Utawala wa dunia chanzo ni uzuri wa maisha na uoga wa kifo

emavalery

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
628
1,237
Habari ya leo Ndugu zangu,

Mambo yamekua mengi kidogo dunia ya leo, wakati kuna pande mbili zinavutana juu ya uhalali au ufanisi wa chanjo hizi za corona, kuna wale wanagoma kuchoma sindano wakisema ni Mipango ya kibinadamu zaidi na sio kuutokomeza ugonjwa huu juu ya uso wa dunia, wakiendelea kutuacha na maswali mengi na wengi wakishindwa waende wapi, ila afya inabakia chaguo la kwanza.

Katika mijadala mingi, nikawaza kitu kimoja cha tofauti kabisa ambavyo vimenifanya niweke bando langu na muda wangu niandike hiki, kinaweza kisilete maana kwa wengi ila kwa wachache nitafurahi tukipeana machache juu ya hii dunia na ulimwengu kwa ujumla.

Moja:
Nadharia ya Maisha, kwenye hili namaanisha tumekuzwa na kuaminishwa kuwa sehemu hii ndio sehemu nzuri na njema yenye kila uhitaji wa kila nafsi kuendelea kuishi hapa, nafikiri sikosei ni kweli..kwa mtazamo huu, nikafikiria je tungekuzwa tuujue upande wa pili ambao tukienda utakua mzuri zaidi, tusingefurahia kukaa hapa na tungetamani tufe ili twende upande wa pili..natoa mfano hapa, tukiwa vijijin tuliambiwa mjini kuna maisha mazuri, hvyo tukabaki kijijini ila tukitamani kwenda mjini siku moja na ilikua hvyo kwa wengi, hata haya maisha ingekua wajua ukifa ndio kuna next good life,..leo watu wasingehofu kufa na mambo ya chanjo wasingejali hata kidg, kuitimisha hapa naona maisha ya kukuzwa na kuaminishwa dunia ndio sehemu salama sio sahihi tungeachwa huru maana tulipotoka hatukujua chochote.

Pili: Uoga wa kifo.
Hapa naangalia juu ya hili jambo la kifo ndio linafanya watu wengi kujawa hofu isio na msingi wala logics zozote, na uoga huu ndio unatumika sana kutufanya tuwe watumwa wa nadharia nyingi hapa duniani, ingekua tofauti hakika nobody angeelewa ukimwambia habari za ukifa kuna moto au pepo, haya mambo ndio yanagharimu hii dunia..

End, Sioni dunia ikiwa salama miaka mingi huku bado tukiendelea kuamini kuwa hapa ndio sehemu salama na uoga wa kifo ukie delea kuutawala ulimwengu huu.

Wenye hizi siri, watabakia kuzitumia miaka 3000 hapa duniani, note:Dunia haiishi leo wala kesho, bado ipo sana tena sana.

Karibuni kwa lolote.
 
Yamepita mengi sana na yatakuja mengi sana ila Dunia na vitu vyake haitoisha mpaka pale muumba aridhie.
Ila hili suala la chanjo ni geni bado kwetu wacha tuone matokeo yake
 
binafsi naamini moto na pepo havipo, naamini mungu ametupa pande mbili za maisha

1. maisha ya kimwili ambayo yanaexpire date
2. maisha ya kiroho ambayo ni ya milele.
Exactly, hamna moto wala pepo...na maisha baada ya haya nahisi ndio mazuri zaidi, maana ni milele.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom