mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,995
- 3,402
Ila fahamu kuna miradi wameitekeleza kwa wakati na kwa ufanisi,nyumba za wanafunzi,udsm,ikulu ya rais Dodoma,wasilaumie moja kwa moja,pengine kuna tatizo lisilo lao,sema mkubwa hakoseiJana mh. Rais kaja juu.
Idara yake penzi ya TBA inasuasua.
Huko Magereza Ukonga ligwaride la ujenzi wa nyumba unaenda kwa mwendo wa kinyonga!
TBA walipewa, CASH, bilioni 20 kujenga nyumba za wana Magereza mwaka 2016, mpaka sasa mradi umefikia 35% ya maendeleo.
Mradi majuzi ulitembelewa na waziri mdogo Mambo ya Ndani, ndg Masauni.
Kwa spidi ya utekelezaji wa mradi TBA itawachukua miaka 12 kukamilisha kazi, leo ni mwaka wa 3-4 toka kazi ianze.
Lakini ngoja kidogo mzee, mh Rais.
Si tulikutonya hapa JF na kwingineko mitandaoni?
Ile ilikuwa early warning.
TBA sio mkandarasi, ni wakala wa nyumba za serikali , na tulijua hilo walitambua vema, maana si mgeni Wizara ya Ujenzi.
WAKALA TBA kazi yake ku manage masuala ya nyumba za serikali, si kujenga.
Vituko vilianza na mabweni ya chuo kikuu Mlimani.
Sitaongelea pesa ndogo kiduchu zinazosemekana kutumika, lakini ni wazi , kazi ilikuwa chini ya viwango
Mwanafunzi aliyelalamika mitandaoni juu ya kupasuka kuta, aliwekwa ndani, lakini si kwa amri yako , ni wale wapambe wasiotaka kukutonya ukweli.
Na kwa kweli hawakutakii mema.
Mawazo yangu mzee, TBA warudi kwenye kazi yao ya Uwakala wa nyumba za serikali, kazi za Ujenzi wawaachie wabobezi, Makandarasi.
Sent using Jamii Forums mobile app
