Utata: Mabomu 20 ya Kurusha Kwa Mkono Yakamatwa Katika Shule ya Msingi Dar es Salaam

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Na Mwandishi Wetu | Sept 23, 2006

MABOMU 20 ya kurusha kwa mkono, yamekamatwa katika moja ya shule za msingi jijini la Dar es Salaam.

Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa mabomu hayo yalikamatwa hivi karibuni, na habari hizo zimeendelea kuwa siri kubwa ndani ya Jeshi la Polisi mkoani humo.

Habari za uhakika zinasema kuwa mabomu hayo yalikutwa yakiwa na nyaraka za mmoja wa waliokuwa wagombea udiwani, kupitia chama ambacho kwa sasa Tanzania Daima inaendelea kuhifadhi jina lake.

Makachero wa Kituo cha Polisi Msimbazi, kwa siku kadhaa sasa wako kwenye uchunguzi mkali wa kujua mmiliki wa mabomu hayo hatari.

Chanzo chetu kilieleza kuwa mabomu hayo yalikuwa ndani ya droo ya meza ambayo ilipelekwa shuleni hapo na baadhi ya waumini kwa madai kwamba ilikuwa ikitumiwa usiku kwa mambo yasiyo ya uadilifu.

Meza hiyo ilitolewa katika moja ya nyumba za ibada zilizo karibu na shule hiyo.

Mwalimu mkuu alikaa na meza hiyo kwa siku nyingi, siku moja akaamua kufungua droo ili kujua kilichomo, alishangaa kuona akikutana na vitu ambavyo hakuvijua.

Walimu walishauriana wavichome, lakini mmoja akaona si vitu vya kawaida, wakaamua kumuita mzee mmoja ambaye amewahi kuwa askari.

Alipofika, alibaini kuwa ni mabomu, taarifa ikapelekwa kwa ofisa elimu wa wilaya, baadaye viongozi na polisi walifika na kuthibitisha kuwa walichokiona ni mabomu ya kurusha kwa mkono.

Ndani ya droo hiyo pia kulikuwa na karatasi za za kugombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kilisema chanzo hicho.

Suala hilo limeendelea kuwa nyeti, kwani hata viongozi wa polisi, hawataki kulizungumza, kwa maelezo kuwa uchunguzi wake bado unaendelea.

Habari zilizopatikana baaaye zilisema mtuhumiwa ambaye alikuwa mgombea udiwani, tayari ameshanaswa na anahojiwa.
 
Back
Top Bottom