF), March 2006-March 2007
 
mimi ni cdm kindaki ndaki, shida yetu hatupendi ukweli, tunalinda udhaifu na changamoto, hapa ndipo tunapotofautiana tuu... mimi nawashangaa sana... tukiendelea hivi itatuchukua miaka 20 mbele kujiimarisha katika uhalisia wa siasa na mwitikio wa hitaji la uma

Wewe ni mfisiem Chadema hakuna mapoyoyo.
1494141104342.jpg
 
Back
Top Bottom