Ni namna gani ulivyoweza kukutana na mke, mpenzi au mwenzi wako? Njoo tupeane uzoefu

Lubebenamawe

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,947
2,185
Binafsi ni stori ndefu kidogo ila nitaifupisha. Mwaka 2004 baada ya kugraduate UDSM nilifanikiwa kuajiriwa katika shirika la umma na nikapangiwa mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini. Baada ya mwaka mmoja wa utumishi wangu niliweza kuwa maarufu kwa umahiri wa kazi.

Mwaka 2007 nilipandishwa daraja na kuhamishiwa Moro ambako nilienda kuwa mkuu wa idara. Wakati nilipoenda kuripoti uhamishoni nilimkuta boss wa shirika katika mkoa huo ni mwanamama. Pamoja na umri kuwa umeenda akiwa kwenye late 40s bado alikuwa ni kisu.

Niliporipoti alinikaribisha ofisi kwake na akanieleza habari za uhamisho wangu kuwa nimeletwa pale mahususi kwa ajili ya kuweka mambo sawa. Inavyoonyesha alikuwa taarifa zangu zote. Na pia alikuwa na imani na mimi. Aliniahidi kunipa ushirikiano na nisisite kupata ushauri kwake. Akanionya kuhusu baadhi ya watu pale kwenye shirika ambao huwategeshea wenzao misala.

Kadri siku zilivyoendelea niligundua huyu mama alikuwa mtu mwema sana na wafanyakazi asilimia kubwa walikuwa wanamkubali sana. Nilijitahidi kufanya kazi kwa weledi sana ili nisipoteze kuaminika kwangu. Boss mama alizidi kuniamini, na alinionyesha kunipenda, na alinipa kazi za nje nyingi sana ili nipate fedha nje na mshahara. Nilimheshimu kama mama yangu na nilizoea kumwita mama. Japo wengi walikuwa wakimwita mama D ikiwa ni jina la binti yake.

Siku moja nikiwa ofisini alinipigia simu na kuniambia niende ofisini kwake. Nilivyoingia nilishutka nilimkuta mdada mrembo sana kafanana na boss moja kwa moja nikahisi atakuwa D. Kwa wenge tu nikajikuta namsalimia tena boss wakati tulikuwa tumeshaonana.
Nikiwa nimesimama aliniambia nadhani ulikuwa hujawahi kumwona D huwa ndiye D mwenyewe ni mwanangu wa pili wa kwanza ni mkaka amehitimu chuo mwaka huu. Yeye D ndiyo kaanza first year mwaka huu.

Baada ya kuniambia hivyo hakunipa nafasi akamgeukia D, na kumwambia D huyu ni kaka yako anaitwa Lube tuko naye hapa sasa karibia mwaka. Baada ya utambulisha, nikakamua na kusema nafurahi kukufahamu naye akajibu my pleasure. Kisha nikamgeukea boss nikamwambia yaani umejitoa photocopy kabisa baba hukumwachia chochote. Naye akasema sasa ulitaka binti afanane na baba yake. Nikamwambia ila hongera. Soon tutagonga hodi kwako. Akasema heee na wewe kumbe una maneno? Nikamwambia niseme nini sasa? Nikamwaaga nikaenda kuendelea na kazi zangu.

Kuna siku D alikuja kwa mama yake bahati mbaya mama yake alikuwa na wageni ambao walikaa naye sana ofisini kwake akamwambia PS wake amlete D ofisini kwangu. Niliongea naye mambo mengi sana na nilikuwa makini nisije nikafanya jambo ambalo angelipeleka kwa mama yake lingenivunjia heshima.

Pamoja na kuongea naye mambo mengi sikuomba hata namba ya simu wala hata kumtongoza. Si mwongeaji ijapokuwa alikuwa na uwezo mzuri wa kujieleza na kufafanua mambo. Baada ya muda kama masaa mawili mama D akaja ofisini kwangu akatuuliza mmeshakula lakini nikisema bado twendeni. Tukaenda, ilikuwa ni siku nzuri sana kwangu, nilimwona D kuwa anafaa kuwa mke bora ila hofu yangu ikawa ni kwamba ninaweza mwambia akachomoa kisha yakafika kwa mama yake nikaharibikiwa. Nilifurahia kampani ya D na mama yake. Mwishoni nilimwambia mama kuwa umeifanya siku yangu kuwa nzuri nimetamani isingeisha. Akaniuliza mbona siku zote tunakula wote kanteen hujawahi sema hivyo au ni D ndiyo ameleta tofauti?. Mimi nikajibu lakini D hakuja mwenyewe. Akacheka akasema kuwa nilikuwa sijakujua vizuri.

