Utekaji huu una baraka za serikali?

Utekaji huu una baraka za serikali?

Wanachohitaji watanzania kwa sasa ni serikali ya CCM kumwachia msanii Roma ambaye walimteka Jumatano jioni. Usitake kututoa kwenye mjadala kwa habari zako za kipuuzi.
 
Jana
Magazeti yaanze kuajiri polisi/wapelelezi/wanajeshi/wanausalama wastaafu na kuwapa mafunzo ya uandishi,pia inunue mashushushu serikalini maana hii nchi tulipofikia tunahitaji waandishi ambao wakifika mahali kufatilia habari wanakuja na mambo kumi badala ya jambo moja.
Hii nchi hatuaminiani tena,unampa mtu kazi na unamlipa ili ashughulikie matatizo yako baadae anageuka na kuanza kukushughulikia wewe...juzi Nape alipotishwa ilipasa waandishi wamfatilie wale waliokuja nabastola,kufatilia gari lao,kazi Yao,majina na wasifu Wao...chaajabu Wao walibaki kumng'ang'ania nape aongee!!
Leo wanakosa kabisa clue ya wapi alipo roma wakati kuna simu na kutrack simu inawezekana...tunahitaji waandishi Wa ukweli sio mareporter wakawaida
namba take kwa sasa haipatikani kaka
 
Hawana walichopata zaidi ya kubebeshwa madawa ya mwenyekiti
Tupe historia ya Home Shopping center na GSM halafu ni viongozi gani wanashirikiana nao utapata jibu
 
"Utekaji kufanyika katika mazingira ya sasa ya Bashite Bashite kunaacha maswali mengi kuliko. Majibu
 
Watanzania tukiendelea kuzoea hii hali na kuwa sehemu ya utamaduni wetu katika kutekana nchi haitakalika,isitoshe kwa serikali kuishia kutoa matamko na kukanusha ilihali kuna makosa ya kiufundi lukuki yanayofanyika kiasi cha wananchi kutilia shaka uendeshaji wa serikali yao.

Tunalichukulia kwa mzaha na kulifanyia kejeli tukio hili laiti likikukuta ndani ya familia yako mzaha unaoufanya sasa usingethubutu kuufanya tena. Usalama wa raia ni jukumu letu sote lakini vipo vyombo ambavyo ndivyo vimepewa jukumu hilo,ikiwa utendaji wake unasubiri matamko kwanza ndipo liingie kazini usalama wetu uko maskakani.

Bunge kupitia kamati yake ya mambo ya ndani inapaswa kushughulikia tatizo hili kwa ufanisi,Leo wamekufa watu kwa kuchinjwa kama mbuzi,wengine ndo hao wanatekwa,kwa nini bunge lisizuie hiyo taharuki
 
Mkuu napata kigugumizi na ukakasi kuamini kuwa upinzan wametekeleza hili kwa kujinufaisha kisiasa ili kuichafua serikali kama ni hivyo basi RC ameeleza kuwa kabla ya j3 watakuwa wameshaonekana wote tena wakiwa hai huoni kama RC anafaham picha nzima ya tukio na huenda ikawa kuna mkono wake kwa 99% kuhusika na hili??
 
Haiwezekani mtu ambaye Simu yake iko hewani asipatikane kwa muda wote huo kama kweli mamlaka zinazohusika zinazohusika zimemtafuta! Simu yake itakuwa imeachwa hewani ili itumiwe kuwanasa wengine hasa members wa magroup ambayo Roma alijiunga!
Ifahamike tu kuwa watanzania si wajinga kiasi hicho! Bila shaka wengi wanakijua kinachoendelea!
 
PART A
Hivi tuweke ushabiki wa kichama pembeni uhusu ROMA.......
Je,ni serikali ndio inahusika juu ya UPOTEVU WAKE???na kama ni serikali ni sababu ipi hasa imefanya serikali ihusike juu ya UPOTEVU WAKE????na kama ni kwa sababu ya mziki wake,je serikali haikuwa na mamlaka ya kuzuia huo wimbo wake usichezwe redioni au ROMA mwenyewe kupewa onyo....na kama kweli ni serikali ndio imehusika juu ya UTEKWAJI wake kwanini still SIMU YAKE ILIENDELEA KUTUMIKA??????huo utakuwa ni uerevu gani wa kipuuzi kwa WATEKAJI wa serikali???????
PART B
Je upande wa pili hauwezi husika juu ya upotevu wa ROMA???na ni kwanini nasema ni upande wa pili INAWEZEKANA WAKAHUSIKA???nasema ni upnde wa pili kwa sababu inawezekana kabsa hawa upande wa pili wakahusika kwa kiasi kikubwa sana ili kujinufaisha wao kisiasa....Kwanini nasema kujinufaisha wao kisiasa....
Nasema hivi nikiwa na maaana ya kwamba WANAWEZA MTEKA ROMA ili kutengeneza tension fulani au kujaribu kuichafua SERIKALI HII KIMATAIFA NA KUFIKIA HATA KUNYIMWA BAADHI YA MISAADA na ambayo mwisho wa siku itaiweka nchi katika wakati mgumu sana na kuwaumiza wanachi wa hali ya chini na kupelekea WANANCHI kuichukia serikali iliyopo MADARAKANI maana hii nayo inawezekana kabsa ikawa ni njia BORA KWA WAO KUJINUFAISHA NA KUPAMBANA NA MAGUFULI maana kaishawashika vibaya mno mpaka sasa hivyo wao kutokuwa na plan B ya kupambna na MAGUFULI itakuwa ni janga sana kwao....NDIO MAANA TUNASEMA INAWEZEKANA KABSA HII TEKA TEKA IKAWA NI PLAN B yao.......
sasa jiulize serikali iliyopo madarakani ikichukiwa hii itakuwa ni faida kwa upande upi????JIBU UNALO MWENYEWE KWA MAONI YANGU hili la ROMA lina ukakasi sana as well as SUALA LA BEN sema tu tatzo kubwa tulilo nalo sisi WATANZANIA tuna mahaba ya KIPUUZI kupita maelezo yaani hatutumii vichwa na bongo zetu kudadavua mambo.....
PART C
Inawezekana ROMA mwenyewe kajiteka kutafuta KIKI au kutafuta HURUMA za mashabiki kwa wimbo wake uo aliokuwa ana rekodi MAANA hakuna kinachoshindikana katika hili.....

kibaya zaidi HUMU NDANI SIKU HIZI kila baya ndani ya NCHI HII anaenyooshewa kidole ni MAGUFULI hivi huyu MAGUFULI mnaemnyooshea kidole yeye haamini kama KUNA MUNGU??mpaka afikie hatua ya kudhuru au kuteka KIJANA wa watu mwenye familia inayo mtegemea???kwani kwenye hii DUNIA WA NGAPI WAMETUKANWA na kwani MAGUFULI yeye ndiye wa kwanza kutukanwa kwenye nchi hii???
KINGNE...kwanini kila BAYA NDANI YA NCHI HII NI CCM????kwani KUNA TOFAUTI GANI KATI YA CHADEMA NA CCM linapokuja suala la uhai wa binadamu????KAMA BAYA LINAWEZA FANYWA NA CCM vipi lisifanywe na CHADEMA?????......Kama ROMA katekwa na CCM kulinda maslahi ya CCM vipi SAANANE asidhuriwe na CHADEMA kukinufaisha CHAMA???????
KIBAYA ZAIDI UNAWEZA KUTA HATA HUO WIMBO alikuwa anataka REKODI ROMA kawa pressurised na hao CHADEMA kumbe behind the scene wana lao jambo kama ambavyo SAANANE alivyokuwa akitumiwa na CDM kutukana RAIS kumbe behind the scene wamemuandalia jambo........HAKISHINDIKANI KITU.....
Acheeni upuuzi hii nchi yetu sote

Duh! Hilo povu. Ungetumia kufulia chupi zako ingekuwa bora zaidi kuliko kulimwaga hapa jamvini.
 
Usalama wa raia ni suala mtambuka sana katika kufikia malengo tarajiwa,unapozungumzia usalama unazungumzia uchumi,unazungumzia jamii unazungumzia amani. Panapokosekana usalama kuna athiri uchumi ambao mazingira yake yanakuwa si rafiki kwa uwekezaji. Kijamii usalama unapokosekana jamii inagawanyika na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe(civil war). Leo ukibeza usalama umebeza uchumi,umebeza amani pia
 
fjjjjj.JPG
Duh! Hilo povu. Ungetumia kufulia chupi zako ingekuwa bora zaidi kuliko kulimwaga hapa jamvini.
Matusi ya nini tena?????WEWE AKILI ZAKO ZIMEKAA KIBANGE BANGE
 
Muuwaji/mtekaij ni serikali period, mengine jadilianeni muda upite!
 
Ni upuuzi mtupu kuamini eti serikali inashiriki upuuzi huu. Serikali kazi yake ni kulinda usalama wa raia na mali zao
 
Back
Top Bottom