Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

hivi mtu huwezi kutoa maoni yako bila kuquote uzi ...?
 
mkuu the bold naomba uteletee historia ya mtu mmoja mbabe sana enzi hizo,The late Manuel Noriega mkuu tafadhali sana tuletee huyu mtu historia yake ni ya kusisimua sana
 
samahani The bold hivi malipo ya 5000 kuunganishwa kwenye wasap ni ya kila mwezi au mimi nimeelewa tofauti??
 
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY



SEHEMU YA TANO


Inaendelea kutoka ilipoishia sehemu ya NNE….



Bay Of Pigs Invasion

Mara tu baada ya Fidel Castro kuchukua madaraka mwaka 1959, mwaka uliofuata yaani mwaka 1960, CIA kwa ruhusa ya Rais Dwight Eisenhower ambaye alikuwa anakaribia kuondoka madarakani walianzisha mikakati ya namna gani watamuondoa madarakani Fidel Castro.

Fursa kuuu waliyoiona ni kutumia wahamiaji walioingia Marekani kutoka Cuba kukimbia utawala wa Fidel Castro uliokuwa "unafanya usafi" dhidi ya raia waliokuwa wanamuunga mkono Fulgencio Batista.

Kwa hiyo CIA wakakusanya mamia ya raia hawa kwa siri kubwa na kuwapandikizia hari na ushaiwshi wa kutaka kumpindua Fidel Castro.

Mwezi March mwaka 1960 rais Dwight Eisenhower alipitisha bajeti ya dola milioni 13.1 kwa ajili ya mpango huu wa mapinduzi.

Raia hawa wa Cuba waluokimbilia uhamishoni nchini Marekani wakapelekwa nchini Guatemala kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi hili kujiandaa na mapinduzi.

Kikosi hiki kiliitwa Brigade 2506.


Mafunzo haya ya kijeshi yakaendelea kwa mwaka mzima nchini Guatemala.

Mpango huu wa kuivamia Libya na kumpindua Fidel Castro ulipangwa ufanyike mapema mwaka 1961 na ulikuwa umekamilika kila kitu lakini rais Eisenhower hakuupa 'approval' na aliacha jukumu hilo la kuidhinisha uvamizi huo ifanywe na atakaye kuja kumrithi yaani Rais JF Kennedy.


Kwa hiyo mara baada ya uchaguzi mkuu mwezi November, 1960 na hatimaye JF Kennedy kuapishwa January 20 mwaka 1961, kitu cha kwanza ambacho alikabiliana nacho ni CIA kumkabidhi mkakati ulioandaliwa na wao CIA chini ya Rais Dwight Eisenhower kuhusu uvamizi wa Cuba na kumpindua Fidel Castro.

Hapa ndipo ambapo kulianza kutokea mfululizo wa matukio ambayo huko mbeleni yalikuja kutengeneza uhasama mkubwa kati ya Rais Kennedy na CIA.


Katika jamii ya intelijensia, taarifa zinazoaminika ni kwamba CIA walipowasilisha mkakati wao wa mapinduzi ya Fidel Castro kuna vitu vingi vya msingi walimficha Kennedy. Na hii inaonekana kwamba walichukua 'advantage' kwa sababu ya ugeni wa Kennedy katika wadhifa wake huu upya wa Urais na kwa hiyo kutofahamu uhalisia wa vitu vingi kwa hiyo CIA wakatumia hiyo fursa 'kum-mislead' katika vitu muhimu kuhusu mkakati huo.

Mkakati ulikuwa ni mpana sana, lakini kwa ufupi ni kwamba, wavamizi hawa wa Brigade 2506 ilikuwa imepangwa wavamie Cuba wakitokea Guatemala na Nicaragua wakiwa na askari wa miguu pekee.

Kennedy hakutaka Marekani ionekane ikihusika moja kwa moja kwenye uvamizi huo ili kulinda taswira yake katika jamii ya kimataifa na pia kuepuka kuamsha hasira za Urusi ambao walikuwa ni mshirika mkubwa wa Cuba.

Kwa hiyo kukabiliana na hili, CIA walipendekeza kuwatumia makomando wake wa SAD katika kuongoza wapiganaji wa Brigade 2506.

Pamoja na hayo yote, Rais Kennedy alisisitiza sana kwamba ili kulinda taswira ya nchi ya Marekani yeye kama Rais hatoruhusu Marekani kufanya mashambulizi ya anga kusaidia katika mapambani hayo ya kumuondoa madarakani Fidel Castro.

