Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

yaani sister, mtoto wangu huwa anapenda sana kuangalia western movie za action, na spy movies. sasa huwa anachukulia zilivyo tayarishwa ni uhalisia. sasa mimi sipendi awe upande hasi, kwa hiyo huwa namfungulia web nyingi tofauti ajifunze ukweli. hasa kwenye wikipedia namwelekeza jinsi ya kuchukua detail kutoka vyanzo tofauti.mimi ni mkristo, ila nimeuchambua ukristo, asili yake, kwa nini kuna madhehebu tofauti. upi uhusiano wa mkristo na myahudi, upi uhusano kati ya mkristo na muislam, kuna uhusiano upi kati ya dini hizi mbili kwenye uumbaji kwa ujumla. na hayo yote mtoto wangu ana uelewa mkubwa sana. sasa kwenye jf huwa nampa baadhi ya posts ambazo naona zitamsaidia kuangalia jinsi watu tofauti wanavyo fikiria( different ways of thinking ) kwa kweli ame improve kiasi kikubwa kwenye IQ yake. kwa sasa sina muda, ila nilipenda sana kama ningeweza kupata muda nikaweka hapa uzi unaohusu ethiopia na sudani, katika ulimwengu wa roho, watu hawawezi kukubali au kuamini kirahisi, lakini ndio ukweli. nikipata muda nitajitahidi. good day sis..[emoji106] [emoji106] [emoji106]
Mbona unajiquote mwenyewe
 
Dr Eric? We et re refat set? See went !? Dr 🙂 🙄 🙁 🙄 🙁 🙁 😕 🙄 😕 🙄 🙁 🙄 😡 🙁 😡 🙁 🙄 🙁 🙁 🙁 🙁 😎 😡 😕 🙄 😳 🙂 🙂 🙁 🙂 😎 🙂 😎 😎 🙂 😎 🙄 🙁 🙄 🙄 🙄 🙄 🙄 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙁 🙄 🙄 🙄 😡 🙁 🙄 🙁 🙄 🙄 🙄 🙁 🙁 🙁 😳 🙁 🙄 🙁 😡 🙄 🙂 😡 😎 😱 😵 😵 🙄 🙂 😳 🙂 😎
Umefurahii mwenyewe ulivyoquote story nzima na kuweka viemoj
 
sister naomba nikuulize, hivi huu ustaarabu wako, hekima, na upole, ni maisha yako halisi ? au ni hapa jf tuu ?
kama ndio ulivyo ki uhalisia, basi una baraka kwa muumba. na kama una mume, jamaa amejaaliwa. hilo ni kutoka moyoni mwangu. una mtazamo ambao ni nadra kupatikana. and that's the fact.
dont ask me why..!!
almighty god keep you bleesed [emoji106][emoji106] !!
 
Niliwahi kuwasoma consipiracistst tofauti tofauti juu ya mauaji ya Kennedy. Nikaona napelekwa in depth hata kwa mengine ambayo sikuyawaza. Hii dunia ina mambo mazito na makubwa.
 
naomba uwe unani tag maana huwa nakufuatilia sana kwenye nyuzi zako,kila wakati huwa naingia kwenye hili forum ili kuona kama umetoa kitu kipya
Mkuu siku nyingine usibonyeze kitufe cha -reply- maana kwa sisi tunaotumia smart phone hadithi ndefu kama hii inatupa shida. Unaweza kumtag kwa kuanza na herufi @ ikifuatiwa na jina lake (id) utakuwa tayari umemfikia
 
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY




SEHEMU YA PILI





Katika sehemu iliyopita nilijadili mfululizo wa matukio yaloyopelekea kukamatwa kwa Lee Harvey Oswald na kuhusishwa na kifo cha polisi J.D Tippit na baadae kuhusishwa na kifo cha Rais JF Kennedy.

