Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Sababu za Dr Prof Shaba kuwa mlevi wa kutupwa baada ya postmotem.
Huyu Prof Shaba inasemekana hakua mlevi ila baada ya tukio hili alikua kama TBL
Muachage uzushi jamani. Prof Shaba alikuwa mlevi wa kutupwa tangu akisoma PhD kule UK mwaka 1965.
 
Wewe pia umesimuliwa. Kama ni kweli ulikuwa chuo mwaka huo ungekumbuka kuwa hakukuwa na waziri aliyeitwa Barongo. Edward Barongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na ni miongoni mwa waliokamatwa katika sakata la uhujumu uchumi, akawekwa mahabusu na kushitakiwa. Sokoine alipofariki Barongo alikuwa anasota mahabusu. Jamaa za Barongo na watu wengine waliokuwa kwenye list ya uhujumu walishangilia sana waliposikia Sokoine kafa.

Sokoine pamoja na Nia yake njema alikuwa na Mikurupuko Kama Kaka yake Ndugai
 
Soma vizuri nilicho kiandika, hakuna alie niambia bali nimejua kupitia maandiko kadhaa ambayo bado yanaacha maswali hayo niliyo yaweka hapo juu...
swali namba 7 ni upuuzi.swali namba 6 unatutania yani mpaka leo kweli hujui hata alipata ajali wapi kuwa serious
kidogo
 
Yesu Kristo aliuwawa.
Mtume Mohamad pia aliwindwa ili auwawe lakini utando wa BUBUI ulimponya.
Mitume wengi tu waliuwawa.
Waliosababisha au waliowaua hawakumbukwi kwamwe.
Katika maisha, cha maana ni kwamba Umewafanyia nini wanadamu, wanyama hata vitu vilivyo hai na visiyo hai ili maradi tu kwa kufanya hivyo uliifanya Dunia iwe pahala bora zaidi pa kuishi.
Baada ya kufanya haya, japokuwa utakuwa umekufa lakini utakuwa u hai.
Kwa hiyo Sokoine, Nyerere na wengine waliokufa wakipigania watu,japo kuwa wamekufa lakini wako hai.
Inawezekana mimi na wewe japokuwa tunaishi na hakuna mtu ana mpango wa kutuua lakini tayari tumekufa kwa sababu hatuna chochote tunacholifanyia Taifa ili watu wake waweze kuishi vizuri zaidi.
 
Inawezekana mabepari walitekeleza mauaji yake kwa sababu hawakupenda siasa ya UJAMAA iliyokuwa inafanywa na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere na walijua wazi kwamba alikua anamuandaa Sokoine kuongoza nchi kwa misingi ya Ujamaa waliyokua wanaipiga vita
 
Waulize Dr Kashimba alie na Siri aina ya majeraha ambayo hata Familia ilikataliwa kuona, pia Muulize Mzee Kizota yule mwenye Bar viwanja vya Saba Saba, alikuwa bodi gadi yake, wakimbizi waliokuwepo maeneo ya karibu na ajali wanadai kuona bodi gadi huyo akifyatua risasi, muda mfupi tu baada ya mheshimiwa kutoka nje ta gari kujaribu kukimbia. Muulize Mwalimu Nyerere aliekuwa Rahisi wa Tanzania
Duh
 
Nakumbuka kwenye hotuba moja Mwl Jk Nyerer alisikika akisema nanukuu "" ukiwambia wananchi Sokoine amekufa kwa ajali watu wanakataa kabisaa..wanaktaa kabisa, lakini tunasema alifariki kwa ajali". Ukwl hata mwlm anajua sokoine alikufaa kifo chenye utata sana, angefnyaje sasa na wakati aliowaamini sana ndio lipoti y usalama ilionyesha waliratbu zoezi kwa kushirikina na wazungu, mzee wangu anasema kifo kile ni kama kilimpiga rungu la magoti Mwl na kumunyon'gonyeza kabisa akaamini kwl sasa anahujumiwa kila sekta maana sokoine wote walijua angekuwa raisi, na moto ungewaka kama angekuwa raisi, Mzee Kizota anaujua ukwl wa kifo cha sokoine, lakini ripoti halali ya postmortem inaonyesha alikuwa na risasi mwilini mwake, japo iliyosomwa kwa wananchi haikuwa hiyo. Sema credit kubwa na wapa usalama wa taifa namna walivo i cover issue ile sio hawa tunaokutana nao bar wanasema mimi usalama wa taifa bwana..........
 
utat kifo cha Sokoinne

marafki wa mimi leo ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati Sokoine kwa vile alipofariki nilikua bado sijazaliwa, nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali na habari za hapa na pale. naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo, napenda kushare na nyie maswali kadhaa ambayo yantekenya ubongo wangu

Ajali iliyosababisha kifo cha Sokoine ilikuwa ya aina gani? Kupinduka kwa gari, kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

. Katika hiyo ajali hayati Sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

Kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

Kama wako hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

.

Kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu..
kma ku na mwenye majibu atujuze
 
uchunguzi uanze upya kwa hisani ya watengenezaji wa benz, ndicho unachotaka kusema ama nini, mie ngoja nilikuwa nimeshazaliwa ila maji nilikuwa naita mma. ngoja na mimi leo nisome historia
 
*UNDANI KIFO CHA SOKOINE*

WAZIRI Mkuu (sasa ni marehemu) Edward Moringe Sokoine alikuwa Dodoma kwenye kikao cha Bunge akiwa ni kiongozi wa shughuli za serikali na alimaliza kikao chake Aprili 11, 1984.

Aliandaliwa usafiri wa ndege ili asafiri na ujumbe wake wakati wa kurejea Dar es Salaam kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa lakini alikataa.

“Safari hii sitaki kurudi Dar es Salaam kwa ndege, nataka kurudi kwa gari ili nione hali ya mazao ya wakulima njiani,” alikaririwa afisa mmoja wa Ikulu akimkariri Waziri Mkuu Sokoine mara baada ya kujulishwa habari ya usafiri wa kumrejesha Dar.

Aprili 12, 1984 msafara wake ulianza akitokea Dodoma huku ukisindikizwa na magari ya polisi na wana usalama wa taifa.

Msafara wake mchana ulipofika eneo la Wami mkoani Morogoro, jirani na palipojengwa makao makuu ya sasa ya Wilaya ya Mvomero, gari yake ilipata ajali kwa kugongwa na gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser.

Sokoine alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari walithibitisha kifo chake.
Rais (wa wakati huo), Mwalimu Julius Kambarage Nyerere siku hiyo majira ya jioni alilitangazia taifa kifo cha waziri mkuu wao. Mwalimu Nyerere, alishindwa kuhutubia kutokana na majonzi aliyokuwa nayo.

Miaka kumi baada ya kifo chache, daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sokoine baada ya kifo, aliweka wazi taarifa ya chanzo cha kifo chake.

Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya ajali, Sokoine alivunjika shingo ambayo ilisababisha kubana mishipa ya fahamu (spinal cord) ambayo ilikata mawasiliano kati ya ubongo na sehemu nyingine za mwili.

Kabla ya kifo chake, Sokoine alikuwa pia Mbunge wa Jimbo la Monduli na mwili wake ulizikwa huko kwa heshima zote za kiserikali, japokuwa mila za Kimasai pia zilipewa nafasi katika mazishi hayo.

Mahali alipopatia ajali Sokoine mara baada ya ajali hiyo panaitwa Wami Sokoine na pamejengwa mnara wa kumbukumbu ya kifo chake.

Maadhimisho ya miaka 34 ya kifo cha Hayati Edward Sokoine yanatarajia kufanyika April 12 Moringe Juu, Arusha. Kutakuwa na ibada maalum pamoja na fursa ya kutembelea kaburi la Sokoine. Tuungane kwa pamoja. Karibuni sana.
IMG-20180411-WA0001.jpg
IMG-20180411-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom