Utata Kifo Cha TUPAC, Majibu Ya Uchunguzi Nyumbani Kwa Keefe D

Eugen TZA

Member
Aug 7, 2023
61
98
Ripoti zinaeleza kuwa risasi zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Rappa TUPAC Keefe D hazifanani na maganda ya risasi zilizokutwa eneo la tukio alipopigwa risasi Tupac mwaka 1996.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchini Marekani vinaeleza kuwa licha ya taarifa hizi bado polisi wala chombo chochote cha habari hawajaripoti kuhusu kama Keefe D hana hatia katika kesi hiyo au nini kinaendelea mpaka sasa baada ya taarifa hizi.

Mapema mwezi uliopita polisi walitangaza kufanya uchunguzi kuhusu risasi zilizokutwa katika nyumba ya KEEFE D ambaye yeye na washkaji wengine wanne walikua na Tupac siku ya tukio la kifo chake kuangalia kama zinafanana na risasi zilizokutwa katika mwili wa Tupac.

Uchunguzi huu umefanyika kutokana na Keefe D kuonyesha kukiri katika mahojiano kuwa alimpa binamu yake Orlando Anderson (Ambaye Pia Ni Mtuhumiwa) bunduki ambayo huenda aliitumia kumpiga risasi Rappa Tupac licha ya kwamba bado visibitisho vinakosekana ikiwemo bunduki iliyotumika Glock Pistol.

Baada ya taarifa hizi baadhi ya mashabiki wameendelea kuzungumzia nadharia ile inayosemwa na wengi kuwa Tupac yupo hai Cuba, Wakijiuliza maswali mengi kuhusu upelelezi unapendelea kufanyika kama utazaa matunda kweli baada ya miaka 30 kupita sasa bado muuaji wa Tupac hajulikani.

CDT/ abcnews via nojumper

PeaceOverInterest
 
Back
Top Bottom