Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Minong’ono ya kuteuliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi katika Mkutano Mkuu wa Januari 19, 2025 jijini Dodoma, imeendelea kutawala na safari hii imnepata kasi baada ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kutangaza kujiuzulu wadhifa wake akitaja uteuzi kuwa moja ya sababu za kufanya hivyo.
Katika barua yake aliyotangaza kujiuzuku Julai 13 na baadaye mkutano wake na waandishi wa habari wa Julai 18, Polepole ameeleza kinagaubaga namna (kwa maoni yake) utarataibu wa kumpitisha mgombea ulivyokiuka katika mkutano mkuu uliofanyika Januari 19, 2025 jijini Dodoma.
Miongoni mwa maswali wanayojiuliza watu, ni pamoja na lini Kamati kuu iliketi ikapitisha majina matano? Lini Halmashauri kuu ilijadili majina matatu? Kwa nini mchakato wa uteuzi wa majina uanzie kwenye Mkutano mkuu na sio Kamati Kuu?
Samia alipotangaza nia
Tangu Rais Samia alipoingia madarakani Machi 2021, alianza kuonyesha nia ya kutaka kugombea urais mwaka huu. Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Denmokrasia Duniani Septemba 15, 2021, Samia aliweka bayana nia yake ya kugombea. Ilikuw ani baada ya gazeti moja kumnukuu vibaya lidai kuwa hatagombea.
Baada ya kauli hiyo ya Rais Samia, mikakati ikaanza na mara tukaanza kuona viongozi wa Serikali na CCM wakisema kuwa fomu itatolewa moja. Japo haikuwa ni kwa kufuata Katiba ya CCM wala kanuni zake, lakini inaonyesha mpango huo ulilenga kuwatisha wanachama wengine waliotaka kugombea.
Japo inafahamika wazi kwamba, CCM imekuwa na utamaduni wa kumwachia rais aliyepo madarakani kugombea peke yake kipindi cha pili, lakini pia kumekuwa na mjadala, kwamba Je, hii ni mara ya kwanza kwa Samia kugombea urais au ni mara ya pili? Wengine wanahoji, Samia amerithi awamu ya tano ya urais au ameanza upya awamu ya sita?
Kwa jinsi anavyotambulishwa kama Rais wa Awamu ya Sita, basi huenda anachukuliwa kama anagombea mara ya pili. Iwe iwavyo, utamaduni huo unafifisha demokrasia.
Uhamasishaji ule wa fomu kutolewa moja, ulikwenda sambamba na kampeni ya kumchangia Rais Samia fomu ya urais, ambapo makundi mbalimbali yalijitokeza kumchangia.
Mkutano wa Januari 18, 19, 2025
Mkutano mkuu wa CCM wa Januari 18 na 19, 2025 ulikuwa maalum, ambapo pamoja na mengine ulimchagua Makamu Mwenyekiti, Stephen Wasira aliyeziba nafasi ya Abdulrahman Kinana na pia mkutano huo pia ulipitisha jina la Rais Samia kuwa mgombea urais.
Pia mkutano huo ulipitisha jina la Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kutetea nafasi yake hiyo, huku pia Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi akiteuliwa kuwa mgombea mwenza.
Inaelezwa kwamba, ajenda ya kumpitisha Samia ilikuja kama ya dharura, kwani ilikuwa ni mapema mno kufanya hivyo. Hata wakati Rais mstaafu, Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano huo, alisema yeye mwaka 2005 alipitishwa katika mkutano huu uliofanyika Mei 2005.
Huenda haraka hiyo ililenga kuwazima midomo makada waliotaja kuonyesha nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Utata wa kupitisha jina mkutano mkuu
Kwa mpangilio wa Katiba ya CCM, Mkutano mkuu ndio mkutano mkubwa wenye maamuzi ya mwisho katika chama hicho.
Katiba ya CCM ibara ya 103(7) kuhusu kazi za Kamati kuu inasema, “unapofika wakati wa Uchaguzi Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itashughulikia … (b) Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu majina ya Wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Kwa upande wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Ibara ya 102 (12) inasema, “Unapofika wakati wa Uchaguzi, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itashughulikia … (b) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya Wanachama wanaogombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuyawasilisha mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.
“(c) Kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.”
Baada ya mkutano huo, ibara ya 100 (5) inasema unapofika wakati wa uchaguzi, Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utashughulikia… (b) Kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.mambo kwenda kinyumenyume.”
Lakini katika mkutano huu, suala la kupendekeza jina la mgombea lilianzia kwenye mkutano mkuu Januari 19, 2025.
Katika mkutano ule, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alishauri mgombea huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mkutabo mkuu, atoke nje ili wamjadili, lakini Rais Samia alikataa akiwataka wajumbe wajadili mambo yote kwa uwazi.
Baada ya majadiliano ya hapa na pale, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete akapewa nafasi ya kutoa ufafanuzi, ambapo alipendekeza kutolewa kwa azimio ambalo wajumbe walipaswa kuliunga mkono au kulikataa.
Kweli pendekezo lile likasomwa na kisha Rais Samia mwenyewe akawauliza wajumbe wanaounga mkono na wanaopinga, inaonekana karibu wajumbe wote waliunga mkono.
Baada ya azimio lile kupitishwa, Rais Samia alisitisha mkutano kwa muda ili Halmashauri kuu ikalijadili jina lake, hivyo wajumbe wakaenda kikao kujadili jina lake na kisha ilipofika saa 9 alasiri, mkutano mkuu ukarudi na kisha kulipigia kura. Hapo ndipo Rais Samia alitoka nje.
Sasa kwa mchakato huu, lini Kamati kuu iliketi ikapitisha majina matano? Linidi Halmashauri kuu ilijadili majina matatu? Kwa nini mchakato wa uteuzi wa majina uanzie kwenye Mkutano mkuu na sio Kamati Kuu?
Maswali kama haya ndiyo yaliyomwibua kada wa CCM, Mchungaji Godfrey Malisa aliyekosoa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho. Lakini Februari 10, 2025, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel alitangaza kumfukuza uanachama Malisa akisema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.
Hayo ndio anayolalamikia Balozi Polepole, Je yatapita hivi hivi?