Utasemaje kwa Kiswahili majina ya watu kutoka mataifa haya?

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Mtu wa Tanzania anaitwa Mtanzania. Je, wakutoka hapa wanaitwaje kwa Kiswahili sanifu?

1. Finland
2. Thailandi
3. Urugwai
4. India
5. Afughanistani

Kiswahili kina maneno mengi ambayo hayajajulikana na watu wengi.
 
Mtu wa Tanzania anaitwa Mtanzania. Je, wakutoka hapa wanaitwaje kwa Kiswahili sanifu?

1. Finland
2. Thailandi
3. Urugwai
4. India
5. Afughanistani

Kiswahili kina maneno mengi ambayo hayajajulikana na watu wengi.


Wafinishi
Wathailandi
Wauruguayi
Waindia
Waafghanistani
 
Wafinishi
Wathailandi
Wauruguayi
Waindia
Waafghanistani
Mkuu umesikika lakini bado. Japokuwa pia nimeuliza katika umoja. "Mtu huyu anaitwaje" ------- hata hivyo kidogo ungepatia "Mhindi" lakini ukafanya kosa la kisasa kwenye Kiswahili cha leo --- la kusema "apa" badala ya "hapa".
 
Hapa numekuelewa.
Ingawa sioni kama tunatakiwa kuhitimisha kwa kusema hakuna irabu 'u'.

Naona kilichotokea hapo ni kile wanachoita uyeyushaji ambapo neno 'Mwanamume' huenda na kua 'Mwanamme'
Hapana mkuu huo sio uyeyushaji bali ni udondoshaji.Uyeyushaji hutokea iwapo irabu zinazotamkiwa juu (u&i) zinapotokea kabla ya irabu zingine (a&e) mfano Mu (ngeli) katika mwanaume ilikuwa mu+anaume hivyo u+a ikawa w pia irabu i+a katika vi+ake inakuwa vyake.Hivyo mfano wako haupo umekosea kidogo.
 
Back
Top Bottom