Uteja wa simu wamponza bibi harusi, atalikiwa saa chache baada ya ndoa kwa kuchat usiku mzima

jr.kiyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
785
4,847
Hii imemgharimu bibi harusi aliyekesha akipokea salamu za pongezi kwenye simu na kumsahau mumewe.
Fuatilia kisa hiki…!
Mwanaume mmoja ameamua kumtalakisha mkewe saa chache baada ya kufunga ndoa, kwasababu mkewe huyo mpya alitumia usiku wao wote wa ‘fungate’ kuchat na rafiki zake.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, bibi harusi huyo alikuwa busy akipokea salamu za pongezi kutoka kwa rafiki yake akimsahau mumewe aliyenaye chumbani muda huo.

“Bwana harusi alijaribu kusogea karibu naye na kimahusiano, lakini alishitushwa kuona mkewe anampotezea, hajibu anachoulizwa au hata kuonesha vitendo,” ndugu wa Bwana harusi aliiambia Al Watan.

“Mwanaume alipomuuliza kama rafiki zake ni muhimu kuliko yeye, alimjibu ndio,” walisimulia mkasa walioelezwa na bwana harusi.

Mahakama ya mwanzo katika eneo hilo imejaribu kuwasuluhisha ili waendelee na ndoa yao, lakini mwanaume ameendelea kushikilia msimamo wake wa talaka.
 
huyo bwana atakuwa alikuwa ame mkinai tu ghafla sasa amepata sababu ya kutokea!
 
Siku muhimu inatakiwa simu zote zizimwe,..bibi harusi alikuwa Hana kungwi nini?..ha ha ha...
 
Mhhhhhhhhhh,jamani au alikua hamttaki mume? manake siku ya ya Ndoa na Fungate cm ya nini jamani? unakuala Happy mwanzo mwishoooooooooo utakuja kuwaeleza nini wajuku zako siku yako ya Honeymoon ulienda wapi na ukafanya nini..
 
Wanajitoaga fahamu mapema sana...
Angepewa talaka 3 kwa mpigo ili akiolewa tena ajifunze namna ya kuishi na mme.
 
Yawekana walianza mahusiano Muda mrefu hivyo wakawa wamechokana ndo maana mke alimwambia mmewe kuwa marafiki ni bora kuliko yeye
 
Ndiyo faida ya kufunuana na kufunikana kabla. Wangekuwa hawajafanya hivyo kabla, ingekuwa mwendo wa kubiringishana kitandani, kila mmoja akijaribu kuonyesha ufundi wake.
 
Kama bibi harusi kasema rafiki ni bora kuliko mume, then jamaa ana haki ya kukasirika.
 
Hata mimi ningempiga chini...Sasa kama unamuuliza marafiki zako ni bora kuliko mimi anasema ndio unakaa nae wa kazi gani?
 
Kwa jibu hilo kwakweli ningekuwa mimi ningemfulumsha hata kabla hakujakucha!
 
Ninafsi mimi ningempa talaka na simu ningeipasulia mbali.... allaaa!!!
 
Ndo tatizoo la kuwaa na uhuruu Mkubwa katikaa maamuzi yakoo bilaa kuwashirikisha wenye busara zaidi yako na pia MUNGU!.....

Ndoaa inachangamoto nyingi saana na ukiamua kujiingiza huko(kwenye ndoa) ni lazima uuvue ubinafsi wako kwanza na ku-fight 4 ndoa yako.....

MUME na MKE woote hawakuwa tayari kwa ndoa!.....

Huwezi muacha mkeo kwa jambo la kitoto namna hiyo kiurahisi hivoo labda kama haujafundwa!..(maana lilikuwa ni jambo la kumuweka mkeo #incontrol)...
Maana angeweza kumnyang'anya simu bi harusi na kutatua tatizo lililopo.
Na kosa la bi harusi ni kuwa na lugha ya ajabu kiasi kile!.
Mie naamin kila MTU akiwa na furaha ya kupitiliza ana jambo analopendaa kulifanyaa!..
Kamaa ilivo kwa bwana harusi alivoona furaha yake ya ndoa itakamilikaa kwa ku-geuzanaa na mkewe...vivo hivoo mkewe labda furaha yake hukamilikaa kwa kuwaoneshaa wenzake(marafiki+ndugu)...

So lilikuwa ni jambo la kutumia busara zaidi kuliko kukombilia TALAKA.
 
Back
Top Bottom