Miezi kama mitatu mbele nikiwa nacheza football huwa desturi ya kucheza football jioni baada ya kazi. Siku moja niliumia goti langu la mguunwa kushoto lilihama, dislocated. Nilikimbizwa hospital moja ya mission hapo Moro, wakanishughulikia na kufanikiwa kuliweka sawa japo niliendelea kupata maumivu makali sana. Wakanilaza na kesho ya nikapigwa X ray. Sikuwa na shida zaidi ya dislocation na injury ya muscles ila ilibidi nilazwe siku tatu hapo hospital kwa ajili ya mazoezi.

Nikiwa hospitali asubuhi alipita Boss akaniletea supu ya kuku, jioni mida ya saa kumi alikuja D na rafiki yake nayo ni pisi kali ila haifiki kwa D. D alimwambia kuwa mimi ni kaka yake na pia akamtambulisha kwangu kuwa ni rafiki yake. Nilikaa nao kwa muda wa masaa mawili hadi walipofukuzwa na nesi sikutaka waondoke. Mpaka hapo sikuwa nimechukua namba za simu ya D. Nikawa nawaza kumlia timing yule rafiki yake. Kuna wakati nilimtuma D aende akaniletee air time (vocha) ajabu yule rafiki akasema lete nikamchukulie nikabaki na D. Mimi nilitaka D aende ili nichukue namba ya rafiki yake. Kisicho riziki hakiliki.

Kesho yake kawaida mama D akiwa anaenda ofisini alinipitishia supu wakiwa na mumewe, a very gentleman. Nilimwambia mama D mbona unahangaika wakati mim. naweza kula vyakula vya hapa hapa canteen. Jioni akaja D peke yake bila rafiki yake. Niliongea naye mengi sana na niliinjoy hata ulipofika muda wa kuondoka alimwomba nesi aendelee kuongea nami nesi alijua kuwa ni mwenzi wangu hakumzuia akamwaambia hata kulala unaweza lala. Siku hiyo aliondoka saa mbili usiku. Aliponiaga akanishika mkono wangu akawa anauminya kama ana anafanya massage. Siku hiyo nilimwomba namba ya simu akanipa.

Jioni nikamtext kipindi hata whatsapp haipo, nikamwambia I wish ningeendelea kuumwa ili uendelee kunijali, najisikia raha kuliko nilipokuwa mzima. Akajibu Ooo no please Lube pona mapema, nitaendelea kukujali hata ukiwa mzima. Chatting tulikuwa tunafanya kwa kingereza.

Kesho yake mama D akapita kama kawaida na mazagazaga kibao, nikamwambia kuwa mchana naweza ruhusiwa, akasema nitamjulisha.

Mchana nikaruhusiwa nikamjulisha mama D kuwa tayari nimesharuhusiwa akaniuliza umeshapata usafiri, nikamwambia nitachukua tax akaniambia subiri kama dk 20. Baada ya nusu akaingia D akanisaidia kufungusha vitu vyangu na kucheck out kwa kupitisha nyaraka za bima alipokamilisha akaniambia tayari tuondoke. Nilikuwa natembelea gongo moja ili nisiumize mguu ulioumia. Ilikuwa ni gari ya ofisini ilikuja kunichukua, Nissan Patrol, kwenye kupanda kwenye gari ilibidi kupata msaada ilibidi D anisaidie. Wakani akinisaidia nilifeel chuchu yake imegusa kwenye shavu langu. Kichwa cha chini kikatamalaki.

Tukaondoka tulipofika nyumbani akanisaidia kushuka kwenye gari kisha wakashusha vinavyonihusu. Alipotaka kuondoka nikamshika mkono na kumwambia niahidi kitu kimoja. Akauliza nini hicho. Nikamjibu tafadhali naomb unijali kama ulivyonijali nikiwa hospitalini. Akajibu usihofu kwa hilo tu nitakujali zaidi ya ulipokuwa hospitalini. Akanikisi shavuni kisha akaondoka.

