Utata wa neno asilimia

Utata wa neno asilimia

Somo la comprehension lirudi shuleni wazee...

Sentensi haina shida mzee baba.... ni sawa na kusema 70% ya wanaJF wanachat PM kila siku.

80% ya wanaochati PM kuhusu mapenzi wanakutana na kuonana..
Mfano wako hauendani mkuu...
 
Mie kilaza naona nipo tofauti na naomba nielimishwe.
Nilitegemea percent ndogo ndogo zifanye total ya mia ukiachia ile 70 percent ambayo tuna asume km 100 percent ya maji yote.
Waoooo, hata mie nilielewa hivo mwazo, na kwa mujibu wa mtililiko wa kiswahili chake nilielewa hivo;

Ila wadau wamekuja na hii kwamba...
○Ile namba ya kwanza ni pasentage ya maji mwili mzima,
○zile namba zinazofuata, kila moja ni pasentage ya maji inayotokana na mgawanyo wa "matilio" za kiungo husika
 
Hodi hapa kwa leo, make nina siku mbili tatu...bila kuingia humu;

Salaam kwenu.
Nimekuja hapa naomba ufafanuzi kutoka kwenu wajuvi wa hesabu.

Nimekutana na ubishi mahala mtu aliyejitanabaisha kama Dk.... akibishana na mwenzake kujusu sentesi ambayo mwenzake alisema haina mashiko, je hii sentesi ya Dokta iko sawa kwa mujibu wa mgawanyo wa asilimia?

"Maji huchukua karibu 70% ya mwili wa binadamu, ambapo seli za ubongo zina karibu 85% ya maji, misuli huwa na 75% ya maji, mifupa huwa na 25% ya maji na damu huwa na karibu na 82% ya maji"

Ngoja niendelee kukuchanganya kama sio kuku-confuse kabisa, hiyo 85% ya maji kwenye seli za ubongo inaweza kua ni asilimia 1 tu ya maji yote mwilini. Nahisi nimeeleweka vema.
 
Baada ya wadau kutoa ufafanuzi hivo hivo ulivosema niliwaelewa, ila kiswahili cha ye Dr. Sikukielewa kabisa mkuu!
 
Hodi hapa kwa leo, make nina siku mbili tatu...bila kuingia humu;

Salaam kwenu.
Nimekuja hapa naomba ufafanuzi kutoka kwenu wajuvi wa hesabu.

Nimekutana na ubishi mahala mtu aliyejitanabaisha kama Dk.... akibishana na mwenzake kujusu sentesi ambayo mwenzake alisema haina mashiko, je hii sentesi ya Dokta iko sawa kwa mujibu wa mgawanyo wa asilimia?

"Maji huchukua karibu 70% ya mwili wa binadamu, ambapo seli za ubongo zina karibu 85% ya maji, misuli huwa na 75% ya maji, mifupa huwa na 25% ya maji na damu huwa na karibu na 82% ya maji"
Kama nimekuelewa vizuri basi ni hivi 70% ya mwili wa binadamu ni maji

Kwa maana ya kwamba katika mwili wote wa binadamu (organs) zote mifupa na kila kitu 70/100 ni maji ya vitu vyote hivyo (70/100 ya mwili wa binadamu unaundwa na maji )

Sell za ubongo Zina 85% ya maji

Maana yake ni hii tukichukua selli za ubongo (kuzitizama zenyewe ) zimeundwa kwa alimia 85 kuwa ni maji au 85/100 ya selli Hizo no maji

Mifupa 25% ni maji maana yake ni hii

Tukichukua mifupa yote ya binadamu tukiangalia kwa jinzi ilivyoundwa asilimia 25 ni maji au pia anaweza kusema 25/100 ya mifupa ni maji

Damu kwa 82% ni maji

Anamaanisha kwamba ukichukua damu ya binadamu 82 asilimia ya kinachounda damu ni maji Hizo asilimia zilizo baki ndo zinaunda vitu vingine Kama seli, rangi na Mambo mengine
 
Hata 101% yupo sahihi. Ukiombwa na mtu mkopo wa sh 2m nawe ukampa 3m hapo umempa asilimia mia tatu-
300% ya alichoomba. Asili ni msingi ie base.
Yupo sahihi anaongelea kitu kizima mwili wa binadamu! Halafu anaongelea sub set za mwili na asilimia zake za damu! Yupo sahihi kimahesabu. Siyo vilaza kama ambao wanasema asilimia 101
 
