Utengenezaji wa rangi za maji za ukutani

Utengenezaji wa rangi za maji za ukutani

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
18,684
Reaction score
45,613
Helloowww mabibi na mabwana,wakaka kwa wadada...hope mko pooa kabisaa kuelekea mapumziko ya mwisho wa wiki..
Kama ilivyo ada watu hatuachi kuhangaika na kujifunza mambo mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku,.basi na Mimi leo nimeona si vibaya niki-share na wajasiriamali wenzangu utengenezaji huu wa rangi ya maji ya ukutani..

Mie nasema hivi;kizuri shea na mwenzio...

Haya tuanze na hatua ya awali kabisa ya utengenezaji huu wa rangi ya maji
*Andaa chombo cha plastiki kama pipa
*Andaa maji safi
*Andaa mwiko mkubwa wa kukorogea
*Andaa malighafi zako
*Andaa mask kwa kujifunika machoni,puani na mdomoni(vifaa kinga)

Aina za malighafi tutakazo tumia na vipimo vyetu
1.NH3....gram150
2.Maji....lita 40
3.Tyles....gram500
4.T 102...kilo 41/4
5.Chaki....kilo80
6.Antiform....gram150
7.Emaltex....kilo7
8.Preservative...gram500

Hatua ya pili..
Hakikisha umevaa mask na gloves kujikinga wakati wa utengenezaji huu
Haya tunaendelea...
Weka preservative namba 8 kwenye chombo chako cha plastiki na uanze kukoroga taratibu ikifuatiwa na malighafi hizi namba 1 weka huku ukiendelea kukoroga,weka namba 6 huku ukikoroga,weka namba 7 hapa tumia nguvu kidogo kukoroga mchanganyiko wako,weka namba 3,4,5 na mwisho unamalizia na namba 2 mwishoni ambayo ni maji..
Endelea kukoroga mpaka utakapoona mchanganyiko wako umekuwa mzito,kisha funika vizuuuri na nasubiri kwa muda wa nusu saa...

Hatua ya tatu na mwisho
Andaa makopo yako(plastic containers)kulingana na vipimo vyako na ujazo utakaopendelea...na mpaka hapo itakuwa tayari kwa kutumiwa kwa matumizi mbalimbali

Mpaka hapo sina la ziada,.nna imani tumepata kitu japo kidogo..Mungu awabariki,.

ANGALIZO:ukiwa unafanya shughuli hii hakikisha watoto wadogo hawawezi kufika eneo hilo.TUWAJALI WATOTO WETU.

"Ujuzi hauzeeki".
 
Sasa Mother confessor kuna kitu umesahau kumalizia je ukisha changanya hizi material zote itatokea rangi gani nyeusi nyeupe au nyekundi ama kijani or ni aina gani ya rangi itatokea apa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Well,.utapata rangi nyeupe.. ukitaka rangi tofauti utaomba preservatives ya rangi nyingine,.na ukitaka kupata rangi nyingine tofauti tofauti basi utachanganya rangi na rangi baada ya kuzitengeneza rangi hizo vizuri.
 
Back
Top Bottom