Nyumbani walimtuma sister wangu kuja kunihudumia, D akawa anakuja kila siku jioni akitoka chuo anamsaida sister kupika kisha tunafanya mazoezi ya kutembea pamoja, kisha tunaachana anaenda kwao. Tukawa tuna chatt mara kwa mara wakati mwingine mpaka saa nane usiku. Mpaka hapo nikawa nimejiridhisha kuwa D ananipenda tena sana. Hata dada yangu aliniambia.

Baada ya wiki hali yangu ikatengemaa japo nilitahadharishwa niepuke mikikimikiki. Nikaanza kwe Sister akaondoka nikabaki mwenyewe. D akawa anakuja japo si siku zote, mara moja moja.

Kuna kipindi alikata kama siku tano bila kuja alikuwa kwenye mitihani na nilijua pia. Ila kwa kumchokoza nikamwandikia message kuwa natamani niuugue tena ili uweze kunijali kama mwanzo. Alipopata message akanipiga simu. Tuliongea kama nusu saa huku akisikitika kwamba hata yeye amenimiss sana.

Baada ya kumaliza mitihani jumamosi moja alikuja tukachill na kufurahi. Ndiyo siku hiyo alinikabidhi usichana wake. Tuliendelea na mahusiano kiasi kwamba mama yake akajua. Aliwahi kuniambia kitu kimoja tukiwa kazini kwamba najua uko kwenye mahusiano na D tafadhali usije ukavunja moyo binti yangu.

Baada ya muda nilimweleza mzee kuhusu kusudio la kuoa. Mzee wangu alikuwa ameshapewa ubuyu na sister.

Muda ulifika mimi na D tulitambulishana rasmi, kisha tukafunga ndoa takatifu. Tumeishi maisha ya raha sana. Tumebarikiwa watoto watatu na nne nilizaa na mkorea. Ilinitia doa sana ijapokuwa D alinisamehe.

Baada ya kufunga na D, niliomba kuhama mkoa kwa sababu sikuona vyema kufanya kazi ofisi moja na mama mkwe.
Hivi ndivyo nilikutana na mpenzi wangu wa maisha ,D asante mama D kwa kumlea D na kuwa mke bora kwangu na mama bora kwa watoto wangu.
 
Binafsi ni stori ndefu kidogo ila nitaifupisha. Mwaka 2004 baada ya kugraduate UDSM nilifanikiwa kuajiriwa katika shirika la umma na nikapangiwa mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini. Baada ya mwaka mmoja wa utumishi wangu niliweza kuwa maarufu kwa umahiri wa kazi.
Mwaka 2007 nilipandishwa daraja na kuhamishiwa Moro ambako nilienda kuwa mkuu wa idara. Wakati nilipoenda kuripoti uhamishoni nilimkuta boss wa shirika katika mkoa huo ni mwanamama. Pamoja na umri kuwa umeenda akiwa kwenye late 40s bado alikuwa ni kisu.
Niliporipoti alinikaribisha ofisi kwake na akanieleza habari za uhamisho wangu kuwa nimeletwa pale mahususi kwa ajili ya kuweka mambo sawa. Inavyoonyesha alikuwa taarifa zangu zote. Na pia alikuwa na imani na mimi. Aliniahidi kunipa ushirikiano na nisisite kupata ushauri kwake. Akanionya kuhusu baadhi ya watu pale kwenye shirika ambao huwategeshea wenzao misala.
Kadri siku zilivyoendelea niligundua huyu mama alikuwa mtu mwema sana na wafanyakazi asilimia kubwa walikuwa wanamkubali sana. Nilijitahidi kufanya kazi kwa weledi sana ili nisipoteze kuaminika kwangu. Boss mama alizidi kuniamini, na alinionyesha kunipenda, na alinipa kazi za nje nyingi sana ili nipate fedha nje na mshahara. Nilimheshimu kama mama yangu na nilizoea kumwita mama. Japo wengi walikuwa wakimwita mama D ikiwa ni jina la binti yake.
Siku moja nikiwa ofisini alinipigia simu na kuniambia niende ofisini kwake. Nilivyoingia nilishutka nilimkuta mdada mrembo sana kafanana na boss moja kwa moja nikahisi atakuwa D. Kwa wenge tu nikajikuta namsalimia tena boss wakati tulikuwa tumeshaonana.
Nikiwa nimesimama aliniambia nadhani ulikuwa hujawahi kumwona D huwa ndiye D mwenyewe ni mwanangu wa pili wa kwanza ni mkaka amehitimu chuo mwaka huu. Yeye D ndiyo kaanza first year mwaka huu. Baada ya kuniambia hivyo hakunipa nafasi akamgeukia D, na kumwambia D huyu ni kaka yako anaitwa Lube tuko naye hapa sasa karibia mwaka. Baada ya utambulisha, nikakamua na kusema nafurahi kukufahamu naye akajibu my pleasure. Kisha nikamgeukea boss nikamwambia yaani umejitoa photocopy kabisa baba hukumwachia chochote. Naye akasema sasa ulitaka binti afanane na baba yake. Nikamwambia ila hongera. Soon tutagonga hodi kwako. Akasema heee na wewe kumbe una maneno? Nikamwambia niseme nini sasa? Nikamwaaga nikaenda kuendelea na kazi zangu.
Kuna siku D alikuja kwa mama yake bahati mbaya mama yake alikuwa na wageni ambao walikaa naye sana ofisini kwake akamwambia PS wake amlete D ofisini kwangu. Niliongea naye mambo mengi sana na nilikuwa makini nisije nikafanya jambo ambalo angelipeleka kwa mama yake lingenivunjia heshima. Pamoja na kuongea naye mambo mengi sikuomba hata namba ya simu wala hata kumtongoza. Si mwongeaji ijapokuwa alikuwa na uwezo mzuri wa kujieleza na kufafanua mambo. Baada ya muda kama masaa mawili mama D akaja ofisini kwangu akatuuliza mmeshakula lakini nikisema bado twendeni. Tukaenda, ilikuwa ni siku nzuri sana kwangu, nilimwona D kuwa anafaa kuwa mke bora ila hofu yangu ikawa ni kwamba ninaweza mwambia akachomoa kisha yakafika kwa mama yake nikaharibikiwa. Nilifurahia kampani ya D na mama yake. Mwishoni nilimwambia mama kuwa umeifanya siku yangu kuwa nzuri nimetamani isingeisha. Akaniuliza mbona siku zote tunakula wote kanteen hujawahi sema hivyo au ni D ndiyo ameleta tofauti?. Mimi nikajibu lakini D hakuja mwenyewe. Akacheka akasema kuwa nilikuwa sijakujua vizuri.
Miezi kama mitatu mbele nikiwa nacheza football huwa desturi ya kucheza football jioni baada ya kazi. Siku moja niliumia goti langu la mguunwa kushoto lilihama, dislocated. Nilikimbizwa hospital moja ya mission hapo Moro, wakanishughulikia na kufanikiwa kuliweka sawa japo niliendelea kupata maumivu makali sana. Wakanilaza na kesho ya nikapigwa X ray. Sikuwa na shida zaidi ya dislocation na injury ya muscles ila ilibidi nilazwe siku tatu hapo hospital kwa ajili ya mazoezi.
Nikiwa hospitali asubuhi alipita Boss akaniletea supu ya kuku, jioni mida ya saa kumi alikuja D na rafiki yake nayo ni pisi kali ila haifiki kwa D. D alimwambia kuwa mimi ni kaka yake na pia akamtambulisha kwangu kuwa ni rafiki yake. Nilikaa nao kwa muda wa masaa mawili hadi walipofukuzwa na nesi sikutaka waondoke. Mpaka hapo sikuwa nimechukua namba za simu ya D. Nikawa nawaza kumlia timing yule rafiki yake. Kuna wakati nilimtuma D aende akaniletee air time (vocha) ajabu yule rafiki akasema lete nikamchukulie nikabaki na D. Mimi nilitaka D aende ili nichukue namba ya rafiki yake. Kisicho riziki hakiliki.
Kesho yake kawaida mama D akiwa anaenda ofisini alinipitishia supu wakiwa na mumewe, a very gentleman. Nilimwambia mama D mbona unahangaika wakati mim. naweza kula vyakula vya hapa hapa canteen. Jioni akaja D peke yake bila rafiki yake. Niliongea naye mengi sana na niliinjoy hata ulipofika muda wa kuondoka alimwomba nesi aendelee kuongea nami nesi alijua kuwa ni mwenzi wangu hakumzuia akamwaambia hata kulala unaweza lala. Siku hiyo aliondoka saa mbili usiku. Aliponiaga akanishika mkono wangu akawa anauminya kama ana anafanya massage. Siku hiyo nilimwomba namba ya simu akanipa.
Jioni nikamtext kipindi hata whatsapp haipo, nikamwambia I wish ningeendelea kuumwa ili uendelee kunijali, najisikia raha kuliko nilipokuwa mzima. Akajibu Ooo no please Lube pona mapema, nitaendelea kukujali hata ukiwa mzima. Chatting tulikuwa tunafanya kwa kingereza.
Kesho yake mama D akapita kama kawaida na mazagazaga kibao, nikamwambia kuwa mchana naweza ruhusiwa, akasema nitamjulisha.
Mchana nikaruhusiwa nikamjulisha mama D kuwa tayari nimesharuhusiwa akaniuliza umeshapata usafiri, nikamwambia nitachukua tax akaniambia subiri kama dk 20. Baada ya nusu akaingia D akanisaidia kufungusha vitu vyangu na kucheck out kwa kupitisha nyaraka za bima alipokamilisha akaniambia tayari tuondoke. Nilikuwa natembelea gongo moja ili nisiumize mguu ulioumia. Ilikuwa ni gari ya ofisini ilikuja kunichukua, Nissan Patrol, kwenye kupanda kwenye gari ilibidi kupata msaada ilibidi D anisaidie. Wakani akinisaidia nilifeel chuchu yake imegusa kwenye shavu langu. Kichwa cha chini kikatamalaki.