Kama nimekuelewa vizuri basi ni hivi 70% ya mwili wa binadamu ni maji

Kwa maana ya kwamba katika mwili wote wa binadamu (organs) zote mifupa na kila kitu 70/100 ni maji ya vitu vyote hivyo (70/100 ya mwili wa binadamu unaundwa na maji )

Sell za ubongo Zina 85% ya maji

Maana yake ni hii tukichukua selli za ubongo (kuzitizama zenyewe ) zimeundwa kwa alimia 85 kuwa ni maji au 85/100 ya selli Hizo no maji

Mifupa 25% ni maji maana yake ni hii

Tukichukua mifupa yote ya binadamu tukiangalia kwa jinzi ilivyoundwa asilimia 25 ni maji au pia anaweza kusema 25/100 ya mifupa ni maji

Damu kwa 82% ni maji

Anamaanisha kwamba ukichukua damu ya binadamu 82 asilimia ya kinachounda damu ni maji Hizo asilimia zilizo baki ndo zinaunda vitu vingine Kama seli, rangi na Mambo mengine
Yess, collect!
Hicho ndicho alichomasnisha mtaalamu eti!
 
Hodi hapa kwa leo, make nina siku mbili tatu...bila kuingia humu;

Salaam kwenu.
Nimekuja hapa naomba ufafanuzi kutoka kwenu wajuvi wa hesabu.

Nimekutana na ubishi mahala mtu aliyejitanabaisha kama Dk.... akibishana na mwenzake kujusu sentesi ambayo mwenzake alisema haina mashiko, je hii sentesi ya Dokta iko sawa kwa mujibu wa mgawanyo wa asilimia?

"Maji huchukua karibu 70% ya mwili wa binadamu, ambapo seli za ubongo zina karibu 85% ya maji, misuli huwa na 75% ya maji, mifupa huwa na 25% ya maji na damu huwa na karibu na 82% ya maji"
Hayuko sahihi.
85%+82%+75%+25%=267%
Hapo kwenye misuli ba mifupa tu pekee kuna 100%
 
Hata 101% yupo sahihi. Ukiombwa na mtu mkopo wa sh 2m nawe ukampa 3m hapo umempa asilimia mia tatu-
300% ya alichoomba. Asili ni msingi ie base.
Usiwe kilaza, ukiona asilimia inazidi 100 ujue base yako ilikuwa kanyabwoya. Nisawa na kusema wasichana nyumbani kwangu ni 7 wakati kwangu kuna watu 6. Asilimia inaweza kuwa probability ambapo 0 asilimia ni kuwa kitu hakitatokea na 100 asilimia ni kitu lazima kitokee. Mfano katika uchaguzi ujao kupata rais wa tanzania ni asilimia 100 (maana hata asipokuwa JPM atapatikana Tundu Lissu etc) Lakini ni kosa kusema katika uchaguzi ujao JPM ana asilimia 100 kuwa Rais. Kama ni hivyo hakuna haja ya kufanya uchaguzi. Lakini mimi katika uchaguzi kuwa rais nina asilimia 0 kwa vile sitagombea. Hapo 101 imetoka wapi? Kwenye kucalculate asilimia kuna numerator na denominator ambapo numerator lazima iwe subset ya denominator bwashee. Kesho tuongelee conditional probability
 
Ukijumlisha zile namba za asilimia zilizogawanywa, mbali na ile namba ya kwanza ya jumla namba inakuwa kubwa zaidi ya mia;

hapo neno asilimia halipotezi maana kwa kuwa badala ya mia imekuwa 100+?
...kila kiungo kilichotajwa hapo kimepimwa kwa asilimia 100 ya maji yaliyomo kwenye kiungo hicho na sio kwa asilimia za maji yaliyomo kwenye mwili mzima! Simple...
 
Hata 101% yupo sahihi. Ukiombwa na mtu mkopo wa sh 2m nawe ukampa 3m hapo umempa asilimia mia tatu-
300% ya alichoomba. Asili ni msingi ie base.

Hesabu zako za msingi zina makosa.

3m is 150% of 2m, not 300%.

300% ya 2m ni 6m.

300% ya y ni y X 3.

300% ya 2m ni 2m X 3, ni 6m.
 
Nimekurupuka kusoma nikajua asilimia za bodi ya mikopo HESLB.

Ok kikubwa kunywa maji mengi viungo visipunjane mma.
 
Ama umesahau hesabu, hujui, mbishi, au kupitiwa. Msingi wetu unalinganishwa na 100, kwa hiyo kama ulikuwa unalipwa sh 1m ukaongezwa na kuwa 2m, umepanda kwa 100%. Lakini kama ungeongezwa kutoka 1m mpaka 3m utakuwa umepanda kwa 200% .

Back
Top Bottom