Utawala wa Majimbo ni wazo zuri, shida ni Jamii kupumbazwa na watawala

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,734
CCM walisha brainwash sana raia kwa kiasi kwamba chochote wanacho tamka huwa inaonekana ni sawa, Walianza kwa Ishu ya Amani kwamba mkichagua Upinzani vita itatokea Tanzania na kweli rai walivyo na uelewa mdogo wakanunua hio Idea na wanaitumia hadi leo hii kuhadaaa raia na mambo ya amani huku wao wakichota pesa kwa mifuko.

Swala la Majimbo nalo raia wana brainwashiwa sana Ohoo kutatokea vita, ni ukabila mara imepnda ikashuka, haya yote ni hadaaa tupu ili watu wenye uwezo finyu wanunue hilo wazo na watawala waendelee kuneemeka, kukaa miezi mitatu Dodoma ni utajiri mkubwa sana.

Kenya Katiba yao Mpya imetengeneza count, ni sawa na majimbo sema wao wanatumia neno count, Hizi Count zina Magavana wao na zina MCA ni kama madiwani vile.

Kila count ina bajeti yake na inapanga cha kufanya, kwa kifupi count zina jiamulia nini cha kufanya na nini sio cha kufanya.

Tanzania sera ya Majimbo ni Idea nzuri sana shida ni jamii ambayo iko brainwashed sana sana na haioni umuhimu wake. Ndio maana Wabunge wanakutana Dodoma kujadili bajeti ya kujenga natundu ya vyoo kule Uvinza, au kujenga kivuko cha waenda kwa miguu kule Sumbawanga, huu ni ujinga sana Bunge linakaa miezi mitatu kujadili vitu ambayo vilipaswa kujadiliwa hata na Madiwani ila wanakaaa miezi mitatu kuvijadili, hawa ndio wanauzia rai uoga.

Pia Sikubalini na mfano unakuta watu ni Wamasai unawaletea Mkuu wa Mkoa Msukuma au Mchaga kuja kuwatawala, hawa walipaswa kutawaliwa na Mmasai mwenzao ndio anaye jua shida zao ndio anaye jua kila kitu kuhusu wao.

Watu wana mila zao na mfumo wao wa Maisha unawapelekea Mkuu wa wilaya mwenye mila na utamaduni tofauti akifika kule ana force sasa raia wale waachane na mila zao wafuate Mila anazo amini yeye, hii ni mifumo ya kikoloni.

Tunafurahia sana kusikia Mbunge anasimama Dodoma pale anaulizia ujenzi wa karavati jimboni kwake Karagwe, hii inatuhusu nini sisi raia labda wa Tanga? Hivi ujenzi wa karavati Karagwe unatuhusu sisi watu wa Arusha?Haya ni maswali ya kuulizwa na Madiwani. Wabunge wanapaswa kuuliza maswali ya Sera tu.

Bunge la Kenya huko walisha toka miaka mingi sana huwezi sikia ujinga huo tena eti waziri anaulizwa mashine ya Xray kwenye zahanati ilioko Tarime,Kenya hio ni kazi ya Gavana na wale MCA ndio kazi yao kumuuliza Gavana wao wakiwa kwenye vikao vya count na sio kumuuliza Waziri.

Bunge la Kenya hawatumii miezi mitatu eti kwenye kujadili Bajeti na kuuliza maswali yanayo pasws kuulizwa hata na Mtendaji wa kijiji.

Kenya Waziri anaulizwa mambo ya Kisera pekee yake na sio mambo ya makaravati sijui mashine ya Xray.

Tuko zama za giza sana Tanzania na Mungu atusaidie sana.

Sera ya Majimbo ni nzuri sema tuko kwenye jamii ambayo bado tuko zama za giza na tunauziwa uongo tuna nunua bila sisi wenyewe kufanya utafiti.
 
Ni ukweli unakuta waziri kuulizwa maswali yanayo husiana na kijiji na mara nyingi huwa wanatoa majibu ya uongo tu na kweli maswali mengine hayahusu watu wengine. Mbunge anauliza swali kwamba kijiji chake hakina barabara haya ni maswali basi ya kuulizwa kwenye vikao vya Halimashauri huko na sio kuja kuyauliza bungeni, tuna safari.
 
Hata kama una hoja nzuri lakini uwasilishaji ndio mbaya sana.

Kwanza, sijapendezwa na namna unavyotaka tufanye kama Kenya utafikiri Tanzania ni sehemu ya Kenya. Hapa ungejikita kutumia Kenya kama mfano tu huku ukilinganisha na Mazingira ya kwetu. Wewe ni mbona Kenya ...., Mbona Kenya...

Pili, Sera itakuwa ni nzuri tena zaidi kama ikitumika kwenye mazingira ya kwetu. Yote yanayosema kama hasara ziangaliwe kwa makini kwa sababu kubomoa ni rahisi kuliko kujenga.
 
Back
Top Bottom