Utengenezaji wa Chakula Cha Kuku

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Wakuu hili swala la Kujitengenezea mwenyewe Chakula Cha Kuku si swala la Kitoto hata Kidogo, Ni kazi Moja ngumu kabisa, kuliko hata Kufuga kwenyewe, na that is why watu wengi wanaona ni Bora kununua Chakula, kitu ambacho huwa Cost watu, Ila kwa kweli kuna Ugumu wa Aina yake katika Kutengeneza Chakula Chenye Viwabgo vinavyop Kubalika,

Kwa Tanzania sijui ila kwa Nchi Kama Kenya tiyali wao wana Maabala ya Kupima Chakula unacho jitengenezea kama Kina Viwango vinavyo kubalika na huwa kuna ghakama za kulipia kama 18000 za kitanzania

Na Utengenezaji wa Chakula Cha Kuku unahitaji mahesabu zaidi kuliko kitu chochote kile na kama ulikimbia Namba shuleni inakuwa ni Vigumua zaidi kutengenezea Chakula chenye Ubora

Na mara Nyingi njiza inayo tumika ni Pearson's Square Method hii njia inakumbukwa kwa mahesabu ya Shule ya Msingi

pearson-square.jpg


Na mara Nyingi kinacho Tushinda ni Hiki hapa

-Tunashindwa Ku constitute Micro Nutrients kama vile
1. Amino Acid
2. Trace Mineral
3. Fat anKiwango Cha maji kinacho hitajika katika hivyo vyakula

So wakuu inahitajika Elimu hasa jinsi ya Kucheza na zile namba na vitu kama vile

1. Digestible Crude Protein (DCP)

2. To determine the total digestible nutrient (TDN)

 
Ni kweli bwana chasha ni kazi ngumu...ukikosea kama ni kuku wa mayai hawatataga na kama ni wanyama hawatakua kwa mda unaotakiwa
 
Ni kweli bwana chasha ni kazi ngumu...ukikosea kama ni kuku wa mayai hawatataga na kama ni wanyama hawatakua kwa mda unaotakiwa

Ni kweli kabisa Mkuu na inahitaji Mahesabu Makali tu, huwa tunazania ni Ishu ya Kuchukua Kilo Kazaa za Dagaa na Kuchanganya na Kilo kadhaa za Mahindi na Kilo Kadhaa za Pumba, Kumbe sio ni zaidi ya Kuchanganya hivyo vitu, Ni lazima Ujue Constration iliyoko kwa kila kitu cha Kuchanganya

Na Mara Nyingi ni lazima Utumia hiyo Formula hapo Juu ili Kujua DCP inayo takiwa kwa kila aina ya Chakula Cha Kuku

Mfano kwa Chakula Cha Kuku wa Mayai ni lazima atleast CP iwe kwenye 18% sasa mziki ni hapo kwenye kuipata hiyo 18% Crude protein kwenye Chakula ulicho Tengeneza na si kwamba ni kwa kujumlisha tu Dagaa na Mashudu no,

Kwa kuku wanyama Consetrarion ya CP ni lazima iwe kati ya 22-24% ikishuka hapo ndo unakuta kuku hawaku kabisa kuku wanyama wanakuwa hawana tofauti na kuku wa Kienyeji

22-24% ni kwa vifaranga na 21- 22% ni kwa kuku baada ya vifaranga
 
Tatizo jingine kwenye Utengenenezaji wa Chakula Cha Kuku ni kwamba CP huwa ina tofautiona katika zao moja
Mfano: unaweza kuta Soya My be ya Mbeya ikawa na CP nyingi kuliko soya my be inayo limwa Dodoma na hii kwa macho huwezi tambua na unaweza kuta soya ya sehemu fulani iliathiriwa na ukame so ikawa na upungufu wa CP, na hiki ndo kinaleta ugumu sana katika kutengeneza Chakula

Na watu wengi hujikuta wanatenhegneza chakula na kuwapa kuku wao matokeo ni kuku either Kudumaa au kuku wa Mayai kuto taga kabisa, hapa tatizo ni jinsi ya Kucheza na DCP na kujua DCP[ inayo hitajika kwa kila aina ya Kuku Vifaranga, mpaka wanao anza kutaga
 
Uzuri wa jf ndo huu!ndugu yangu chasha tupe elimu uliyo nayo.angalizo.utengenezaji wa chakula cha kuku si wa kukurupukiwa!ni lazima kujipanga na akili iwe imetulia.nitaendelea kupitia huu Uzi kujifunza zaidi
 
Ni kweli ni kazi ngumu sana, Ila mimi ninacho kifanya ni Kupeleka Sample Nairobi Kenya wakapime kujua kiwango cha CP katika hicho chakula, kwa Bongo sijui kama kuna kitu kama hicho, kwa Kenya kuna Maabala na unacho fanya ni kupeleka sample na kupimwa ni ndani ya muda mfupi then wanakupa majibu na sample unaweza ituma hata kwa DHL s lazima upeleke wewe mwenyewe,

