Serikali yetu ianze kutoa tuzo kwa watunza (wazungumzaji) Kiswahili kutoka mataifa ya nje

Gadafhi

New Member
Apr 14, 2023
1
0
Ni ukweli usiopingika kwamba dunia nzima inatambua lugha ya Kiswahili ina unasaba mkubwa na Tanzania. Kwa tafsiri fupi ni kwamba Tanzania tunaweza kuiita ardhi ya Kiswahili.

Sasa nataka niongee kidogo kuhusu lugha hii adhimu na wizara yenye dhamana ya lugha hii kwamba lazima itumie mbinu mbadala ili kukiimarisha kiswahili katika ngazi za kidunia.

Maana yangu ni hii, wakati tunafanya royal tour na mengineyo inatakiwa pia tukitangaze kiswahili kwa uzito ili hata mtu akisikia kiswahili huko China, USA n.k basi moja kwa moja ajue hii ni lugha ya Tanzania kwa kufanya hivyo pia itaweza kuvutia utalii.

Juzi nimeona balozi wa Tanzania huko Uganda akitoa tuzo kwa wahifadhi wa kiswahili(at Makerere University) kitendo ambacho mimi nimekifurahia lakini bado unaona kasi ni ndogo ya kukitangaza Kiswahili.

Mfano South Africa kuna msanii anaitwa Sho Majodzi mwanadada huyu amekuwa akionyesha umahiri na juhudi kubwa za kuimba na kuongea kiswahili, je kama taifa tumefanya kitu gani kumtia moyo? Ilipaswa mtu kama huyu aitwe hapa nchini au kwenye ubalozi wetu huko kwao apewe tuzo ya heshima kwa kukienzi kiswahili. Kwa kufanya hivyo itaamsha na watu wengine duniani kwa kujiona kwamba kiswahili kinawathamanisha na kuwaheshimisha.

Tuliona hapa nyumbani yule masai Killy na dada yake taifa la India limewaheshimisha kutokana na wao kuimba zile nyimbo za kihindi sasa sisi watanzania tunakwama wapi katika kukikuza Kiswahili?

Wahusika liangalieni hili kwa maslahi mapana ya taifa maana tunatamani kuona kiswahili kikiongelewa hata na kina Rihana huko. Tuwafanye wageni wajisikie fahari na kujiona kuthaminiwa kwa kuongea Kiswahili.
 
Vipi wewe kwani wadhani kiswahili ni lugha ya Tanzania pekee famasiala nini
 
Attachments

  • Screenshot_20230515-123054.png
    Screenshot_20230515-123054.png
    40.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom