Utatoa maamuzi gani?

Kuna jamaa alikuwa na kesi mahakamani,na wakili wake alimshauri kwamba ategemee fine au akishindwa
kulipa atapelekwa jela,na hukumu imebaki siku 2.
Jamaa alikuwa hana hela,akamkopa boss wake na boss akasema hana.
Alipo rudi nyumbani alimweleza mkewe na mkewe akasema atajaribu kutafuta.
Kesho yake mkewe alipata hela na fine ikalipwa.
Usiku wake jamaa hakupata usingizi,akachungulia simu ya mke wake.
Akaona sms inasema,nisipo kusaidia wewe mpenzi nitamsaidia nani?
Namba ni ya boss wake na yeye ni dereva.
Mke wake alikuwa hajui mumewe anamwendesha nani na boss inasemekana hajui kama ni mke wa dereva wake.
Kama wewe je uta muuliza mkewe au boss wako?
Au uta endelea kufanya kazi au utaacha?
Pagumu hapo.

Mbona jibu simpo tu!! Kwani cha kwanza ni nini?! kufadhiliwa ili asiende jela au mke wake kutoka nje ya ndoa?! Kama mke huyu angetoka nje ya ndoa kwa ajili tu ya kumuokoa yeye asiende jela, basi hapo pagumu kuamua kwavile mwanamke aliamua kujidhalilisha kwa ajili ya mumewe..... infact, ningemsamehe! Lakini kwa hii issue ni kwamba mwanamke alikuwa sio mwaminifu tangu hapo....hivyo, kama hukumu yangu kwa mke aliyeisaliti ndoa yangu ingekuwa ni taraka basi huyu ningempa na hivyo visenti vya hawala yake ningevichukulia kama faini tu ya umalaya wao!
 
lupango noma,unaweza ukaingia huko unaitwa mr ukatoka unaitwa aunty fulani...ningeuchuna kimya na miye ntafute kimada wangu
 
Back
Top Bottom