GE2025 Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025

GE2025 Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025.

Kilichojiri kwenye utetezi wa tano kipo hapa: GE2025 - Utetezi wa tano wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 15, 2025

===
Majaji wameingia kwenye ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kesi ya Mhe. Lissu kuanza. Watu wamezuiwa kuingia ndani ya Mahakama kama ilivyokuwa jana.

Imebidi Viongozi wote wa Chama na Wanachama wote ambao tayari walikuwa wameshaingia ukumbini wametoka nje kuonyesha kutounga mkono kitendo cha Polisi kuzuia watu waiingie Mahakanani.

Mhe. Lissu amesema hataendelea na shauri lolote mpaka pale watu wake wote waliozuiwa njee watakapo ruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Mahakama.

Kesi imeahirishwa mpaka saa 5:08 ili majaji wafanye maaumuzi juu ya hali ya kuzuia watu nje ya mahakama.

Lakini pia kumuuliza msaidizi wa Mafwele ZCO George juu ya amri hii ya kuzuia waTanzania kuja kushudia kesi. Mahakama imerejea.

Sauti ya High Court imepigwa.

Majaji wameingia na Mheshimiwa Lissu nae ameingia.

Waandishi wanapiga picha na kuchukua video kadhaa.

Majaji wanachungulia kule juu ya ukumbi wa Mahakama anaona hakuna watu na hapa chini pia hakuna watu. Wananong'onezana.

Maana waliobaki humu ndani ni maaskari vipenyo kama 20 hivi na waandishi wa Habari mbalimbali na sisi tumo pia tunakomaa nao.

Majaji wanaandika bado.
Jaji Nduguru anauliza mko tayari.

Pande zote zinasema tuko tayari.

Jaji anasema mnakumbuka kuna hoja iliibuka kuwa watazamaji au wananchi wameondolewa Mahakamani kwa amri ya Polisi na ZCO.

Mahakama imefuatilia kama kuna amri hiyo kwa Jeshi la Polisi. Hatujapata amri yoyote kutoka kwa Polisi ni sawa na kusema hakuna amri yoyote kutoka kwa Polisi.

Na tuliona tu watu wanatoka hapa mahakamani na tukarejea kwenye tafsiri ya Mshitakiwa kwa kuonesha kama kulikuwa na kuhamsishwa watu watoke.

Sasa kwa vile hakuna amri yoyote na kwa vile huu ni ukumbi wa wazi na una limit ya watu. Utumike utaratibu wa week iliyopita mbona tulienda vizuri tu.

Kama kuna jambo lolote linapotokea basi litafutiwe ufumbuzi kabla mahakama haijaanza.

Utaratibu uliotumika week iliyopita uendeleee kutumika maana haukuleta taharuki yoyote iwe hivyo sasa.

Amemaliza Mhe. Jaji

Tuendeleee sasa Majaji wanasema.

Anaanza Mh. Lissu.

Naomba niseme nina hoja nyingine kwa taarifa tu. Taarifa iliyopo mbele ya Mahakama hii na viambatanisho vyake hasasa maelezo ya mashahidi yapo kinyume cha Sheria.

Na kwasababu yapo kinyume cha Sheria ni sawa na hakuna maelezo ya kisheria nitaeleza hapo baadae.

Niliona nitoe taarifa ya jambo hili kwa sasa kama sijaendelea na nilipoishia jana.

Tarehe 03 April nilitengeneza nia ya watu kuzuia uchaguzi.

Sasa ninataka kuzungumzia

Anasimama Katuga anasema hajatutajia sheria kuhusu ile notice yake

Kifungu cha 11, 262, 263, 266 vya CPA amevitaja Mhe. Lissu.

Ameruhusiwa aendelee na submission yake sasa. Publication inayozungumziwa kwenye kifungu cha 39(2) cha Penal Code sio oubli

Sasa publication inayozungumziwa hapa sio publication ya magazeti kabisa. Ukisema nilifanya publication ni lazima useme nilifanya publication gani na lazima iwe proved.

Kwenye hati ya Mashitaka inasema I uttered some words and publish the same.

Sasa nilipublish kwa nani?

Hao watu wanapaswa kusemwa yaani pleaded separately.

Hata nature ya publication hata hawajasema ilikuwa ni nini?

Ilikuwa ni barua, email au kitu kingine hawajasema na hiyo vilevile inaifanya hati ya mashitaka kuwa incurable defective.

Watu waliokuwa wametoka nje wameingia mahakamani muda huu na Mh. Lissu amesimama kutoa maelezo au submission yake. Majaji wanateta kidogo kupisha watu kuingia ndani.

Anaendelea Mhe. Lissu

Hati ya mashitaka imeandikwa na watu wasiojua namna ya kudraft Hati ya Mashitaka.

Anasimama Katuga anasema mwenzetu atumie maneno mazuri akisema watu hawajui kudraft charge anakosea. Mahakama ndio itaamua.

Jaji: mshitakiwa unasemaje?

Lissu anasema sawa, naondoa hiyo kuwa watu wasiojua kudraft mashitaka.

Sasa niendelee sitaki kuhangaika na mambo ya ajabu ajabu kwa sasa naomba niendeleee.

Kesi ya Mataka mahakama ya rufaa na Khatibu Gandi na wenzake. Hizi kesi zilisema Hati ya Mashitaka inapaswa kuwaje, kesi zilielezea vizuri.

Waheshimiwa Majaji kwenye Sheria ya Mwenendo wa Jinai haijaweka utaratibu wa kuandika charge sheet za Treason.

Na haya maneno nayatoa kwenye Grey Likungu Mataka ile ya High Court na Court of Appeal na kesi ya Gandi pia. Ndio yameelezewa hivyo.

Kwahiyo kwasababu hakukuwa na bado hakuna utaratibu wa namna ya kuandika charge sheet za Treason.

Grey Likungu na Khatibu Gandi zilisema utaratibu unaopaswa kutumika ni English Procedure.

Sasa hiyo English Procedure ni ipi?

Ni kwamba Charge sheet ya Treason kunakuwa statement of the offence, particulars of the offence na overt act (manifestation of the offence)

Kama ni publication unapaswa ku plea separate kwa mujibu wa sheria zetu na si vinginevyo.

Sasa sheria inataka hiyo publication ukishaifanya kwa mtu mwingine ni lazima huyo mtu mwingine aripoti kwenye vyombo.

Asipofanya hivyo na yeye anapaswa kuwa sehemu ya washitakiwa.

Sasa Hati ya Mashitaka tuliyonayo hapa haisemi nilifanya publication kwa nani na huyo nani yuko wapi?

Hawajasema kama ni shahidi wala ni mtuhumiwa mwenzangu.

Ndio maana nilisema information hii ni defective. Sasa ile Charge sheet ya Tarehe 10/04 ilikuwa inasema maneno yafuatayo...anaisoma hapa.

Ya Tarehe 18/09 inasema hivi ...... nayo anaisoma hapa. Maneno yaliyoongezwa kwenye hii mpya ni yafuatayo:

1. Within Kinondoni District for the purpose of intimidating the Executive of Republic na lingine 3. By his deed of uttering .

Hayo maneno hayakuwepo kwenye Charge sheet ya Kisutu ile ya mwanzo. Leo wamekuja nayo. Wameyatoa wapi? Shitaka nililosomewa Tarehe 10 April 2025 na shitaka ambalo nimesomewa jana waheshimiwa Majaji yako tofauti.

Zipo hizo nyongeza. Hoja yangu ni kwamba hizo nyongeza zimeruhusiwa na Mahakama ipi?

Amendment za Charge Sheet zimekuwa authorised na Mahakama gani?

Hoja yangu ni kwamba once a Charge is read to the accused person, he is given notice regarding that particular Charge and if there is any change it must be authorised by the Court.

Walibadilishaje bila ruhusa ya Mahakama au mahakama ilikutana nao wapi wakajadili na kuruhusiwa wapi?

Hayo mabadiliko yanapaswa kuwa expunged na yafutwe.

Hayo Mabadiliko Waheshimiwa Majaji sio innocent kama yanavyoonekana. They are not innocent at all.

Ukiachilia hilo la yalikuwepo Kinondoni ila ukibadili na kusema for the purpose of intimidating the executive of Republic wakati ile ya awali ulisema for the purpose of intimidating general election.

Sasa haya ni mambo mawili tofauti.

Mwanzo hamkusema haya mambo ya ku intimidate Republic.

Hamkusema mwanzo mnaanza kusema leo ili mjiokoe.

By his deed ukisema maana yake unataka ku plead overt act wakati maneno hayo by his deed hawakuwahi kuyaweka kabisa huko nyuma.

Hawajaomba ruhusa it should go.

Hayo mambo matatu yanapaswa kuondolewa kabisa yasiwe sehemu ya hati ya mashitaka. Nataka niende kwenye additional point of objection kwa sasa hapa.

Na baadae nitamalizia kwa kusema je hii hati inarekebishika? Anasimama Katuga anasema Tunaomba mwongozo mwenzetu anahamia kwenye additional objection inayozungumzia statements za mashahidi hazina uhusiano wowote na Hati ya Mashitaka.

Na hiki kitu hakiwezi kuletwa muda huu. Statement za mashahidi zikiwa defective haziwezi kufanya mashitaka yasiwe na msingi.

Kwa sasa milango imefungwa anakotaka kutupeleka sio kabisa.

Amemaliza hivyo Katuga hapa. Kama amemaliza kwenye hoja yake ya defectiveness ya Charge sheet basi tupewe nafasi tumjibu.

Lissu: may I reply your honor?

Jaji Nduguru anamwambia subiri kwanza naona kama wanajadili tena mawakili wa serikali wanaweza kusema wanaondoka pingamizi lao subiri kwanza.

Wako wanateta hapa.

Katuga: sasa mheshimiwa PO inaelezewa on pure point of law na sio mambo mengine kabisa. Vifungu alivyoeleza vina mambo mengi sana.

Ameitwa tena na mwenzake wanamuelekeza Katuga. Naona wameleta pingamizi ambalo hata Katuga mwenyewe halielewi vizuri.

Anaendelea tena maneno haya yamekuwa supported na kesi ya Jackline Gkasi vs Mlatia Asei maombi ya madai/2021.

Anaendelea Katuga

Kesi hii ilizungumza mambo matatu yakuzingatia kwenye PO na hapa hajazungumzia kabisa.

Katuga anasema naomba nieleweke hivyo.

Jaji: Mshitakiwa unaweza kujibu?

Anasimama Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji naomba nimjibu Wakili wa serikali Mkuu.

Kwanza sio utaratibu ku anticipate mpinzani wako anataka kusema nini wakati hujamsikia. Anataka kuleta hili au kile Kabla hajafanya hivyo.

Kwahiyo utaratibu alipaswa anisikilize kwanza.

Anaelekea ana majibu asubiri atanijibu.

Witness statement ni tofauti na Charge sheet.

Sio kweli sheria inasema nini kinapaswa kuambatana na information.

Hizi kesi zinahitaji nini kiambatane nacho huo ndio ukweli.

Pingamizi langu ni kwamba mkikubaliana na hoja yangu kesi haiwezi kusimama kunakuwa hakuna kesi maana sheria inasema Charge sheet inapaswa kujumuisha vitu gani?

Na waheshimiwa Majaji pendekezo lake ni kwamba tuliache muda huu tusubiri kwenye mashahidi huko.

Sasa mimi nauliza ili iweje? Kama zipo zinaweza kuonekana na mahakama na nina case law ku submit my submission

Hii inaweza kufanyika sasa na mwisho wa siku naomba ieleweke kwamba baadae anayo nafasi ya kujibu.

Hili shauri linaweza kumalizwa mapema tu hapa sio lazima tufike huko kwenye mashahidi kote. Awe mvumilivu tu.

Tunasubiri mahakama kutoa maelekezo.

