Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Baada ya mashambulizi ya Sept 11 2001 ilikuja kufahamika kati ya magaidi 20 waliotekeleza mashambulio hayo 19 walikuwa ni raia wa Saudi Arabia, wote tunajua baada ya ugaidi huo mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha yao huko Afghanistan, Iraq nk.
Leo tumeona nchi ikitumika tena kwa kutaka kuleta vita vya kinyuklia mashariki ya kati kwa kutoa kisingizio kuwa Iran imeshambulia vituo vyake vya mafuta. Huu mpango wa utawala huu ukishirikiana na Israel ni baada ya kuona mahusiano ya serikali ya Marekani na Iran yalikuwa yanaanza kuimarika na hata kufikia hatua ya Rais Donald Trump kumtimua kazi aliyekuwa mshauri wake wa usalama John Bolton ambaye alikuwa mstari wa mbele kutaka nchi ya Iran ishambuliwe.
Dunia nzima inajua serikali ya Saudi Arabia na washirika wake unyama wanaoufanya dhidi ya watu wa Yemen ambapo mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia wameuwawa pia. Leo wananchi wa Yemen wakijibu mapigo wanakuwa magaidi na Iran inasingiziwa kuwa ndio imeshambulia.
Dunia isitegemee kuwa salama chini ya hawa wafalme Bin Saudh wa Saudi Arabia.