Katika sehemu hii ya tano nitajadili kuhusu utata unaozunguka uhusishwaji wa Oswald na kifo cha Kennedy na muingiliano uliopo na magenge ya uhalifu pamoja na vyombo vya ulinzi unaoonhesha dalili ya uhusika wao katika kifo cha Kennedy.


Tuendelee…




OSWALD CHINI YA MIKONO YA POLISI NA KIFO CHAKE


Baada ya Oswald kukamatwa kutoka jumba la kuonyesha sinema la Texas Theatre, moja kwa moja akapelekwa makao makuu ya polisi ya Dallas.
Akiwa hapo kituoni Oswald alihojiwa na Asifa wa FBI, Special Agent James P. Hosty pamoja na Afisa mkuu wa Polisi kituo cha Dallas Captain Will Frizt.

Oswald alikana kuhusika kabisa na mauaji yote mawili, yaani mauaji ya Rais Kennedy na mauaji ya polisi J. D Tippit.
Akajieleza kwamba siku ya tukio ni kweli alikuwa kwenye jengo la Texas School Books Depository na hakukuwa na ajabu yeye kuwepo hapo kwa kuwa anafanya kazi kwenye jengo hilo.
Akaendelea kujieleza kuwa wakati tukio linatokea alikuwa anakula chakula cha mchana kwenye ghorofa ya kwanza na hakuwa anajua kinachoendelea huko mtaani na baada ya kumaliza kula chakula akapanda mpaka ghorlfa ya pili ili kwenda kuchukua soda aina ya coca cola kwenye 'vending machine'. (Ndio hii soda ambayo nilieleza kwenye sehemu iliyopita kwamba kuna mama secretary wa jengo hilo alimuona Oswald ameibeba akiwa anatoka nje ya jengo).

Oswald akaeleza kuwa akiwa anarejea kutoka ghorofa ya pili kwenda ghorofa ya kwanza alikuta na wafanya kazi wengine wawili weusi ambao nao ni waajiriwa wa jengo hilo. Oswald aliwaeleza kumtambua mfanya kazi mmoja kwa jina la 'Junior' na mwingine hakuwa anamkumbuka kwa jina.

Polisi baadae waliwahoji wafanyakazi weusi wanaofanya kazi kwenye jengo hilo na walijitokeza wafanya kazi wawili Junior Jarman na Harold Norman ambao walikiri kwamba walimuona mtu akiwa kwenye chumba cha chakula au 'Domino Room' kama ambavyo walizoea kukiita lakini walikiri kuwa hawakuwa makini kumuangalia ni nani hivyo hawakumbuki.

Oswald akaendelea kueleza kuwa aliporejea kwenye chumba cha chakula na kuketi ili ajiburudishe na soda yake ya coca cola, ndipo ghafla alishituka anaingia polisi ambaye baadae alikuja kumtambua kama Marion Baker na kumnyooshea bastola.

Licha ya maelezo yote haya lakini bado waliendelea kumbana na kumlazisha kukiri uhusika wake kwenye kumdungua Rais Kennedy.

Walimuonyesha Picha ambayo ilionyesha Oswald akiwa ameshikilia bunduki ambayo iliaminika kumdungua Rais Kennedy.
Oswald alikanusha na kudai kuwa picha hiyo imetengenezwa.

Wakamuonyesha pia risiti za ununuzi wa bunduki hiyo kwa kutumia jina bandia la "A.J Hidell" lakini bunduki hiyo ilitumwa kwenye anuani ya nyumbani kwake.
Oswald akakanusha kufanya manunuzi hayo na kusisitiza kuwa huo ni "mchoro" kuna watu wanajaribu kumsingizia yeye shutuma hizo ili kuficha wahusika halisi.

Kitu pekee ambacho Oswald alikiri ni kumiliki bastola 0.38 revolver na alidai kuwa anaimilili kwa mujibu wa sheria na ulinzi binafsi.
Pia ikumbukwe kuwa Oswald aliwahi kutumikia jeshi la Marekani kikosi cha Marine Corps.

