mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,610
- 1,602
Asante mdau, ila kwanini unasema mwanamke wa kisabato ni msumbufu?Wasabato wasumbufu sana, usijelogwa kutaka kuoa mwanamke msabato..
Ishu ni ushauri ndugu, kumbuka yule ni mchumba na inawezekana anampenda sana.Huyo mwanaume mwambie aache utoto yani na misuluali yake mikubwa mikubwa anashindwa kufanya uamuzi wa kiume...?
Asante mdau, ila kwanini unasema mwanamke wa kisabato ni msumbufu?
Naomba uzoefu wako katika hili jambo ndugu
Unajua ishu ni kwamba nahitaji kujua usumbufu wa wasabato ili nipate picha kamili?Wasabato ...mmh..! Fanya maamuzi ya kiume kwisha kazi kama vipi muache huyo demu ila wasabato niwasumbufu
Busara ni msichana kumfuata mvulana, ikishindikana kijana aachane naye maana maisha yanayoanza na vijikwazo kama hivyo mbele itakuja shida kubwaIshu ni ushauri ndugu, kumbuka yule ni mchumba na inawezekana anampenda sana.
Una mshauri achukue maamuzi gani?
Asante sana kwa ushauri wako, ngoja tusubiri wadau wengine kwa ushauri zaidiBusara ni msichana kumfuata mvulana, ikishindikana kijana aachane naye maana maisha yanayoanza na vijikwazo kama hivyo mbele itakuja shida kubwa
Asante kwa ushauri, tusubiri wadau wengine kwa ushauri mwingine piaKwa kuwa wote ni waumini wa biblia takatifu nawaambia kabisa hapo hakuna uchumba wala nini. Wameongozwa na matamaa yao ya kimwili sasa wanajua wazi kuwa hakuna popote watapata suluhisho. Si mchungaji wa KKKT au Sabato ataifunga hiyo ndoa.
Kwa kuwa wote wanaiamini biblia takatifu wasome 2 Kor. 6 : 14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa.....
Kati yao ni nani anaamini sawa sawa na mwenzake?? Hakuna. Basi hawatafanikiwa bali wanapotezeana muda.
Wazo la kimwili; Kijana ajitahidi amtotoe huyo binti. Atalainika tu
Asante mdau, unaweza weka hicho kifungo cha kwenye biblia ili iwe reference nzuri zaidiImeandikwa
Mwanamume atamwacha baba na mama yake ataambatana na mkewe
Ugumu uko wapi mwambie afuate ushauri wa Mungu huo[emoji115]tena bora wote wa mwelekeo mmoja majumba tofauti tuu
Una maana gani mdau?Msabato hawezi kuhamia kkt maana kkt huhesabiwa kama wa-mataifa tu
Mwanzo 2:24Asante mdau, unaweza weka hicho kifungo cha kwenye biblia ili iwe reference nzuri zaidi
Asante, nitakipitia hiki kifunguMwanzo 2:24
Leo ni mara ya kwanza kuingia kwenye hili jukwaa wadau, nategemea ushauri wa maana juu ya hili jambo.
Iko hivi kuna kijana wangu anaomba ushauri kuhusu tatizo linalomsumbua yeye ni mkristo wa dhehebu la KKKT na ana mchumba wake ni msabato, sasa mda unazidi kwenda kijana anataka kufunga ndoa.
Kijana akatoa wazo kwa binti kwamba ndoa inatakiwa ifungwe kanisani KKKT na baada ya ndoa binti ataendelea na dhehebu la kisabato.
Sasa binti amegoma kabisa, binti nae kasema hawezi kufunga ndoa KKKT anataka ndoa ifungwe kanisani sabato na baada ya ndoa kamruhusu kijana aendelee na dhehebu la KKKT.
Sasa ubishano upo kwenye wapi ndoa ifungwe kati ya Kanisani KKKT au sabato, na imefika hatua kwamba endapo mmoja atakataa kukubali mawazo ya mwenzie wanasema bora mahusiano yaishe.
Sasa wadau mnaushauri gani ili kuweza kuwanusuru huyu kijana pamoja na huyo mchumba wake.
Nimewashauri kuhusu ndoa ya kiserikali, ila wote hawako tayari kwa ndoa ya kufungwa serikalini.
Je mnamshauri nini huyu kijana na mchumba wake ili waweze kufanikisha mipango yao ya kufunga ndoa pamoja?
Asante kwa ushauri nduguKwa kukushauri tu, mwambie atafute mtu wa KKKT au dhehebu lolote la Kikristo, Ndoa na Msabato ni pasua kichwa, Msabato hachangamani na Mkristo yoyote, nimeshuhudia mateso makubwa ya ndoa a Msabato na Mkristo (Catholic, KKKT, Mlokole) Kuoa ni mara moja tu na ukikosea ni kila kitu