Utawala unavyobadilika ndivyo chawa pia wanavyobadilika

Utawala unavyobadilika ndivyo chawa pia wanavyobadilika

Bwana Kheri

Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
26
Reaction score
50
Katika utawala wa Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuna watu walikuwa ni lulu jamani. Kila kitu kizuri mtaani ni chao. Kila jambo kubwa na nyeti ni lao. Nisemacho hichi, utamkumbuka huyu bwana Riz1. Alitamba na madaraka ya mzee yakamtambisha haswa. Ingawa mambo mengine alizushiwa tu, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba yeye licha ya kuwa mtoto wa Rais, bali pia alikuwa chawa haswa wa rais wetu mstaafu ambaye kwa bahati nzuri yeye alikuwa baba yake.

Nadhani mtakumbuka hadi miradi mikubwa ilidaiwa hadi bwana Riz1 ahusishwe ndipo ikubalike katika maeneo mbalimbali ndani ya serikali au kwenye sekta binafsi. Nilishika kichwa nilipokuwa Mwanza kwa mapumziko kipindi fulani nikaambiwa hata hoteli ya Malaika eti ni ya Riz1. Vituo vyote vya mafuta ama vyake binafsi au anahusika navyo kwa namna moja ama nyingine.
Hili linaweza kuwa ni ukweli au ni uzushi tu, lakini tujiulize jambo moja. Riz1 yupo wapi? Mbona hasikiki tena? Amebanwa na mfumo? Kwanini hatajwi tajwi tena mtaani na serikalini?

Jibu ni moja tu, Riz kwa sasa hana impact yoyote zaidi ya kubakia na ubunge wake, ubunge ambao hata akigombea leo, asiposaidiwa na system hawezi kushinda. Lakini haya yanasababishwa na nini! Ni kwasababu utawala uliomtambisha bwana Riz1 kwa sasa haupo na ukijaribu hata kukosoa wanaambiwa wana washwa washwa, wanyamaze. Kwanini wasinyamaze?

Kama hivyo ndivyo, kumbe hata hawa wanaojifanya miungu watu chini ya utawala wa Rais Magufuli, wakatembea kwa malingo, wakajaribu hata kutusi watu wengine ipo siku nao watanyamaza kimya. Ndio watanyamaza. Ni pale mzee wetu Magufuli atakapoenda kupumzika kwa kumaliza vipindi vyake viwili vya urais huko Tanzania.

Huo ndio ukweli. Muulizeni bwana Msiba, alikuwa anaenda kushinda kutwa nzima pale Maktaba ya Taifa ilipokuwa ofisi ya Rizone, akijisogeza kwa bwana mkubwa yule ili naye maisha yaende. Labda riz mwenyewe hawezi kuamini kwamba bwana msiba yule ndio huyu wa leo anaweza akaitisha press akasema lolote apendalo na asiguswe.

Hiyo ndio raha ya utawala ukiwa upande wako. Lakini yanaenda na kupoa. Huenda mwaka 2026 Tanzania ikazalisha Msiba mwingine au ndugu Makonda RC wa Dar es Salaam ambao kwa hakika licha ya kwamba ni mchapakazi haswa, lakini pia System imemkubali. Rejea skendo ya Makontena Bandarini angekuwa mwingine ingekuwaje.

Nipunguze porojo hapa, ila nashauri tu, nyie viongozi ambao Mungu amewabariki mpo karibu na utawala huu msilewe sifa. Tumieni fursa hii vizuri na muwashauri viongozi wetu wa juu haswa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ili waitumikie nchi yetu vizuri.

Mkijifanya nyie ni wajuaji sana, fikiria utawala huu ukienda mwishoni, mtaishi vipi mtaani. Najiuliza maswali, hivi bwana Msiba anavyotukana watu, anavyochafua watu ndani ya nchi yake ikatokea mmoja wapo anayechafuliwa anakuja kuwa kiongozi wa juu serikalini ataishije?

Tumuogopeni Mungu jamani! Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na utawala wa sheria. Sasa inakuwaje kuna wachache wanaweza kufanya wapendalo na wasiguswe?

Jamani, jamani.
 
Umesahau kumtaja Wasira, aliyekuwa mratibu wa juice ya Ikulu na wapinzani. Ila leo kuna tetei kazuiwa kuingia Ikulu kwa maagizo toka juu
 
Back
Top Bottom