Habari wakuu,
Naomba mniwie radhi kwa kuwa kimya, kuna changamoto imejitokeza...
Gazeti la
RAI wanafanya uhuni kwa kuiba hii makala humu na kwenda kuichapa huko kwenye gazeti lao bila kunitaarifu au makubaliano yoyote.
Hili suala limeniuma sana sana wakuu, kuandika hizi makala ni kazi nzito na inahitaji kujitoa hasa... Inatumia muda mwingi, kutafiti na kukaa chini kuandika na pia kuumiza akili ili kuweza kuandika kwa ubunifu itoke makala ya kuvutia.! Bila kusahahu kuwa pia kuna rasilimali natumia ili kufanikisha haya yote... Rasilimali fedha na rasilimali muda!
Mara nyingi inanibidi nijibane muda wangu mchana nifanye mizunguko yangu mingine halafu usiku nisilale ili nijipe muda wa kuandika hizi makala.! Inauma sana pale wanapojitokeza wahuni fulani na kunakili andishi langu na kwenda kulitumia pasipo ruhusa yangu, wala kunitaarifu au makubaliano yoyote!
Mwaka jana pia ilitokea changamoto kama hii kwa gazeti la Kisiwa kunakili makala yangu ya "Geranimo" na tulisumbuana sana..
Niko natafuta msaada wa kisheria ili kuona nashughulikia vipi changamoto hii ya uhuni uliofanywa na gazeti hili la
RAI...
Hapa chini nimeweka screenshots kutoka katika tovuti yao...
Na si hawa tu, Shigongo moja ya watu ninao waheshimu sana amefanya uhuni kama huu kupitia tovuti yake ya Global Publishers kwa kunakili makala yangu ya "Plata O Plomo" kuhusu maisha ya Pablo Escobar...
Nimeweka screenshots hapa chini pia...
Wakuu, hili suala limeniuma sana moyo, haiwezekani mimi niteseke kukesha usiku kuandika halafu wahuni fulani wanakuja kujinufaisha kwa kazi zangu bila makubaliano nami...
Niko natafuta msaada wa kisheria nione nafanyaje! Pia naomba ushauri wako kwa namna yoyote unayohisi inaweza kunisaidia kuwawajibisha hawa wahuni..
Inauma sana wakuu!!