Utaratibu wa kuhama kwa Watumishi wa umma kwenye mashirika ya umma ukoje?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,908
Nimeuliza kwa faida ya mtu mwingine ambae amekuja kuniuliza akidhani najua kila kitu.

Je, kwa watumishi au mtumishi wa umma ambae anafanya kazi shirika au taasisi ya umma inayojitegemea akitaka kuhamia taasisi nyingine anafuata utaratibu upi?

Kwenye mtandao au kwenye tovuti ya utumishi inaongelea tu watumishi walioko tamisemi, kwa mkurugenzi wa halmashauri, katibu tawala ambao hawahusiki na utumishi kwenye mashirika au taasisi za umma.

Mfano mtu alieko NSSSF anataka kuhamia SUMATRA (latra) ama alieko nhif anataka kuhamia udsm.

Watu kama hao wanatakiaa kufuata utaratubu gani?

Natanguliza shukrani kwa majibu yenu.
 
Asante kwa swali zuri, mtumishi anayetaka kuhama tok taasisi moja Kwenda nyingine anatakiwe kwanza ahakikishe kule anakotaka Kwenda Kuna nafasi, na pia aandike barua kupiti mwajiri wake Kwenda anakotaka kuhamia ili kuomba kuhamia huko. Ndio utaratibu huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo tu mkuu? Akimaliza hapo anahamia moja kwa moja?
 
Akimaliza hapo, ile Barua yake aliyoiandika kwenda Taasisi X atajibiwa (coz alishaomba nafasi wakamruhusu!

Majibu yatatolewa kwa Maandishi (barua) kwenda kwa Mwombaji na Copy kwenda kwa Mwajiri.

Mwombaji ukishapata barua yako kutoka Taasisi X kuwa Umekubaliwa kuhamia... Utaandika Barua kwenda kwa KTB MKUU UTUMISHI ukimuomba kuhamia Taasisi X. Barua hii itapitia tena kwa Mkuu wako.

Safari hii barua hii itaambatana na ile ilotoka Taasisi X.

Pia barua hii itakuwa na ATTACHMENTS zingine zote zinazohusu UTUMISHI wako ukiweza weka na report ya UHAKIKI.

Barua hii unaweza kutuma kwa POSTA japo ni vzr uipeleke mwenyewe physically MTUMBA, MTAA WA SERIKALI au UTUMISHI UDOM. Kwenye barua yako usisahau kuweka sentensi hii: GHARAMA ZA UHAMISHO HUU NI JUU YANGU.

Utumishi wataingiza Maombi yako ktk mfumo wao wa kielektroniki na wewe utapata SMS kuwa maombi yako yamefika.

Muda wa kushughulikiwa maombi yako ni siku 21 na baada ya hapo ruksa kuanza kuulizia status ya Maombi yako.

Majibu yatatolewa kwa Maandishi (barua) kwenda kwa Mwombaji na Copy kwenda kwa Mwajiri...
Umeeleza vizuri sana aisee.

Swali la lingine ila sio la mwisho.

Report ya uhakiki anaitoa wapi? Je baada ya siku 21 inachukua miezi mingapi hadi apewe barua ya kuhama jumla kutoka kwa katibu mkuu?

Hizo attachment zinazomhusu mtumishi ni zipi?
 
Upo sahihi 100%, kwa kuongezea hizo siku 21 hazijumuishi siku za wkend, ni siku 21 za kazi ambazo kwa wastan ni kama wiki 4.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza vizuri sana aisee.

Swali la lingine ila sio la mwisho.

Report ya uhakiki anaitoa wapi? Je baada ya siku 21 inachukua miezi mingapi hadi apewe barua ya kuhama jumla kutoka kwa katibu mkuu?

Hizo attachment zinazomhusu mtumishi ni zipi?
Nakala la vyeti vya taaluma (kuanzia Sekondari, chuo n.k)
Barua ya ajira yako ya mwanzo na barua ya kuthibitishwa kazini kama ipo

Kwenda kwa KM Utumishi ambatanisha hizi:-
Nakala la vyeti vya taaluma (kuanzia Sekondari, chuo n.k). Barua ya ajira yako ya mwanzo na barua ya kuthibitishwa kazini kama ipo.

Bila kusahau ile barua yako uliyojibiwa kwamba nafasi ipo kule ulikoomba kuhamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenda kwa KM Utumishi ambatanisha hizi:-
Nakala la vyeti vya taaluma (kuanzia Sekondari, chuo n.k)
Barua ya ajira yako ya mwanzo na barua ya kuthibitishwa kazini kama ipo
Bila kusahau ile barua yako uliyojibiwa kwamba nafasi ipo kule ulikoomba kuhamia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa. Ngoja nimjulishe mhusika.

Maximum time hadi kujibiwa na katibu mkuu inachukua miezi mingapi mkuu kwa uzoefu wako.
 
Akimaliza hapo, ile Barua yake aliyoiandika kwenda Taasisi X atajibiwa (coz alishaomba nafasi wakamruhusu!

Majibu yatatolewa kwa Maandishi (barua) kwenda kwa Mwombaji na Copy kwenda kwa Mwajiri...
Mkuu Barua ya kuomba nafasi razima ipitie kwa mwajiri? Let say kuomba nafasi kutoka Halmashauri kwenda Taasisi X au Bodi X
 
Sawa. Ngoja nimjulishe mhusika.

Maximum time hadi kujibiwa na katibu mkuu inachukua miezi mingapi mkuu kwa uzoefu wako.
Hakuna formula this is Tanzania, zikipita siku 21 anza kufatilia.
Kwa kawaida barua ukipeleka mwenyewe jitahidi upate simu ya watu wa masjala uwe unafatilia kuanzia hapo au kama una mtu kule ndani basi mambo yako yataenda fasta ila kama ndio mwenzangu namimi kaa utulie tu inaweza kuchukua hata mwaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuepusha Matokeo hasi, watumishi wengi huanza kuongea na Mwajiri wake informa kuhusu dhamira ya kuhama, na kule unakotaka kuhamia pia unaenda kuongea kwa mdomo na Mwajiri. Akikubali ndio unaandika.

Back
Top Bottom