briophyta plantae
Member
- Feb 18, 2017
- 63
- 62
Na gari binafsi na pikipiki je?zinahusika kwenye huu utaratibu?UTARATIBU WA KUDAI FIDIA YA BIMA KWA ABIRIA ALIYEPATA AJALI
(CLAIM PROCEDURE)
Imeandikwa na BINTI MAKINI
0714351954
Abiria anapaswa kuandika barua kwenda kampuni husika ya bima iliyokatiwa hilo Bus. Katika barua hiyo aambatanishe vifuatavyo
1.TIKETI YA SAFARI.
2.CHETI CHA MATIBABU YA HOSPITALI.
3. FOMU YA POLISI (PF 3).
4. MCHANGANUO WA GARAMA ALIZOINGIA.
5. PF 90.
6. PF115
7. TIKETI YAKE kama bado anayo (kama imepotea kutokana na mazingira ya ajali itaeleweka haina shida sana).
Cha muhimu ni kwamba kama hakuzidiwa sana basi ahakikishe yeye mwenywe kuwa jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya polisi ya majeruhi kwa kutaja majina yake yote kamili.
8. Cheti cha kifo, ikiwa unadai kwa niaba ya ndugu aliyefariki katika ajali.
9. Hakikisha unaziwasilisha nyaraka hizi kwenye ofisi ya bima husika.
KUMBUKA: Utalipwa tu iwapo,ulipanda magari ambayo yaliyoruhusiwa kubeba abiria tu ndiyo (PSV) yaani Passenger Service Vehicles kama vile mabasi ya abiria,daladala, na taxih zilizosajiliwa.
NB: Kampuni ya bima ikikataa kulipa madai unayoona ni halali, wasilisha mgogoro wako katika ofisi za Msuluhishi wa Migoigoro ya Bima zilizopo PPF Tower Dar es salaam au ofisi ya Mamlaka ya Bima(TIRA) zilizpo nchi nzima
ELIMU YA BIMA IWAFIKIE WATU WOTE.
Mkuu tunashukuru kwa elimu hii,
hebu tusaidie kujua kazi ya bima ndogo(Third part) kwenye gari binafsi na comprehensive(Bima kubwa) kwenye gari binafsi pia
Duh kusema kweli nilikuwa silijui hili jambo mkuu asante kwa uzi huu.
Duh asee ni noma sana. Sasa mfano zile mwendo kasi ambazo zimekuwa designed watu wengi kusimama kuliko kukaa inakuaje mkuu?Bima inacover kwa idadi ya siti za gari hisika, daladala zinasimamisha, kwenye case ya namna hii receipt ni muhimu na ni first come first serve to the maximum number ya siti zilizokuwa insured.
Ulichelewa inakula kwako.
Duh asee ni noma sana. Sasa mfano zile mwendo kasi ambazo zimekuwa designed watu wengi kusimama kuliko kukaa inakuaje mkuu?
Bima mdogo (Third part):
Bima kubwa (Comprehensive):
- Kama umekata bima ya namna hii ukapata ajali, bima itahusika kumlipa yule uliyemgonga, awe mtu au uwe umegonga gari. Wewe mwenye bima hutalipwa isipokuwa yule uliyemsababishia madhara.
- Ukipata ajali kama una bima ya namna hii unalipwa wewe na yule uliyemgonga.
UTARATIBU WA KUDAI FIDIA YA BIMA KWA ABIRIA ALIYEPATA AJALI
(CLAIM PROCEDURE)
Imeandikwa na BINTI MAKINI
0714351954
Abiria anapaswa kuandika barua kwenda kampuni husika ya bima iliyokatiwa hilo Bus. Katika barua hiyo aambatanishe vifuatavyo
1.TIKETI YA SAFARI.
2.CHETI CHA MATIBABU YA HOSPITALI.
3. FOMU YA POLISI (PF 3).
4. MCHANGANUO WA GARAMA ALIZOINGIA.
5. PF 90.
6. PF115
7. TIKETI YAKE kama bado anayo (kama imepotea kutokana na mazingira ya ajali itaeleweka haina shida sana).
Cha muhimu ni kwamba kama hakuzidiwa sana basi ahakikishe yeye mwenywe kuwa jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya polisi ya majeruhi kwa kutaja majina yake yote kamili.
8. Cheti cha kifo, ikiwa unadai kwa niaba ya ndugu aliyefariki katika ajali.
9. Hakikisha unaziwasilisha nyaraka hizi kwenye ofisi ya bima husika.
KUMBUKA: Utalipwa tu iwapo,ulipanda magari ambayo yaliyoruhusiwa kubeba abiria tu ndiyo (PSV) yaani Passenger Service Vehicles kama vile mabasi ya abiria,daladala, na taxih zilizosajiliwa.
NB: Kampuni ya bima ikikataa kulipa madai unayoona ni halali, wasilisha mgogoro wako katika ofisi za Msuluhishi wa Migoigoro ya Bima zilizopo PPF Tower Dar es salaam au ofisi ya Mamlaka ya Bima(TIRA) zilizpo nchi nzima
ELIMU YA BIMA IWAFIKIE WATU WOTE.
Ombeni kampuni ya bima iunganishwe kwenye kesi alafu mahakama itaamua.