Tukaondoka tulipofika nyumbani akanisaidia kushuka kwenye gari kisha wakashusha vinavyonihusu. Alipotaka kuondoka nikamshika mkono na kumwambia niahidi kitu kimoja. Akauliza nini hicho. Nikamjibu tafadhali naomb unijali kama ulivyonijali nikiwa hospitalini. Akajibu usihofu kwa hilo tu nitakujali zaidi ya ulipokuwa hospitalini. Akanikisi shavuni kisha akaondoka.
Nyumbani walimtuma sister wangu kuja kunihudumia, D akawa anakuja kila siku jioni akitoka chuo anamsaida sister kupika kisha tunafanya mazoezi ya kutembea pamoja, kisha tunaachana anaenda kwao. Tukawa tuna chatt mara kwa mara wakati mwingine mpaka saa nane usiku. Mpaka hapo nikawa nimejiridhisha kuwa D ananipenda tena sana. Hata dada yangu aliniambia.
Baada ya wiki hali yangu ikatengemaa japo nilitahadharishwa niepuke mikikimikiki. Nikaanza kwe Sister akaondoka nikabaki mwenyewe. D akawa anakuja japo si siku zote, mara moja moja.
Kuna kipindi alikata kama siku tano bila kuja alikuwa kwenye mitihani na nilijua pia. Ila kwa kumchokoza nikamwandikia message kuwa natamani niuugue tena ili uweze kunijali kama mwanzo. Alipopata message akanipiga simu. Tuliongea kama nusu saa huku akisikitika kwamba hata yeye amenimiss sana.
Baada ya kumaliza mitihani jumamosi moja alikuja tukachill na kufurahi. Ndiyo siku hiyo alinikabidhi usichana wake.
Tuliendelea na mahusiano kiasi kwamba mama yake akajua. Aliwahi kuniambia kitu kimoja tukiwa kazini kwamba najua uko kwenye mahusiano na D tafadhali usije ukavunja moyo binti yangu.

Baada ya muda nilimweleza mzee kuhusu kusudio la kuoa. Mzee wangu alikuwa ameshapewa ubuyu na sister.

Muda ulifika mimi na D tulitambulishana rasmi, kisha tukafunga ndoa takatifu. Tumeishi maisha ya raha sana. Tumebarikiwa watoto watatu na nne nilizaa na mkorea. Ilinitia doa sana ijapokuwa D alinisamehe.
Baada ya kufunga na D, niliomba kuhama mkoa kwa sababu sikuona vyema kufanya kazi ofisi moja na mama mkwe.
Hivi ndivyo nilikutana na mpenzi wangu wa maisha ,D asante mama D kwa kumlea D na kuwa mke bora kwangu na mama bora kwa watoto wangu.

Asante kwa kuwa mume bora kwa mwanangu Lubebenamawe
Naendelea kuwaombea maisha marefu yenye amani na furaha tele. Mkawaone hadi wajukuu wa wajukuu zenu

Fene ndie mie huyo mama wa D na mamamkwe wa Lube
 
Similar Discussions

37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom