Utata wa kuhamia Dodoma unahatarisha kibarua cha waziri mkuu?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
11,114
39,130
Hofu imeanza kutanda miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali kuhusu hatma ya nafasi ya PM kuhusiana na kusuasua kwa suala la kuhamia Dodoma jambo ambalo Mheshimiwa Rais alilitangaza kwa msisitizo mkubwa sana.

Hofu hiyo inatokana na mambo haya hasa.
1/Mpaka sasa PM ofisi yake na makazi yake yapo Dar, japokuwa alishamuaga Mheshimiwa rais Ikulu kuwa anahamia Dodoma zaidi ya Miezi mitatu iliyopita.

2/Kushindwa kwa PM kuwashinikiza kwa nguvu mawaziri na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kuhakikisha wawe wamehamia Dodoma.

3/Gharama kubwa zinazotumiwa na baadhi ya maafisa wa serikali kwenda Dodoma na kisha kurudi tena Dar ili kuendelea na kazi.

4/Mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya Umma uliyopo Dar ambayo amehamia Dodoma huku akiyaacha majengo yake waliokuwa wanayatumia Dar yarudi kwenye mamlaka zingine za Kiserikali au yapigwe mnada kama Agizo la mheshimiwa rais anavyotaka.
 
Mlete mada kweli hata movie za kina Kanumba hazijamsaidia! Ina maana katika drama mtu akimwaga boss/baba wake "naenda dodoma" ndo husafiri kweli dodoma?
Hayo yalikuwa maigizo mkuu yasikupe tabu ila muda ukifika pm atakuwa hapo kilimani.
 
Aanze mkubwa(mkulu) kwanza, alafu awaambie asiyekuja dodoma hapati mshahara
 
Kuna kipindi niliona pale ikulu ya chamwino kulikuwa na ujenzi wa mwendokasi wa wachina, sijui walishamaliza?
Kama hawajamaliza labda ndo kinachomkwaza mkulu
 
PM yuko vizuri tu, hawezi kutumbuliwa. Kumtumbua PM si rahisi kama kumtumba mkurugenzi, mkuu wa wilaya, mkoa, au waziri mwingine. Halafu serikali haiwezi kuhamia Dodoma kwa miguu, daladala au bajaj.
 
Hofu imeanza kutanda miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali kuhusu hatma ya nafasi ya PM kuhusiana na kusuasua kwa suala la kuhamia Dodoma jambo ambalo Mheshimiwa Rais alilitangaza kwa msisitizo mkubwa sana.

Hofu hiyo inatokana na mambo haya hasa.
1/Mpaka sasa PM ofisi yake na makazi yake yapo Dar, japokuwa alishamuaga Mheshimiwa rais Ikulu kuwa anahamia Dodoma zaidi ya Miezi mitatu iliyopita.

2/Kushindwa kwa PM kuwashinikiza kwa nguvu mawaziri na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kuhakikisha wawe wamehamia Dodoma.

3/Gharama kubwa zinazotumiwa na baadhi ya maafisa wa serikali kwenda Dodoma na kisha kurudi tena Dar ili kuendelea na kazi.

4/Mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya Umma uliyopo Dar ambayo amehamia Dodoma huku akiyaacha majengo yake waliokuwa wanayatumia Dar yarudi kwenye mamlaka zingine za Kiserikali au yapigwe mnada kama Agizo la mheshimiwa rais anavyotaka.
Wewe inaelekea uko Mahenge! Kuhamia Dodoma ni reality. Watu wameshafunga mizigo na awamu ya kwanza mwezi huu January. Serikali hii ni makini na haina longolongo!!
 
Back
Top Bottom