Utata wa chuo kipi bora umalizike hivi

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,809
Yaani kama una hasira unaweza pigana na watu kabisa!

Utakuta mtu amekaza hadi shingo kwamba CUHAS ndo chuo bora, mwenzake wa upande wa pili naye amekomaa MUHAS ndo chuo bora, huku kwa wenzangu nako ugomvi ule ule, wa SUA anasema pale ndo kuna msuli, UDSM ndo wanavaa vitambulisho hadi bar kuonesha ndo superior, MZUMBE nao wanakuja juu kwamba wao ndo bora yaani kiujumla ni fujo.

Sasa kumaliza huu utata mamlaka inayohusika anzisheni mitihan ya kitaifa ya vyuo vikuu alafu matokeo yapangwe kama Sekondari yaani wanafunzi 10 bora, vyuo vikuu 10 bora pia wanafunz wabovu 10, vyuo vikuu vibovu 10 nadhani hapo tutamaliza atleast hii ligi.

Maana mmezidi sasa, hadi walimu wakaifundisha shuleni siku anawainspire watoto waende kwenye chuo chake, wengine JORDAN UNIVERSITY, wengine TECU.. watoto wakija nyumbani utashangaa wanaanza kukuuliza kuhusu vyuo,

HII LIGI IFIKE MWISHO.
 
Mkipanga ubora kwa matokeo ya mitihani tu vyuo vyote vitabaki kuwa na ubora wa kidhana.

Tuonyesheni matunda ya kazi za wahitimu katika maisha ya Mtanzania ya kila siku.

Wahitimu wa chuo gani wamegundua nini na kuanzisha nini kipya ambacho hakikuwepo?

Mitihani kuna watu wanapiga mpaka profesa inabidi akope maksi za kuongezea, lakini kwenye application hawana kitu.
 
Sahh mkuu
 
Yaani kama una hasira unaweza pigana na watu kabisa!

Utakuta mtu amekaza hadi shingo kwamba CUHAS ndo chuo bora, mwenzake wa upande wa pili naye amekomaa MUHAS ndo chuo bora, huku kwa wenzangu nako ugomvi ule ule, wa SUA anasema pale ndo kuna msuli, UDSM ndo wanavaa vitambulisho hadi bar kuonesha ndo superior, MZUMBE nao wanakuja juu kwamba wao ndo bora yaani kiujumla ni fujo.

Sasa kumaliza huu utata mamlaka inayohusika anzisheni mitihan ya kitaifa ya vyuo vikuu alafu matokeo yapangwe kama Sekondari yaani wanafunzi 10 bora, vyuo vikuu 10 bora pia wanafunz wabovu 10, vyuo vikuu vibovu 10 nadhani hapo tutamaliza atleast hii ligi.

Maana mmezidi sasa, hadi walimu wakaifundisha shuleni siku anawainspire watoto waende kwenye chuo chake, wengine JORDAN UNIVERSITY, wengine TECU.. watoto wakija nyumbani utashangaa wanaanza kukuuliza kuhusu vyuo,

HII LIGI IFIKE MWISHO.
Umewaza kitoto sana mkuu, kuna chuo kama SUA unakuta hakifanani ata course 1 na chuo kama UDSM sasa huo mtihani utakuwa wa kuhusu nini ili wanafunzi wote wapimwe kwa mtihani mmoja, secondary ndio inawezekana kwakuwa wanafunzi wote wanasoma syllabus moja ndomana tunapata shule ya 1 hadi ya mwisho kwa ufaulu

Issue za kupima graduates wa chuo kipi ni wazuri kuliko wengine labda tuwe tunaangalia wafanyakazi wenye nafasi kubwa baadhi ya wizara na makampuni binafsi kwamba wamechangia vipi maendeleo ya sehemu husika walipo, japokuwa nakili sio kazi rahisi kujua kila boss wa sehemu flani ni graduate wa chuo fulani
 
Unapoongelea ubora wa chuo unamaanisha nini ?
mfano kwa exposure ya wanafunzi kwa wagonjwa wengi muhas is first, cuhas second ,kcmc third
Kwa majengo kcmc first, muhas second cuhas third
Kwa specialists wengi muhas first, cuhas second m kcmc third .... so huwezi kugeneralize vitu, kutoa product nzuri ni juhudi binafsi ya mwanafunzi kuclerk wagonjwa wengi na kujifunza kwa seniours.. mwanafunzi mzembe wa muhas atazidiwa mbali sana na mwanafunzi wa kiu anaejituma
 
Back
Top Bottom