Utendaji mzuri wa Serkali ya awamu ya tano umebadili siasa za Tanzania

Kwa ujumla sitaki kujikita zaidi kuelezea juu ya namna gani utendaji kazi mzuri wa serikali ya awamu ya tano umeweza kuleta mabadiliko katika ukusanyaji mapato, kudhibiti mianya ya rushwa na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Najua kila mtu anajua kuwa watu waligeuka michwa ya kutafuna pesa za umma na hii ilisababisha serikali kushindwa kutekeleza miradi mingi ambayo ni muhimu kwa maisha ya watanzania. Lakini kwa kipindi cha miaka mitano tumeona mabadiliko makubwa sana.

Huko nyuma tulizoea kusikia, kuna upigaji Halmashauri fulani ukiibuliwa na wapinzani, mara wizara fulani kuna ufisadi wa kuogofya lakini leo hii tunaona kila pembe ya nchi,wanaojaribu kukwapua pesa ya umma wanadakwa na kupandishwa kizimbani.

Badiliko hili limefanya wapinzani kukosa kick za kisiasa na sasa wamekuwa kama waimba taarabu ambao wanadhania siasa ni mipasho.Kwamba siasa ni kupashana vijembe ambavyo havina mbele wala nyuma hata kama havina umuhimu kisiasa.

Manoni; Habari ya kuanza kuleta mipasho ya kufatilia kiongozi wa nchi kasema nini kanisani ni kufiliska kisiasa. Kama mnataka game anzeni upya kunadi sera zenu tuone kama wananchi wataitikia.
Teh!
 
Back
Top Bottom