Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,648
- 698,243
Uchumi unahujumiwa hapa
1. Bodaboda
Nchi zinakotoka zimeshapigwa marufuku kutokana na kuongezeka kwa walemavu, yatima na wajane huku nguvukazi ya taifa ikipungua na hata kutishia kizazi kijacho.
2. Kamari
Wawekezaji wa hii michezo ya kubahatisha na kamari nchini kwao ni marufuku na ni kosa la jinai lenye adhabu kali ukikutwa unacheza hii michezo, Taifa lao limetenga eneo maalum la visiwa mbali na wengine kwa wale wenye kupenda kuchezea pesa.. Sisi huku hatuna hiyo mipaka kwakuwa tu washika dau pamoja na chama chawala wanakula %.
3. Pombe kali za vichupa vya plastic mbadala wa viroba.
Wawekezaji ni mixer na wabongo lakini mashine zinatoka kulekule.
Picha likoje!
Kijana aliyefeli maisha kwa namna zote anapata pikipiki ya mkataba. Lakini kumbuka huyu ni kijana damu changa na limbukeni wa mengi na vingi.. Kwa bahati mbaya sana anaingia kwenye mtego wa kuhudumia familia, wazazi na wengine hata ndugu.. Lakini pia anahitaji matumizi binafsi
Picha linaendelea
Boda boda lake na hata kijiweni nyingi zimefungwa FM radio ambazo nyingi muda wote zinahamasisha michezo ya bahati na sibu na kamari kama njia ya kutoboa kimaisha kwa kujishindia mamilioni. Akifikiria ndoto zake, akifikiria majukumu yake anajikuta hana jinsi bali ajaribu bahati yake, prngine Mungu atamuona
Asichojua kamari ni biashara ya kitapeli isiyo na chembe ya huruma inayozingia faida yake tu. Anacheza michezo miwili mitatu na kuputwa mapato yote ya siku na pengine na hakiba.
Picha linafikia patamu sasa. Kwa stress za kuliwa na kukosa utajiri wa haraka, huku akiwa hana sent mfukoni anakopa kwa mshkaji 5000 aweke mafuta ya buku, anunue chochote cha buku 2 cha kurudi nacho home.. Kishapo! Buku 2 atoe lock kwa vipombe vikali maana hiyo ni sawa na bia moja ambayo haimfikishi popote!
Anakapiga kachupa chap bila kuzingatia kuwa kako dry kisha anaenda home kupumzika. Lakini huko njiani anaweza kukutana na mengi Kutokana na kilevi. Ajali ndogo ya kumlaza ndani siku mbili tatu
Ajali kubwa ya kupelekwa hospital akuwa majeruhi na kutumia siku kadhaa akiwa kitandani. Ajali kubwa zaidi ya kumsababishia majeraha makubwa na ulemavu na kubaji kuwa tegemezi badala ya tegemewa!
Ajali kubwa kabisa ya kumsababishia kifo Na kuacha yatima na wajane.
Serikali ya chama chawala inaruhusu baadhi ya biashara bila kutafakari madhara yake kwa kina ya sasa na ya baadae. Wanachoangalia na kujali ni kile kinachoingia mifukoni mwao. Huu ni uhujumi uchumi mkubwa sana kwa baraka za chama chawala.