Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,798
- 12,240
Nimesikitishwa na kauli ya waziri wa fedha Dr. Mgimwa kuwa ataunda tume itakayojumuisha TRA na wizara yake kujadili namna ya kuondoa kodi mbili wanazotozwa wafanyabiashara za Zanzibar!
HEY SERIKALI YA CCM ONDOENI AIBU HII YA KERO HARAKA!
- Hivi kweli serikali ya CCM imeshindwa kushughulikia kero hii ya muungano kwa miaka yote hii ikiwa madarakani?
- Ni sheria ipi imekuwa ikiwakwaza mawaziri wote na viongozi wa TRA waliopita kuondoa kero hii?
- Ni ugumu gani ulioifanya serikali ya muungano kutowasilisha marekebisho ya sheria hiyo ya wizi kama ipo?
- Hivi si kweli tumekuwa na mawaziri wa fedha wasiowajibika au wasiojua kazi yao kwa kipindi chote cha muungano?
HEY SERIKALI YA CCM ONDOENI AIBU HII YA KERO HARAKA!