Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Mmoja wa majeruhi katika shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam juzi, Rubani Francis Shumila amefariki dunia jana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi), alikokuwa akitibiwa.
Wakati hilo likitokea, mama mzazi wa Christine Alfred, binti anayedaiwa kuwa chanzo cha shambulizi hilo, Hellen Alfred amekana kutambua uchumba baina ya marehemu Gabriel Munisi na mtoto wake huku kaka wa marehemu huyo akieleza kwamba alitambulishwa na mdogo wake, kwa binti huyo kwamba ni mchumba wake.
Katika shambulizi hilo, Munisi anadaiwa kuwashambulia marehemu Shumila, Hellen, Christine na mdogo wake Alpha ambaye alifariki dunia papo hapo katika shambulizi hili linaloelezwa kuwa lilitokana na wivu wa mapenzi. Baada ya shambulizi hilo, Munisi naye alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Patrick Mvungi alisema jana kwamba Shumila alifariki dunia saa 12.40 asubuhi akiwa katika Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).
Hellen amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na hali yake inaendelea vizuri na Christine aliruhusiwa kutoka hospitali juzi hiyo hiyo.
Taarifa ya daktari
Mvungi alisema kuwa taarifa za awali za daktari zinaonyesha kwamba Shumila alipoteza damu nyingi kutokana na majeraha ya kupigwa risasi tatu.
Alisema alipigwa risasi kichwani, mkononi na tumboni.
Ndugu zake Shumila ambao walibainika wanatoka Kenya waligoma kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo.
Ofisa wa Ubalozi wa Kenya nchini alisema jana kwamba wamesikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari lakini akasema ni mapema kulizungumzia.
Utata wa uhusiano
Ofisa Uhusiano wa MNH, Jacqueline Msuya alisema kuwa amezungumza na mama yake Christine ambaye alimweleza kwamba anatambua kwamba Shumila na mwanaye anayesoma huko Cyprus walikuwa wachumba na kusema kwamba binti yake huyo aliwahi kumwambia kwamba Munisi alikuwa rafiki yake wa kawaida tu.