Oswald pia alikataa kabisa kuwakilishwa na mawakili wa utetezi qa serikali au wale ambao serikali ilikiwa tayari kumlipia kama haki yake ya kiraia, Oswald alidai kuwa hakuwa na imani na watu hao au serikali kumtendea haki kwenye suala hili.

Wakili pekee ambaye Oswald alikubali amuwakilishe kwenye mahojiano na kipindi cha kesi kusikilizwa alikuwa ni Bw. John Abt ambaye alikuwa anatokea American Civil Liberties Union.
Lakini ajabu ni kwamba kwa siku zote mbili za mahojiano ya Oswald, John Abt alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya nyumbani wala sehemu yake ya kazi.

f800e95991f420e7f347769001ec33e9.jpg

Sekunde chache kabla ya Lee Harvey Oswald Kuuwawa... Tazama huyo mkono wa kulia pembeni anayemsogelea Oswald na silaha huku wanausalama wakimtazama


Mahojiano ya polisi na Oswald yaliendelea kwa muda wa siku mbili mfululizo.

Siku mbili zilipopita yaani siku ya Novemba 24, 1963 vyombo vya ulinzi viliazimia kumuhamisha Lee Oswald kutoka katika mahabusu ya polisi kituo cha Dallas na kumpeleka gerezani kwa ajili ya kushikiliwa kwa usalama zaidi akisubiria mahojiano zaidi na kesi yake kuanza kuunguruma.

Muda wa saa 5 na dakika 15 asubuhi, Oswald alifunguliwa na kutolewa kwenye selo na baada ya kusainiwa kwa makaratasi yake ya kuhamishwa kutoka hapo kituoni ili apelekwe gerezani.


Saa 5 na dakika 19 Oswald alikuwa anakaribia kufika kwenye mlango wa ghorofa ya chini kabisa (basement) ili kupelekwa kwenye gari maalumu lisilopenya risasi ambalo lilikuwa linasubiri ili kumbeba na kumpeleka gerezani.

Tukio hili lilikuwa limeteka hisia za taifa zima na lilikuwa linafuatiliwa kila kona ya nchi ya Marekani na duniani kote kwa hiyo vituo vingi vya televisheni lilikuwa vinarusha tukio hili moja kwa moja, mubashara kabisa.

Saa 5 na dakika 20 polisi wawili walitoka mlangoni ili kuhakikisha usalama na sekunde chache baadae Oswald akiwa amefungwa pingu na kuzungukwa na wanausalama kila kona alitoka kwenye mlango wa jengo kuingia basement ili aweze kupelekwa kwenye gari inayowasubiri.


Oswald na maaskari waliokuwa wamemzunguka walipiga kama hatua tano tu au sita na ghafla akajitokeza mtu aliyekuwa pembeni yao amekaa pamoja na wana Habari, na mkononi mwake alikuwa ameshika bastola akiielekeza moja kwa moja kwa Oswald.

Hii lilikuwa ni saa 5 na dakika 21.

Kabla wanausalama hawajafanya lolote, mtu huyu alimfyatulia risasi ya tumboni Oswald na moja kwa moja Oswald akadondoka chini.
Wanausalama wakafanikiwa kumdhibiti mtu huyu na kumkamata na moja kwa moja wakamuingiza ndani kwenye kituo cha Polisi pamoja na Oswald.

Mtu huyu aliyempiga risasi Oswald anaitwa Jack Ruby na ni moja ya watu maarufu sana Dallas katika kipindi hicho kutokana na kumiliki Klabu kubwa ya usiku mjini hapo.

Dakika chache baadae Oswald alichukuliwa na gari ya wagonjwa na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital (hospitali ile ile aliyofia Kennedy siku mbili nyuma).


Risasi aliyopigwa Oswald iliingia ubavu wa kushoto na ilikuwa imeenda kuharibu kabisa bandama, aorta, vena cava, figo, ini, diaphragm na mbavu ya kumi na moja ya kushoto na ikakwama katika ubavu wa kulia.