CIA huku wakijua fika kwamba hawawezi kushinda uvamizi huo pasipo mashambulizi ya anga wakakubaliana na sharti la Rais Kennedy kwamba hakutakuwa na mashambulizi ya anga. Walikubali hili huku wakiwa na dhamira iliyojificha kwamba mara tu vita hiyo itakapoanza watamshinikiza Rais Kennedy atoe ruhusa ya kufanyika mashambulizi ya anga. Walikuwa wanaamini kwamba lazima Rais Kennedy atakubaliana na shinikizo lao pindi atakapoonyeshwa umuhimu wa mashambulizi ya anga pindi vita ikiwa inaendelea, na lazima atafanya hivyo ili kuepusha Marekani kuaibika kushindwa vita wanayoiunga mkono ili kulinda heshima yai ya kijeshi ambayo ilikuwa inahitajika kuliko kitu chochote katika kipindi hiki cha vita baridi.

Rais Kennedy aliidhinisha rasmi uvamizi huu siku ya tarehe 4 April 1961, takribani miezi mitatu tu baada ya kuingia madarakani.

Wapiganaji wapatao 1400 wa Brigade 2605 waliogawanywa katika infantry batalioni zipatazo tano na paratrooper battalion moja waliingia katika pwani ya Cuba iitwayo Playa Girón kwa kutumia boti kutokea Guatemala na Nicaragua siku ya tarehe 13 April 1961.

Baada ya uvamizi tu kuanza CIA wakaanza kuweka shinikizo kwa rais Kennedy aruhusu japo shambulio moja la anga la ndege za kivita za Marekani kuharibu miundombinu ya viawanja vya ndege za kijeshi vya Cuba. Kennedy alikataa katakata lakini CIA walipozidisha shinikizo na kumpa angalizo kuwa wasipofanya hivyo kuna uwezekano wa wapiganaji hao kushindwa kutekeleza mapinduzi ya kumuondoa Fidel Castro, Kennedy alilainika na kuruhusu mashambulio ya anga kwa awamu moja pekee.


Hivyo basi tarehe 15 April 1961 ndege za kijeshi zilizo chini ya CIA aina ya B-26, zilishambulia viwanja vya ndege za jeshi la Cuba na hatimaye tarehe 16 April wapiganaji wa Brigade 2506 walivamia rasmi Cuba.

Mwanzoni mwa uvamizi huu wapiganaji wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa SAD katika CIA walionekana kulidhibiti jeshi la Cuba ambapo mwanzoni mwa mapambano haya upande wa Cuba vikosi vya kijeshi vilikuwa vinaongozwa na José Ramón Fernández.

Baada kuonekana kuwa jeshi la Cuba linazidiwa ujanja na wavamizi hawa waliokuja kufanya mapinduzi, Fidel Castro mwenyewe akaingia katika uwanja wa vita na kumuondoa José Fernández kwenye jukumu la kuongoza jeshi kwenye mapambano haya na kujipa yeye binafsi hilo jukimu la kuongoza wanajeshi.

Baada ya Castro kushikilia usukani wa kuongoza mapambano kwa upande wa jeshi la Cuba, wavamizi wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa Marekani walizidiwa ujanja na mbinu zote na wakaanza kupigwa kwa aibu kubwa.
Mpaka kufika tarehe 19 April, ilikuwa dhahiri kwamba ushindi uko upande wa vikosi vya Cuba, kwani walikuwa wanawapiga wavamizi kwa urahisi kana kwamba wanamsukuma mlevi.

Ndipo hapa ambapo CIA wakarudi tena kwa rais Kennedy kutaka aidhinishe mashambulizi mengine ya anga.
Safari hii Kennedy alikataa katakata, akidai kuwa dunia nzima itaona uvamizi huu imefanywa na Marekani na sio raia wa Cuba wanaoishi uhamishoni.
Kennedy alihofia kuwa kama Marekani itaingilia mapigano hayo kwa kiwango hicho, kulikuwa na uwezekano wa Urusi nayo kuingilia vita hiyo kusaidia upande wa Cuba.

Kutokana na mvutano mkubwa uliokuwepo baina yao, Kennedy alihofia kuwa ingeweza kuchochea vita nyingine kati ya Marekani na Urusi, vita ambayo ingeigharimu pande zote mbili na Dunia nzima kwa ujumla na pengine hata kusababisha vita kuu ya Tatu ya Dunia.
Kwa hiyo Kennedy safari hii akakataa katakata kuidhinisha mashambulio ya anga kwa kutumia jeshi la Marekani.