Jaji Nduguru anasema kwa sababu mahakama imesema kuna ubishani basi uendelee kwa vile pande zote mbili zinasema kuna ubishani basi tunakuamuru uendeleee halafu mahakama itaamua. nakuamuru uendeleee tu.

Anaendelea Mhe. Lissu.

Kifungu . Cha 194, 204. 262, 266 Vya CPA. kanuni ya 7 ya kanuni za ulinzi wa Mashahidi. Waheshimiwa Majaji maelezo ya mashahidi katika kesi za jinai ni taarifa zinazohusu kufanyika kwa kosa la jinai, zinazotolewa either kwa mdomo au kwa maandishi kwa afisa wa Polisi au kwa mtu mwingine mwenye mamlaka kifungu cha 10(1) cha CPA.

Taarifa hiyo lazima iandikwe kwa namna ilivyoelekezwa kwenye kifungu cha 11(3)(4) cha CPA.

Kifungu. 11(4) cha CPA ndio kifungu proper kinachohusu mashahidi na huko nyuma kilikuwa ni 10(3) cha CPA.

Hicho kifungu ndio kinaweka namna ya kuandika maelezo ya mashahidi.

Kinasema Police officer atapaswa kuandika maelezo ya shahidi au mtu anayejua mazingira ya kosa na kuandika maelezo yake.

Kumbe anayeandika hayo maelezo ni police offer na atamuandika mtuhumiwa. Na maelezo hayo yataoneshwa au kusomwa kwa mtuhumiwa.

S. 11(6) of CPA inasema anayeandika na anayeandikwa nae atasaini. Wote kwa pamoja watafanya hivyo.

S. 11(8) ya CPA inasema kuhusu Caution. Shahidi anapaswa kukanywa.

Kwamba sema ukweli unaweza kushitakiwa.

Sasa kwa mlolongo huo niliosema hapo juu inafanywa na police officer anayeandika maelezo.

Sasa naomba muangalie witness statement za mashahidi wafuatao.

Shahidi wa 1 hadi wa 4. Akiwemo George Deputy ZCO nenda pia 13, 17, 18, 19 akiwemo ASP masalanga. Labda niseme kwa namba zilivyo. Ili nisiwachoshe majaji.

Ni wafuatao.1-4, 14 to 16, 20, 24 -26 and 28. Jumla ni mashahidi 10 wa Polisi na wote ni Polisi officers.

Na hao mashahidi wote hakuna mtu aliyewaandika hizo statement ni kwamba amejiandika mwenyewe.

Ameanza mimi ASP George nathibitisha amejiandika mwenyewe ile Caution ya kusema usiseme uongo, hapa amejikanya mwenyewe.

Yeye ndio amejiambia usiseme uongo na maelezo yako yatatumika mahakamani na endapo utasema uongo hayo yote amejiambia mwenyewe bila mtu.

Tena aliandika Caution statement ya nyongeza nayo hivyo hivyo. Kifupi alijiapisha kiapo mwenyewe.

Ukienda kwa mashahidi wote wanaofuata nao pia wote wamejiandika wenyewe.

Nataka sana niwataje majina Andrew Churu, yule George, Kaaya, Masalanga, Utufye, Mahamba na wengine wote ambao ni mapolisi walijiandika wenyewe maelezo yao.

Sasa naomba niwaonyeshe utofauti wa hayo maelezo na utofauti wa maelezo yaliyoandikwa na mapolisi wenzao wengine.

Ukiangalia maelezo ya mashahidi ambao ni raia wa kawaida yanatofautiana na maelezo ya mapolisi wenzao.

Maelezo ya AMANI MICHAEL kwenye orodha ni No. 20.

Huyu ni Detective Kopro ukisoma maelezo yake kuna askari amemuandika Kopro Robert, amemuandika maelezo Kopro Amani.

ASP Masalanga No. 21 na huyo vilevile ameandikiwa maelezo yake na another officer, nathibitisha kwa uaminifu nimemuandika na nimempa asome.

ASP. Charles Makunja kutoka kule Songea uthibitisho mimi D.cp ... nathibitisha nimemuandika maelezo na nimempa asome ameridhika yako sawa.

Sasa waheshimiwa mtapata muda kuangalia hayo niliyosema hapo juu.

Maelezo ya mashahidi yanapaswa kuandikwa kwa mujibu wa sheria kabisa na yakiandikwa yapelekwe kwa DPP na baadae yawe committed na tunafika Mahakama kuu.

Maelezo hayo yote yalisomwa Mahakama ya Kisutu kama yalivyo na yapo kinyume na sheria.

Hao waliojiandikia sio maelezo na yapo cha Sheria.

Sasa naomba nihamie kwenye maelezo ya akina P kuanzia P1 hadi P11 yalisomwa hadharani kama yalivyo na yameletwa mahakamani kama yalivyo. Yenye majina ya a
kina P.

Yanakiuka kifungu cha 194(4) cha CPA na rule 7 za kanuni ya ulinzi wa mashahidi.

S. 194 cha CPA inasema AMRI ya kuficha mashahidi hupaswi kuwatoa kabisa.

Sheria inasema maelezo hayo mtuhumiwa hapaswi kupewa pale ambapo mahakama imetoa amri ya maeneo fulani yasipewa kwa accused person.

Ndio sheria inasema hata kama sipendi.

Kanuni ya 7(3) ya ulinzi wa mashahidi inasema pia hivyo hivyo.

Kesi inapaswa kusikilizwa kwa amri husika.

Amri ya mahakama kuu katika kesi hii kwamba majina ya mashahidi yasiwepo na utanbulisho wao wote na mashahidi wote ambao mahakaama ilitoa amri ya kuwalinda haijawalinda.

Tunafahamu makazi yao, mitaa yao, kazi wanazofanya hadi namba zao za simu tumepewa.

Sasa kwa mazingira hayo maana yake mashahidi wameandaliwa bila kufuata utaratibu kabisa.

Ni wasilisho langu kuwa Waheshimiwa Majaji mna maelezo ya mashahidi ambayo yamekiuka sheria kwa mujibu wa Sheria zetu.

Maelezo yote hayo yanapaswa kuwa expunged from the record.

Sasa hatuhitahi kwenda huko maana tunaweza kulimaliza hapa.

Naomba sasa niwape authority waheshimiwa majaji.

Kesi ya Benga Said Kasamwa Abuu Rajabu abou Masoud Criminal session Case.

Kwenye hiyo kesi wakati wa Commital proceedings kwa ajili ya kesi ya mauaji taarifa iliyokuwa committed high court maelezo yalikuwa na maelezo ya juu tu.

Hiyo statement ilisomwa kwenye committal na ikapelekwa Mahakama kuu na Mahakama kuu ikasema kwasababu hakujaonekana ukurasa wa pili basi taarifa yote ikawa quashed. Iliondolewa information yote.

Jaji alisema hayo masharti ni masharti ya lazima ni lazima yafuatwe.

Hizo witness statement zote na mashahidi wote waliopaswa kulindwa na hawajalindwa ukizifuta maana yake hakuna kesi ita collapse kabisa. Out of 30 witness statement zinaondoka 23.

Nini kinabaki hapo?

Zifutiliwe mbali.

Sasa Waheshimiwa majaji naomba naomba kumalizia.

Naomba nimalize kwa swali lifuatalo.

Kifungu cha 295(1) cha CPA kinasema the information inayotakiwa kufutiliwa mbali ni ile ambayo s.294 haijazingatiwa.

Is this information capable to sustain?

Hapana haina miguu ya kusimamia hii. Ni wasilisho langu kwamba haiwezi kurekebishika.

Nimesema tangu jana, haioneshi kosa lolote la jinai, haioneshi kosa la uhaini nililoshtakiwa nalo.

Sasa unarekebishaje kitu ambacho hata sio kosa kabisa hayo maelezo ambayo wanasema niliyasema hayajafafanuliwa.

Hawakusema walielewaje nikisema kukinukisha maana yake ni nini?

Haya mambo hayawezi kurekebishika kwa hatua ya sasa huwezi rekebisha ambacho hakipo..

Hawawezi kuleta pleading mpya ya overt act.

Anaendelea Mhe Lissu

Sasa hii charge sheet is incapable of amendment na sio kingine.

S. 295 (1) of CPA charge sheet isiyoelezea kosa na kueleweka inapaswa kuwa quashed ni incurable defective information na witness statement nazo zinapaswa kuwa quashed wakati huu.

Naomba nimalizie kwa maneno haya:

Nimekaa gerezani leo ni siku ya 162 nikishitakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Nashtakiwa kwa uhaini kwa maelezo ambayo hayaoneshi kosa lolote.

Waheshimiwa Majaji nawaombeni mtumie mamlaka ya mahakama hii kufuta uonevu huu.

Whatever you do kwa haya ambayo nimeyasema naombeni mfute uonevu.

I'm an innocent man na sijakosea nchi yangu wala kumkosea mtu yeyote.

Naomba kumalizia hapo.

Majaji wanaandika hapa.

Nafikiri hatua inayofuata ni upande wa Jamhuri kuanza kutoa majibu yao (Reply Submission) na baadae wakimaliza au hata kesho Mhe. Lissu atarudi na Rejoinder wanaita majumuisho au majibu ya majibu ya serikali dhidi yake.

Tunasubiri hapa muongozo.

Jaji anaita Upande wa Mashitaka.

Anasimama Katuga anasema tulikuwa na ombi naomba niseme kama ifuatavyo

Defective ya mashitaka inaweza kuwa ni form au substance.

Sasa tunaona kama pingamizi la mwenzetu liko sana kwenye substance..

Mwenzetu amezagaaa kwenye maeneo mengi ya form na substance na leo ameongeza hoja mpya ya pingamizi pia hatukuwa na notice nayo hilo pingamizi.

Anaendelea tunaomba na sisi tupewe nafasi tuende kujiandaaa ili tujibu na ametupatia authorities nyingi sana.

Tukisema tujibu muda huu hatuwezi kujibu kwa undani kwa kila kitu alichosema, tutajibu kwa kupalaza palaza.

Tunaomba mtupatie nafasi tukapitie kwa undani sana ili kesho tuendelee au kama Mahakama hii itaona busara kutuongeza pia siku zingine tutashukuru.

Kifungu cha 302 Cha CPA, kinaipa mamlaka mahakama hii kuweza kuahirisha shauri hili.

Nawahesabu mawakili karibu saba wapo hapa eti wanapirukushana na mtu yuko jela tena mmoja tu wakat wao wapo kikundi wanasema baada ya mawasilisho yote haya hawajaona hata waanze kujibu leo na wamalizie kesho.

Jaji anamuuliza Lissu. Lissu anasema wasikilize tu wao wanataka muda gani mimi nimesema mambo mazito sana na kama mawakili 6 wa serikali wanahitaji huo muda na wanaona utawatosha kujiandaa acha tuone wataenda kujiandaa na nini?

Jaji anaandika hapa

Amesema tukutane Tarehe 18/09/2025 saa tatu asubuhi.

Jaji anasema anaomba leo tusiimbe sana baada ya muda wa Mahakama kuisha.

Leo tunaishia hapa, tuonane tarehe 18. Nawatakia wakati mwema.

Mwendelezo, utetezi wa saba: Utetezi wa saba wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 18, 2025
 
Mkuu nikupe hongera zako kuweza kutuhabarisha moja kwa moja kutoka viunga vya Mahakama

Kama utaweza, tutengenezee PDF ya mwenendo wa kesi yote ili tupate cha kuwahadithia Wajukuu zetu namna Mahakama zetu zisivyo huru

Barikiwa sana
 
Wakisoma hivi wanatamani wakuteke wakupe kesi
Ndiyo kawaida ya vilaza. Wangekuwa wana akili timamu, wangefahamu ya kwamba human beings are political animals!
Binadamu siyo ng'ombe, mbuzi au kondoo! Kutofautiana mtazamo kupo hata ndani tu ya familia. Unaweza ukatofautiana mtazamo na mke/mume/mtoto/mzazi/ndugu yako, nk.

Haya mambo ya kulazimishana kumuabudu na kumtukuza mtu mmoja; nadhani yanatafakarisha sana. Kwa sababu hayawezekani hata kidogo.
 
Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025.

Kilichojiri kwenye utetezi wa tano kipo hapa: GE2025 - Utetezi wa tano wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 15, 2025

===
Majaji wameingia kwenye ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kesi ya Mhe. Lissu kuanza. Watu wamezuiwa kuingia ndani ya Mahakama kama ilivyokuwa jana.

Imebidi Viongozi wote wa Chama na Wanachama wote ambao tayari walikuwa wameshaingia ukumbini wametoka nje kuonyesha kutounga mkono kitendo cha Polisi kuzuia watu waiingie Mahakanani.

Mhe. Lissu amesema hataendelea na shauri lolote mpaka pale watu wake wote waliozuiwa njee watakapo ruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Mahakama.
Sasa Majaji wetu wanasemaje, kuhusu Hilo la watu kuzuiwa, na watu kutoka ubalozini wapo au hawapo leo.

Hivi Mahakama zipo chini ya Polish au chini ya Mahakama zenyewe.
 
Naipenda nchi yangu Jamhuri ya Tanganyika
FB_IMG_1702085740919.jpg
downloadfile.png
 
siku za kampeni nyingi sana
 
Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025.

Kilichojiri kwenye utetezi wa tano kipo hapa: GE2025 - Utetezi wa tano wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 15, 2025

===
Majaji wameingia kwenye ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kesi ya Mhe. Lissu kuanza. Watu wamezuiwa kuingia ndani ya Mahakama kama ilivyokuwa jana.

Imebidi Viongozi wote wa Chama na Wanachama wote ambao tayari walikuwa wameshaingia ukumbini wametoka nje kuonyesha kutounga mkono kitendo cha Polisi kuzuia watu waiingie Mahakanani.

Mhe. Lissu amesema hataendelea na shauri lolote mpaka pale watu wake wote waliozuiwa njee watakapo ruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Mahakama.

Kesi imeahirishwa mpaka saa 5:08 ili majaji wafanye maaumuzi juu ya hali ya kuzuia watu nje ya mahakama.

Lakini pia kumuuliza msaidizi wa Mafwele ZCO George juu ya amri hii ya kuzuia waTanzania kuja kushudia kesi.
Nchi kweli imebakwa yani watu kuja tu sikiliza kesi wanapigwa ,wanajeruhiwa hii ni haibu kubwa kwa taifa
 
Utetezi wa sita wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 16, 2025.

Kilichojiri kwenye utetezi wa tano kipo hapa: GE2025 - Utetezi wa tano wa Tundu Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi yake ya Uhaini, Septemba 15, 2025

===
Majaji wameingia kwenye ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kesi ya Mhe. Lissu kuanza. Watu wamezuiwa kuingia ndani ya Mahakama kama ilivyokuwa jana.

Imebidi Viongozi wote wa Chama na Wanachama wote ambao tayari walikuwa wameshaingia ukumbini wametoka nje kuonyesha kutounga mkono kitendo cha Polisi kuzuia watu waiingie Mahakanani.

Mhe. Lissu amesema hataendelea na shauri lolote mpaka pale watu wake wote waliozuiwa njee watakapo ruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Mahakama.

Kesi imeahirishwa mpaka saa 5:08 ili majaji wafanye maaumuzi juu ya hali ya kuzuia watu nje ya mahakama.

Lakini pia kumuuliza msaidizi wa Mafwele ZCO George juu ya amri hii ya kuzuia waTanzania kuja kushudia kesi.
Heparin ubarikiwe sana kwa kujitolea muda wako kutujulisha neno kwa neno kwa kinachoendelea mahakamani
 
Mkuu nikupe hongera zako kuweza kutuhabarisha moja kwa moja kutoka viunga vya Mahakama

Kama utaweza, tutengenezee PDF ya mwenendo wa kesi yote ili tupate cha kuwahadithia Wajukuu zetu namna Mahakama zetu zisivyo huru

Barikiwa sana

Kwa kweli
 
Back
Top Bottom