Na hiyo nda njia pekee ya Kujua kama chakula chako kinafaa kulishia Kuku au la, make tatizo liko kwenye kutambua CP na ile haiwezi tambulika kwa macho wala kwa kuchanganya changanya vyakula, ila ni kwa Kipimo maalumu,
 
Mkuu kwa anaye taka kupelekewa kwenye Maabala ya Nairobi Kenya tunaweza wasiliana make sijajua kwa Tanzania kama kuna Maabara hata ya Serikali ya Kupima DCP, ila kwa kwenye wao wanayo na unalipia kama TSH 18000 Za Bongo,
 
Kwa anye taka kutuma Sample ya chakul chake kwa ajili ya Kutetiw contct ni hizo hapo KARI Naivasha P.O. Box 25, 20117 Naivasha, Tel. 0726 264 032.

Jamaawana Maabara ya kupima DCP na unacho fanya ni kupeleka sample yachakulaulicho tenegneza wa ajili ya vifaranga au kuku wa kubwa
 
Wakuu Mtu wa Kwanza Huku Arusha aliye tuma Sample ijumaa iliyo pita, Amepata majibu yake na katika Chakula chake kuna vitu ameambiwa aongze kidogo ili kufiukia kiwango kinacho takiwa kwa ajili ya kuku na Vifaranga, amenipigia simu kunitaarifu hili,

Ila kwa kifupi ni lazima anaye tak na aliyeko siriai atume sample hapa hakuna cha Maujanja kwa sababu Zle composition zinatofautiona that is why, mfano, Mahindi my be ya Rukwa yanaweza yasiwe na protein sawa na mahindi ya Dodoma, ivyo hivyo kwa soya, Matama, na kazalika so ni lazima upeleke sample kwa kutumia hizo anuani,
 
Anaejua jinsi yakutengeneza chakula cha kuku wa kienyeji badala yakwenda kununua madukani jamani msaada
nini na nini vinachanganywa na kiasi chake

mungu akubariki
 
Mkuu hivi vitabu na maelezo tuliweka kwenye uzi wa Kubota, nakuwekea tena kina maelezo yote banda chakula na vipimo vyake. Karibu tufuge
 

Attachments

  • ufugaji-bora-wa-kuku-wa-asili.pdf
    1 MB · Views: 856
  • ufugaji bora wa kuku Heifer international.pdf
    2 MB · Views: 836
Kwanini usiwape tu hiki cha dukani kama kuku wako hawazidi 10? Binafsi kuku wangu nawapa hiki hiki cha madukani,nyanya.mchicha,ubwabwa,ugali na pumba za mahindi.
Nalog off
 
Kwa mwenye kauwezo alichopewa na Allah swabaanah wataala jamani jinsi yakuchangnya nakupata mlokamili wakuku was kienyeji nimechoka nahii biashara yakunua vyakula
Pls msaada
 
Karibuni hapa tupeane mawazo/ujuzi/mbinu za kutengeneza chakula cha kuku tajwa mimi huwa natengeneza hivi kwa kuchanganya vifuatavyo na huwa kuku wa kienyeji wanataga balaa..
1.Chenga za mahindi(kubarazwa) kg 30
2.Mtama Kg 10
3.Pumba za mahindi Kg 21
4.Dagaa(Kubarazwa) Kg 15
5.Mashudu(alizeti kubarazwa) Kg 20
6.Premix Kg 0.5
7.Chumvi Kg 0.5
8.Chokaa Kg 3
Jumla Kg 100
 
asante MOPAOZI, lakini hicho kiwango unachotengeza ni kwa idadi
ya kuku wangapi na kinatumika kwa muda gani
 
Karibuni hapa tupeane mawazo/ujuzi/mbinu za kutengeneza chakula cha kuku tajwa mimi huwa natengeneza hivi kwa kuchanganya vifuatavyo na huwa kuku wa kienyeji wanataga balaa..
1.Chenga za mahindi(kubarazwa) kg 30
2.Mtama Kg 10
3.Pumba za mahindi Kg 21
4.Dagaa(Kubarazwa) Kg 15
5.Mashudu(alizeti kubarazwa) Kg 20
6.Premix Kg 0.5
7.Chumvi Kg 0.5
8.Chokaa Kg 3
Jumla Kg 100

Mkuu ahsante kwa kutuwekea formula yako ambayo imekuletea matokeo mazuri. Ila naomba ufafanuzi kidogo. Hivyo ulivyoorodhesha ukishavichanganya na kupata hizo kilo 100 unatakiwa uvisage kwanza kwa pamoja au ukishamaliza kuchanganya basi unawapatia kuku? Na je hii formula ulishawahi kui apply kwa kuku wa kisasa wa mayai? Kama ndivyo vipi matokeo yake yalikuwa mazuri kama ilivyokuwa kwa kuku wa kienyeji?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom