sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Nimeisikiliza hotuba ya Mh. Lema bungeni kwa mara ya kwanza akichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu baada ya kutoka kifungoni/mahabusu miezi minne,nimetafakari sana juu ya kupotea au kutekwa kwa watu mbali mbali ambao wanahusishwa na kuikemea serikali.
Hofu yangu imejikita kwenye mambo makuu manne kama ifuatavyo
1) . Usalama wa raia na mali zao upo salama kama inavyobainishwa na katiba ya JM.
2) . Hofu tunayojazwa Watanzania ni kwa mujibu wa sheria au ni utashi wa MTU
3) . Nini kazi ya bunge kama chombo cha uwakilishi kwa wananchi.
4) . Hatima ya uvunjivu huu wa amani ni nini
Nazungumzia usalama ambao umejikita katika kutekeleza haki za msingi za binadamu ambazo kupitia kwayo Tanzania imesaini mkataba wa amani wa Geneva,mkataba unaolinda haki za binadamu zinazozuia mtu kudhalilishwa na kutwezwa utu wake,ambayo haki ipo pia kwenye katiba yetu.
Inapofikia nchi,wananchi wake wanapotezwa/kutekwa ilihali vyombo vya dola vilivyopo chini ya serikali vipo na hakuna kauli ya chombo chochote wala serikali kukemea ugaidi huo juwa kuwa hali ya nchi kiusalama ni tete. Kama hali si tete basi kuna mawili,kama serikali haihusiki basi serikali inawajua wahusika ila inawaogopa.
Haitoshi wabunge tena wa upinzani wakemee bungeni lakini bunge ambalo ni chombo cha utetezi na uwakilishi wa wananchi linyamazie bila kuchukua maamuzi sahihi dhidi ya matukio haya,kisha tuseme nchi iko salama.
Mkuu wa mkoa alipowatuhumu wabunge wanasinzia bunge lote lilizizima hatimaye mkamwita kwenye mahakama yenu,iweje usalama wa raia mnao waongoza upo mashakani lakini bunge lipo kimya,au kutekwa/kupotezwa kwenu kuna maslahi nanyi.
Matukio ya uvunjaji amani yanayoshamiri siku hadi siku ilihalî vyombo vyenye mamlaka na uzuiaji wa matukio hayo vipo chini ya serikali, na kazi ya bunge ni pamoja na kuisimamia serikali,iweje bunge lishindwe kuiwajibisha serikali kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusimamia haki za usalama wa raia wake,tukasema nchi ipo salama!
Ikiwa bunge linalotunga sheria lakini linaogopa kuitumîa sheria kuibana serikali kuna haja gani ya kuwa nà chombo hicho. Kama limeshindwa hata kuisimamia katiba na kuifanya katiba kitabu cha hadithi za kufikirika,sisi raia tusimamia mamlaka ipi kujitetea juu ya usalama wetu.
Tujitazame tulipojikwaa,tukizoea halo hii nchi hataikalika.