Vile vile pia baada ya "juhudi kubwa" za madaktari kuokoa maisha ya Oswald kutozaa matunda hatimaye muda wa saa 7 na dakika 7 siku hiyo ya Novemba 24, Dallas Police Chief Bw. Jesse Curry aliutangazia uliwengu kuwa mtuhumiwa pekee wa mauaji ya Rais JF Kennedy, Bw. Lee Harvey Oswald amefariki dunia.


Mara moja baada ya habari hii kutangazwa iliwafanya watu wengi waanze kukuna vichwa.

Siku mbili nyuma mara baada ya Rais Kennedy kupigwa risasi kulianza kuibuka minong'ono mitaani kwamba huo ulikiwa ni 'mchoro' wa watu wenye nguvu kwenye 'system'!
Baadae siku hiyo hiyo ilipotangazwa kuwa muuaji wa Kennedy amekamatwa, sintofahamu ikaongezeka zaidi kuwa imekuwaje mtu ambaye ametekeleza mauaji makubwa hivyo akamatwe 'kizembe' na kwa haraka namna hiyo.


Lakini ilipotolewa taarifa ya Oswald kuuwawa, huko mtaani asilimia kubwa ya wananchi wazo moja kuu lilitawala vichwani mwao, kuwa "Oswald alikuwa amenyamazishwa"! Kuna uwezekano mkubwa wahusika halisi wa kifo cha Kennedy walikuwa wanahofia kesi ya Oswald kuanza kuunguruma kwani walihofia labda Oswald "angemwaga mchele!"

Pia kilichosgangaza zaidi ni mtu aliyempiga risasi Oswald. Jack Ruby ni mfanyabiashara mkubwa, mtu mwenye 'status' hapo Dallas.
Inawezekaje mtu wa hadhi yake afanye kitu cha kipuuzi kiasi hicho kwa kumpiga mtu risasi hadharani mbele ya vyombo vya habari kwa suala ambalo alimuhusu moja kwa moja?? Ana maslahi gani kufanya hivyo??


Sasa ilikuwa dhahiri kwamba, kuna jambo kubwa zaidi linafichwa nyuma ya pazia… kuna wahusika halisi wa kifo cha Kennedy!!


Ni kina nani?? Na kwa nini walimuua Kennedy??

Hakuna mwenye majibu kamili ya asilimia mia, lakini nitajitahidi kuleta kwenu vidhibiti kadhaa ambavyo vitasaidia kila mmoja kufikia conclusion yake binafsi!!


Tazama Video jinsi ambavyo Jack Ruby alimpiga risasi Oswald mbele ya Wanausalama na vyombo vya habari

Itaendelea...


The Bold - 0718 096 811
 
sister naomba nikuulize, hivi huu ustaarabu wako, hekima, na upole, ni maisha yako halisi ? au ni hapa jf tuu ?
kama ndio ulivyo ki uhalisia, basi una baraka kwa muumba. na kama una mume, jamaa amejaaliwa. hilo ni kutoka moyoni mwangu. una mtazamo ambao ni nadra kupatikana. and that's the fact.
dont ask me why..!!
almighty god keep you bleesed [emoji106][emoji106] !!

Ndivyo nilivyo mkuu,nimerithi hekima na busara za baba yangu kipenzi.
Nashukuru sana mkuu,ubarikiwe zaidi.
 
SEHEMU YA PILI


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden



bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa
 
Mods tafadhari fanyeni mpango iwe kama unaperuz kwa uc browse kama Uzi ni mrefu usomeke kwa uchache alafu kuwe na option ya click to expand. Asante
Sasa huyo uliye mquote ndiye mod???

Hivi mbona mna akili za mbuzi namna hii, tunalalamika msi nukuu uzi wote mnasababisha usumbufu.

Subirini dawa iko jikon, itakuwa una quote, unakula ban ya mwezi, mpaka mtaelewa somo.
 
The Bold, Mungu akuzidishie zaidi ya ulichonacho kwa kweli. Big Up bro.
 
Back
Top Bottom