Utekaji huu una baraka za serikali?

Wanachohitaji watanzania kwa sasa ni serikali ya CCM kumwachia msanii Roma ambaye walimteka Jumatano jioni. Usitake kututoa kwenye mjadala kwa habari zako za kipuuzi.
 
Jana
namba take kwa sasa haipatikani kaka
 
Hawana walichopata zaidi ya kubebeshwa madawa ya mwenyekiti
Tupe historia ya Home Shopping center na GSM halafu ni viongozi gani wanashirikiana nao utapata jibu
 
"Utekaji kufanyika katika mazingira ya sasa ya Bashite Bashite kunaacha maswali mengi kuliko. Majibu
 
Watanzania tukiendelea kuzoea hii hali na kuwa sehemu ya utamaduni wetu katika kutekana nchi haitakalika,isitoshe kwa serikali kuishia kutoa matamko na kukanusha ilihali kuna makosa ya kiufundi lukuki yanayofanyika kiasi cha wananchi kutilia shaka uendeshaji wa serikali yao.

Tunalichukulia kwa mzaha na kulifanyia kejeli tukio hili laiti likikukuta ndani ya familia yako mzaha unaoufanya sasa usingethubutu kuufanya tena. Usalama wa raia ni jukumu letu sote lakini vipo vyombo ambavyo ndivyo vimepewa jukumu hilo,ikiwa utendaji wake unasubiri matamko kwanza ndipo liingie kazini usalama wetu uko maskakani.

Bunge kupitia kamati yake ya mambo ya ndani inapaswa kushughulikia tatizo hili kwa ufanisi,Leo wamekufa watu kwa kuchinjwa kama mbuzi,wengine ndo hao wanatekwa,kwa nini bunge lisizuie hiyo taharuki
 
Mkuu napata kigugumizi na ukakasi kuamini kuwa upinzan wametekeleza hili kwa kujinufaisha kisiasa ili kuichafua serikali kama ni hivyo basi RC ameeleza kuwa kabla ya j3 watakuwa wameshaonekana wote tena wakiwa hai huoni kama RC anafaham picha nzima ya tukio na huenda ikawa kuna mkono wake kwa 99% kuhusika na hili??
 
Haiwezekani mtu ambaye Simu yake iko hewani asipatikane kwa muda wote huo kama kweli mamlaka zinazohusika zinazohusika zimemtafuta! Simu yake itakuwa imeachwa hewani ili itumiwe kuwanasa wengine hasa members wa magroup ambayo Roma alijiunga!
Ifahamike tu kuwa watanzania si wajinga kiasi hicho! Bila shaka wengi wanakijua kinachoendelea!
 

Duh! Hilo povu. Ungetumia kufulia chupi zako ingekuwa bora zaidi kuliko kulimwaga hapa jamvini.
 
Usalama wa raia ni suala mtambuka sana katika kufikia malengo tarajiwa,unapozungumzia usalama unazungumzia uchumi,unazungumzia jamii unazungumzia amani. Panapokosekana usalama kuna athiri uchumi ambao mazingira yake yanakuwa si rafiki kwa uwekezaji. Kijamii usalama unapokosekana jamii inagawanyika na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe(civil war). Leo ukibeza usalama umebeza uchumi,umebeza amani pia
 
Muuwaji/mtekaij ni serikali period, mengine jadilianeni muda upite!
 
Ni upuuzi mtupu kuamini eti serikali inashiriki upuuzi huu. Serikali kazi yake ni kulinda usalama wa raia na mali zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…