Joint Chiefs Of Staffs wakaja na pendekezo kwamba litengenezwe shambulio la uongo kwenye pwani ya Marekani na kisha kutupa lawama kwa Cuba ili kuhalalisha mashambulizi ya anga nchini Cuba, lakini bado pia Kennedy alishikilia msimamo wake kwamba hawezi kuidhinisha shambulio lolote la anga kufanywa na jeshi la Marekani.

Hapa ndipo ambapo CIA iliumbuka, mkakati wao tangu awali ulikuwa ni lazima mashambulizi ya anga yafanyike kama ili kuweza kushinda mapigano na kuvishinda vikosi vya Castro na kumuondoa Madarakani. Lakini walimficha kitu hiki Rais Kennedy baada ya kumuona kuwa hasingeli idhinisha uvamizi huo kama wangemuweka wazi kuwa hawawezi kushinda pasipo mashambulio ya anga. Tegemeo lao la kumshawishi tena kwa mara ya pili yafanyike mashambulio ya anga ndio yalikuwa yamegonga mwamba.


e675d7549fa820670831d38c5e89795e.jpg

Fidel Castro akiwa mstari wa mbele kuongoza wanajeshi wake


8658476c60b8adff99b95ef29f0d1ec7.jpg

Mateka walivamia Cuba kwenda kumpindua Fidel Castro wakiwa chini ya Ulinzi


4756a8ee74d31e100e362ba04c03d7de.jpg

Vikosi vya Cuba wakishangilia ushindi



Tarehe 20 April 1961, siku tatu baada ya uvamizi, wapiganaji waliipatowa mafunzo na kuongozalwa na makomando wa Marekani, waliovamia nchini Cuba ili kumpindua Fidel Castro waliweka silaha chini na kusarenda kwa vikosi vya jeshi la Cuba.

Ilikuwa ni aibu kubwa ambayo haijawahi kutokea katika historia ya jeshi la Marekani. Mateka waliokamatwa na vikosi vya Fidel Castro walihojiwa mubashara kwenye televisheni nchini Cuba na kutoa siri zote namna ambavyo Marekani ilihuiska katika uvamizi huo.

Wakati ambapo Marekani walikuwa wanatafuta sehemu ya kuficha nyuso zao kwa aibu, nchini Cuba taifa zima lilikuwa linasheherekea kwa shamra shamra kushangilia ushindi huo mnono. Fidel Castro aligeuka kuwa shujaa mpya wa Taifa na kujipatia heshima kubwa kimataifa kwa kushinda vita dhidi ya jeshi hatari la 'Marekani'.


Huko Marekani bado bundi alikuwa ndio kwanza ametua. Kila upande ulikuwa unamsukumia lawama upande mwingine.

CIA walimuona Rais Kennedy kama ndio kisababishi cha wao kushindwa kutekeleza kwa ufanisi uvamizi na hatimaye kufanikisha kumuondoa madarakani Fidel Castro.
Na kwa upande wa Rais Kennedy aliwaona CIA kama wasaliti kwa 'kumdanganya' na kutompa mkakati kamili tangu mwanzoni kwamba wasingelieweza kushinda vita ile pasipo mashambulizi ya anga.


CIA wakamuona Rais Kennedy kama kiongozi ambaye si imara na shupavu au jasiri, na kwa muono wao walihisi kuwa hatoshi kuwa Rais wa Marekani.
Kwa upande wake Kennedy aliwaona CIA kama taasisk iliyopewa nguvu kiasi kwamba imelewa madaraka na kujiona wako huu ya kila kitu na kila mtu. Na moyoni mwake aliamini kuwa hilo linatakiwa kubadilika.

Ikumbukwe pia kwamba hapa ilikuwa imepita miezi mitatu pekee tangu CIA wamuue Patrice Lumumba siku ya Tarehe 17 January, 1961 jimboni Katanga, Congo-Kinshasa.
Kennedy anafahamika kuwa hakupendezwa na hili tukio lakini kwa kuwa lilitokea kabla hajawa Rais (siku tatu kabla) basi alilimezea mate lakini bado alibaki na kinyongo. Kwa hiyo kufeli kwa uvamizi wa Bay of Pigs kuliamsha hasira zake zote alizonazo dhidi ya CIA.

Japokuwa katika umma na hata alipoongea na wanahabari Kennedy alikubali kubeba lawama zote kwa kuwa yeye ndiye aliidhinisha uvamizi huo, lakini pembeni akiwa faragha na wakubwa wenzake alikuwa anaotupia lawama kubwa CIA kuwa ndio waliosbabisha aibu kubwa hii iliyoipata Marekani na jeshi lake.

Baada ya hapa mwenendo wa Kennedy ukaanza kubadilika mno. Mwanzoni alipoingia madarakani alikuwa ni tegemezi mno kwa kupatiwa muhtasri wa hali ya usalama wa nchi (Daily Presidential Briefing) kutoka kwa vyomvo vya Ujasusi hasa CIA, lakini baada ya tukio la kufeli kwa uvamizi wa Cuba hakutaka tena kupatiwa briefing na CIA badala yake briefings zake zote sasa alizipokea kutoka kwa washauri wa usalama wa taifa (National Security Advisors).

Lakini hakuishia hapo tu, Kennedy kuonesha ni namna gani alikasirishwa alienda mbali zaidi kufanya kitendo ambacho kilipingwa na maafisa wengi wa CIA na wanazi wao.
Kennedy alimfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Allen Dulles.

Katika ulimwengu wa Intelijensia unapomuongelea Allen Dulles hamuongelei tu jasusi, bali ni jasusi mkongwe na mzoefu na wa kiwango cha daraja la kwanza kabisa na mwenye heshima iliyotukuka.

Allen Dulles ndiye Mkurugenzi wa CIA aliyetumikia kwa kipinfi kirefu zaidi katika historia ya Taasisi hiyo mpaka leo hii (tangu 1953 mpaka 1961).

Allen Dulles ndiye aliyesimami mapinduzi ya Waziri mkuu wa Iran miaka ya 1940s (Operation Ajax).

(Nimewahi kuandika hiki kisa, wasiliana nami kama hujawahi kukisoma nikutumie)

Allen Dulles ndiye aliyesimamia mapinduzi ya Rais wa Guatemala mika 1950s.

(Nimeandika pia kuhus kisa hiki, tuwasilianne kama hujakisoma).

Allen Dulles ndiye aliyesimamia program ya ndege za kijeshi ya Lockheed U-2.

Allen Dulles ni kaka wa John Dulles, waziri wa mambo ya nje wa Marekani (Secretary of State) wakati wa utawala wa Rais Dwight Eisenhower ambaye ndiye amerithiwa na Kennedy miezi mitatu iliyopita.

Kwa hiyo inahitaji kujitoa ufahamu kumgusa mtu kama Allen Dulles. Na Kennedy alijitoa ufahamu na kumfuta kazi Allen Dulles mtu ambaye anapendwa na kuhusudiwa na majasusi wa CIA pengine kushinda hata Kennedy mwenyewe.


cb30a46961fd88457fd1261a80604edf.jpg

Karatasi ya juu ya ripoti rasmi ya CIA ambayo ndani yake kuna baadhi ya paragraph zikionyesha kuwa CIA hawakuridhishwa na namna ambavyo Kennedy alifanya maamuzi juu ya kukataa mashambulio ya anga

Kennedy hakuishia hapa tu… akiwa faragha na wakubwa wenzake alitamka kauli iliyokuja kuwa maarufu sana hapo baadae baada ya kuvuja, alisema hivi, namnukuu;


"…i want to splinter CIA in a thousand pieces and scatter it to the wind.."

(Nataka kuivunja vunja CIA kwenye vipande elfu na kuipeperusha kwenye upepo)


Akiwa na maana kwamba, amedhamiria kuibomoa CIA taratibu sana kipande kimoja baada ya kingine mpaka taasisi hiyo ipotee yote na isiwepo.


Kauli yake hii, ilikuwa ni kana kwamba alikuwa ametia sahini ya kifo chake mwenyewe.






84e282da29fb20519baa8a97556179a7.jpg

Huyu ndiye jasusi mbobezi Allen Dulles aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CIA




Itaendelea....


THE BOLD - 0718 096 811


Nimepata ufahamu kiasi kikubwa kuhusu haya mauwaji ambayo yalitokea miaka hiyo.
 
pamoja na hayo kunatetesi zinasema kwamba kennedy alitaka CIA isiwepo thats why wakammaliza.
 
Back
Top Bottom